Wafariki kwa kufunikwa na mlima –Same | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafariki kwa kufunikwa na mlima –Same

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  IDADI ya watu ambao bado haijafamika wamekufa baada ya kufunikwa na mlima uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea usiku wa kuamkia leo huko kata ya Manka Wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Msiba huo umetokea baada ya mlima mmoja kumeguka na kufunika zaidi ya nyumba kumi na inadaiwa watu wote waliokuwa wamelala ndani, wamepoteza maisha kufuatia tukio hilo na kudaiwa nyumba hizo zimesombwa kwa maji hayo.

  Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika majira ya saa 7:00 usiku, katika kata ya Miamba kitongoji cha Manka wilayani Same.

  Maafa hayo yametokana na mvua zilizonyesha mfululizo kwa siku tatu na kusababisha mlima huo kumeguka.

  Na mvua huzo kubwa zimekuwa zikinyesha kwa siku tatu mfululizo katika majira ya usiku tu, hali hiyo imesababisha udongo na miamba kumeguka na kufunika nyumba kumi katika kitongoji cha Manka, huku watu wakiwa wamelala ndani.

  Imedaiwa katika juhudi za kuwaokoa katika nyumba hizo hakuna mtu ambaye ameokolewa akiwa hai.
  Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango amesema kuwa hadi sasa miili kumi na moja imeshatolewa chini ya kifusi na juhudi zaidi zinaendelea kuokoa miili hiyo.

  Amesema hali ya uokoaji inakuwa ngumu kutokana na nyumba hizo kuwa chini ya milimani ambako sio rahisi kufikika kwa vyombo vya uokoaji.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3523422&&Cat=1
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Rais atoa rambirambi, na kutoa tahadhari kwa wakuu wa mikoa

  RAIS Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, kufuatia vifo vya watu 25 vilivyosababishwa na kuporomoka kwa ardhi na kufukikwa na kifusi cha mlima.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, iliyotolewa kwa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete amemweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa amepokea habari za vifo vya watu hao kwa huzuni na majonzi makubwa.


  "Nimepokea kwa huzuni kubwa na majonzi mengi habari za vifo vya watu 25 katika ajali hiyo ya maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku nne mfululizo katika Wilaya ya Same. Kwa hakika, nimesikitishwa sana na upotevu huo wa maisha," alisema Rais Kikwete


  "Napenda kwa dhati kabisa kutoa pole kwako wewe Mkuu wa Mkoa, na kupitia kwako, kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu wote 25 ambao maisha yao yamepotea katika maporomoko hayo ya ardhi."


  "Moyo wangu uko na familia zilizopoteza wapendwa wao. Nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo," alisema.


  Alisisitiza: "Vile vile nawaombea waliojeruhiwa katika maporomoko hayo wapone haraka, ili warejee katika shughuli za maisha yao ya kawaida."


  Rais alitumia nafasi hiyo, kutoa maelekezo kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nchini kuchukua tahadhari na hatua za haraka kujiandaa kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea katika sehemu nyingine nchini kutokana na mvua za vuli na masika zilizoanza kunyesha katika baadhi ya mikoa nchini.


  "Nachukua nafasi hii pia kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuchukua kila aina ya hatua na tahadhari kujiandaa kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea kutokana na mvua za vuli, na katika baadhi ya mikoa mvua ndefu, zilizoanza kunyesha katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu," alisema.


  Wakazi hao wa Kijiji cha Manka, Kata ya Miamba, Tarafa ya Mamba, wilayani hapa, wamepoteza maisha kufuatia siku nne za mvua mfululizo iliyosababisha maporomoko ya ardhi na watu hao kufunikwa na kifusi katika eneo hilo la milimani.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3538846&&Cat=1
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Waliofunikwa kwa mlima wazikwa leo
  Miili ya watu 20 walioopolewa jana, katika tukio la kufunikwa na kifusi cha mlima kwenye kitongoji cha Mamba, Kijiji cha Goha, Kata ya Myamba, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wamezikwa leo.
  Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Bw. Ibrahim Marwa, imesema kuwa mazishi hayo yamekamilika na kugharamiwa na serikali.

  Katika mazishi hayo ibada ya kuombea marehemu imefanyika kwa pamoja na kisha kila mwili kuzikwa katika kaburi lake.


  Amesema katika juhudi za kuokoa miili hiyo tokea tukio hilo litokee u siku wea kuamkia jana umepata idadi ya miili 20 hadi kufikia jana usiki na hiyo ndiyo imezikwa leo na zoezi la kuokoa miili mingine inaendelea.


  Amesema zoezi hilo linafanywa na kikosi cha watalaam kutoka wilayani wakishirikiana na askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia (F.F.U).


  Hata hivyo amesema baada ya shughuli ya uopoaji wa maiti, kutafanyika uchunguzi wa kina kubaini sababu zilizosababisha maporomoko hayo ya milima.


  Amesema hawajaridhika na sababu moja ya maji tu ambayo yanaweza kusababisha maporomoko hayo, "tutawaleta wataalam wa miamba ili waweze kufanya uchunguzi zaidi kubaini sababu hasa zilizosababisha maporomoko hayo"


  Katika tukio hilo watu zaidi 25 wamehofiwa kufariki dunia kwa kufunikwa na kifusi cha udongo, kilichotokea baada ya nyumba saba walizokuwa wakiishi kufunikwa na tope baada ya mlima kumeguka kutokana na mvua kumbwa kunyesha wilayani humo.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3532098&&Cat=1
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mbwa wahitajika zoezi la kutafuta miili- Same
  [​IMG]
  Friday, November 13, 2009 10:45 AM
  BAADA ya zoezi la kukamilika kwa kuzikwa kwa miili 20 iliyopatikana kwa kufunikwa na mlima, Serikali imeombwa kupeleka mbwa wa kunusa ili kusaidia kutafuta maiti nyingine ambao hazijapatikana.
  Inadaiwa kuwa maiti nyingine zaidi ya tano bado hazijapatikana na zoezi hilo kuwa gumu kwa kuwa maiti hizo zilifunikwa na tope baada yam lima huo kuporomoka.


  Jumla ya nyumba saba zilifunikwa katika maporomoko hayo na watu wote waliokuwamo katika nyumba hizo usiku wa manane wa kuamkia juzi walikufa.


  Ombi la kuomba kikosi cha mbwa, lilitolewa jana na Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa maelezo kwamba, juhudi pekee za wananchi hazitafanikiwa kupata miili iliyosalia bila kuopolewa.


  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega, aliwataka wananchi kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari kwa hali yoyote isiyokuwa ya kawaida katika eneo hilo na kuripoti maramoja.


  Katika tukio hilo walioopolewa kati yao kulikuwa na mama wajawazito wawili na miili ya vichanga hivyo vilitolewa tumboni mwa mama zao na kuzikwa tofauti, ambapo mama mmoja aliyefariki alishatimiza mimba ya miezi tisa.


  Maiti zilizotambuliwa na kuzikwa ni pamoja na Neema Shambi (70), Napenda Bakari (7), Namsemba Bakari (11), Sikudhani Elitabu (20), Nath John (12), Haika Charles (3) na Mariam Juma (4), Wemaeli Mhina (30), Ruth Mhina (6), Neema Bakari (8) na Christina Kiondo (32).


  Mingine ni Elitabu Shambi (30), Shambi Elineema (11), Ndimangwa Elineema (5), Amani Mhina (9), Kiondo Amani (37), Imani Kiondo (9) na Nikundiwe Kiondo (5), wote wakazi wa Goha.  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3539810&&Cat=1
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,436
  Trophy Points: 280
  huyo rais mwenyewe hajawahi kufika huko toka azaliwe..nyerere ndiye aliyewahi kufika pale akakuta watu wote ni wafupi
   
Loading...