Wafanyakazi wote wa TAKUKURU watakiwa kuwasilisha vielelezo vya mali wanazomiliki

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Waziri Angellah Kairuki awataka wafanyakazi wote wa TAKUKURU kuwasilisha vielelezo vya mali wanazomiliki; aonya kuhusu udanganyifu.
============

Waziri wa Nchi, Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ina baadhi ya watendaji wametumia nafasi zao vibaya na kufanya chombo hicho kukosa uaminifu hivyo na kufanya chombo hicho kuwa na ‘majipu’ ambayo yanatakiwa kupasuliwa.

Angela ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa utendaji kazi wa Takukuru uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema chombo hicho ni muhimu lakini kuna baadhi wametumia nafasi zao vibaya katika kufanya kazi na taarifa anazo hivyo atashughulikia ikiwemo na kuandika kiapo cha mali zao na kama walifanya warudie kujiridhisha.

Amesema kuwa Takukuru inatakiwa kufika wilayani na mikoani kutokana na fedha nyingi za miradi ya serikali zinakwenda huko ambapo ameutaja mkoa wa Kilimanjaro unawatendaji ambao wametumia madaraka vibaya wa ubadhirifu wa fedha za serikali hivyo Takukuru lazima ichukue hatua dhidi yao.
Amesema kuwa ikitokea kuwepo na kutowajibika kwa chombo hicho serikali iamweza kuwandoa wote kutokana na kuwepo kwa watu wenye sifa wa kufanya kazi hiyo.

Aliongeza kuwa katika Takukuru inatakiwa kujiridhisha na uchunguzi na sio kuwa idadi nyingi za kesi ambazo mwisho wa siku kesi hizo wanashindwa kutokana kuushindwa kuwa na uchunguzi wenye ushahidi.

Aidha amesema kuwa baadhi ya mahakimu watakosa kazi kutokana na baadhi ya kesi wameendesha kwa kupindisha na kuwapa washitakiwa haki wasio kuwa nayo.

Waziri Angela amesemaTakukuru wafanye kazi kwa waadilifu kwa kuwalinda watoa taarifa ili waendelee kutoa taarifa kwa watu wanaojua kuwa wanahujumu nchi kwa kutumia madaraka yao.

Amesema watumishi wa Takukuru wana masilahi mazuri kuliko wa wafanye kazi wengine ikiwa ni kuwaondoa katika ushawishi wa kuwa na tama kutokana unyeti wa chombo hicho.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina (CP), Valentino Mlowola amesema wameokoa sh. Bilioni Saba (7) ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa masilahi yao.

Amesema walipokea malalamiko 4,675, uchunguzi uliokamilika wa majalada hayo ni 667, majalada yaliyokwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), ni 278, majarada yaliyorejeshwa na DPP, ni 172 kwa ajili ya vibali vya kufungua mashitaka na kesi mpya 314 nchini kote, na kesi zilizoshinda 132 ambao wamefungwa na wengine kulipa faini.


Chanzo: Michuzi
 
Kazi ndo imeanza, Magufuli alisema "Nawapa Muda mawaziri wangu, na mimi nipeni muda"

Naona sasa Mawaziri wameamka, maana Magufuli hana cha waziri wala nini...!
 
Bungeni nako wasikose, akina Chenge hadi wang'oke tu! Bunge sio chaka la mafisadi.

Wanaotakiwa kupitia na kuchukulia hatua fomu za malizao ambao hawajafanya chochote kutokana na mali za wizi ni majibu.
 
Kuna mfanyakazi wa TAKUKURU namfahamu na magari anayomiliki sijui kama ataandika ukweli
 
Mali wanazomiliki
VIELELEZO.

Hivyo vitu viwili vinashabahiana lakini vina uzito tofauti. Unaweza kutaja mali unazomiliki tena unaweza kukuta ni za halali kabisa. Ila ukiambiwa lete VIELELEZO, hapo ndipo tatizo linapoanza
 
Hatofanikiwa, maana mali zitafichwa. Angewafanyia upelelezi bila wao kujua, kisha ndo akatangaza. Lkn kwa sasa atadanganywa
 
Bungeni nako wasikose, akina Chenge hadi wang'oke tu! Bunge sio chaka la mafisadi.

Wanaotakiwa kupitia na kuchukulia hatua fomu za malizao ambao hawajafanya chochote kutokana na mali za wizi ni majibu.
Chenge hakamatiki. We umesahau kama alienda mahakamani kupinga tume ya maadili kumhoji? Kwani walimfanya nn?
 
Hili ni jambo la kimaadili, Je? Aliye towa hayo maagizo naye ni muadilifu kiasi gani?
Zisiwe hadithi za samaki akimla binadamu ni ishu ila binadamu akimla samaki siyo ishu.
 
Hahahaa eti jizi andamizi jk watu wa jf mnavituko

Kwani uongo mkuu, hukuona mitoto yake ilivyokuwa inafurahi CCM iliposhinda, ilifikiri itaendelea kunyonya majasho ya wanyonge ambao hawakuwa na na njia mbadala zaidi ya kutaka kuing'oa CCM.
 
Waziri wa Utawala Bora, Angela Kairuki, ameagiza watumishi wote wa TAKUKURU waorodhoshe mali zao mara moja. Kwa maagizo yake, atakayedanganya na akabainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria
 
Kama kawaida yao kila cku comedy ufisadi tz umekua jambo la kawaida .....wizara ya mambo ya ndani ndio no 1 kwa rushwa hilo liko wazi
 
Waziri wa Utawala Bora, Angela Kairuki, ameagiza watumishi wote wa TAKUKURU waorodhoshe mali zao mara moja. Kwa maagizo yake, atakayedanganya na akabainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria
Hilo halina Shida kwani wengi mali zao wamezificha kwa majina ya ndugu jamaa na marafiki Kama walivyofanya watu wa TRA , mfano yule Afisa wa TRA wa Temeke ambaye alihamia huko toka TRA mwenge Gasper Mhina anamiliki nyumba nyingi kuliko Masamaki lakini kaficha kwa majina ya siri na kile kikundi chake cha wachina na wahindi anaowasaidia kukwepa Kodi nao wanamlinda kwa syle zote hata Takukuru wakienda wanashindwa pa kumnasa ni mjanja kuliko Maelezo.
 
Mali zake utaonyeshwa kidogo sana mara nyingi watangaza mali huwa wanaficha nyingi.
 
Back
Top Bottom