Wafanyakazi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wafungiwa nje

Hivi kwa nini kila tukio linalofanyika waandishi wa habari huwa tayari wapo.....!? Kweli intelijensia ya media za bongo kiboko, wanajua hadi kile waziri anachokusudia kufanya siku inayofuata tena akikipanga akiwa chumbani mwake....!? Tutaona mengi mwaka huu.

Acheni waandishi wa habari wafanye kazi. Tena ingekuwa bora zaidi kama jerry m. Angekuwepo kwa kipind kama hiki.
 
kigwangala endelea kuwafungia mageti mpaka wakome,mlizoea kufanya kazi kwa mazoea sio, unaripoti ofisini saa 3 umechelewa hakuna wa kukuuliza na bado
 
Frankly speaking Dar inatakiwa ipewe special attention ikiwezekana muda wa kazi uanze saa 3 (tatu). Halafu siku hizi viongozi wameanzisha kamtindo, wakiona foleni ni kubwa huwa wanapita barabara ya upande wa kulia (kwa mfano maeneo ya kutoka Morocco hadi Salender Bridge na maeneo mengine mtindo wa viongozi na wanajeshi ni huo huo) wakati mfanyakazi amesota pale kwa saa nzima. Huyu ndiye anawahi kukufungia wafanyakazi nje wakati mtu ametoka home saa 11 alfajiri ila tatizo ni infrastructure mbovu; it is not fair.

Kwa wale wa maeneo ya Kimara na Mbezi wenye mamlaka wamegeuza barabara ya mwendo kasi ndio njia zao za kutanulia wakati wengine hawaruhusiwi kukanyaga humo na daladala ikikamatwa faini ni laki 1. Hebu tuweke mazingira yawe fair kwa wote ili tuwe na just and fair judgement.
Watanzania wengi ni wapvmbavu na wanashindwa kuendana na kasi ya rais kama wewe! Saa tatu? Hivi kwa akili za watanzania wengi unafikiri ndo utatatua tatizo? Kama saa tatu wengi wataondoka nyumbani saa mbili!
Hii spidi ya Maguguli wataizoea tu, hawawezi, waache kazi sababu kuna watu kibao mitaani wana uwezo wa kufanya hizo kazi na sifa wanazo!
Kama unatakiwa kureport saa moja, ondoka kwako mapema zaidi asubuhi, hamnaga foleni na unawahi, huo ndo ukweli! Mfano: Kwa mkazi wa Segerea anayefanya kazi city center Dar, ukiondoka kumi na moja asubuhi huwezi chelewa mjini! Tena kwa usafiri wa daladala, naongea kwa experience!
 
Leo Dr Kigwangala amewafungia geti watumishi wa wizara ya afya waliochelewa kufika kazini , kwa mtizamo wangu hizo ni minor issue zinazotakiwa kuwa taken care na afisa utumishi au human Resource Manager, yeye angetoa directives kwa watumishi wote kuhusu umuhimu/ulazima wa kuwahi kazini na atakayekiuka anataka taarifa za hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao kutoka kwa Human Resource Manager, Naibu Waziri ana mambo mengi makubwa ya kitaifa ya kushughulikia, siyo kukimbizana na staff waliochelewa kazini, nahisi kama kama kwenye kozi yake ya udaktari,MD na Master of Public Health, MPH aliyonayo kama hakusoma mambo ya Leadership and Management kwenye somo la Development studies.

Hao uliowataja wote wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kulea uzembe ambao naibu waziri kauona.Wangekuwa wachapa kazi uzembe aliouona naibu waziri usingeonekana.Hao na ni majipu ya kutumbua waondoke wapishe wengine washike hivyo vyeo vyao.

Hayo mambo makubwa ya kitaifa ya afya unayosema yanafanywa si na waziri tu bali na hao wafanyakazi wa wizara pia.Kuchelewa kwao ina maana wanachelewa kufanya mambo ya kitaifa yahusuyo tiba kwenye vitengo vyao
 
Wavivu utawajua tu! Lzma ilalamike
Shnz typ nyie mlishazoea kuingia kazini saa nne asubuhi. ...pumb@--f zenu
 
Waandishi wa habari na kamera kibao wamejuaje kwamba atawafungia nje duh haya bana mwendo wa kushtukiza...nazani hiyo si kazi ya Naibu Waziri ni kazi ya Afisa Utumishi na Utawala kazi ya Naibu Waziri ni masuala ya kisera kama kuhakikisha MADAWA yanapelekwe mahosptalini na hosptali za rufaa zinaongezeka zikiwa na huduma stahiki si rufaa jina...ila pia si kila kitu kiitiwe waandshi wa habari ilitosha Naibu Waziri afanye kimya kimya tusiforce popularity
 
Hoja za kijinga zinajibiwa kijinga vile vile. Wale wanahoji kwamba walipoomba kazi hawakujua kama Dar kuna foleni? Na wao wajiulize Magufuli aliposema kwamba taifa linapoteza mabilioni ya fedha kutokana na foleni za Dar, alikuwa kachanganyikiwa? Hivi Kikwete aliposema kwamba foleni za dar ni dalili kwamba nchi imeendelea hakujua hayo "Maendeleo" yanaleta hasara alizosema Magufuli?

Mimi nina ndugu yangu anakaa Kibamba anafanya kazi mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji, ili awahi kazini kwake, tena kwa kutumia usafiri wake binafsi huamka saa kumi alfajiri na saa kumi na moja Alfajiri ni lazima awe ameshakuwa barabarani ili afike kazini kwake saa mbili asubuhi. Huyo Kigwangala Hakumsikia Magufuli alipokuwa anaomba kura aliposema kwamba anataka kujenga Flyovers na kutumia usafiri wa Boti ili watu wawahi kazini, hizo ahadi zimeshatekelezwa? Aache sifa za kijinga!!

Waliwahi na kufunga hayo mageti leo wamefika kazini na ungo?
Watangazaji wanaoendesha vipindi vya redioni vya saa kumi na moja alfajiri wanalala studio?
 
Umesema kweli. Hakuchaguliwa kukagua mahudhurio.Cha msingi ni kutoa maelekezo kwa human resource manager kuhusu watu kuwahi.
Akazania kuboresha huduma katika Taasisi ya saratani Ocean Road.Sera ya serikali ni kuwapa huduma bure wahanga wote wa saratani ila huduma za mionzi na chemo ni hafifu sana.
Aache mbwembwe za masuala yasiyo na msingi.

HR mwenyewe kafika saa 4asbh
 
Leo Dr Kigwangala amewafungia geti watumishi wa wizara ya afya waliochelewa kufika kazini , kwa mtizamo wangu hizo ni minor issue zinazotakiwa kuwa taken care na afisa utumishi au human Resource Manager, yeye angetoa directives kwa watumishi wote kuhusu umuhimu/ulazima wa kuwahi kazini na atakayekiuka anataka taarifa za hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao kutoka kwa Human Resource Manager, Naibu Waziri ana mambo mengi makubwa ya kitaifa ya kushughulikia, siyo kukimbizana na staff waliochelewa kazini, nahisi kama kama kwenye kozi yake ya udaktari,MD na Master of Public Health, MPH aliyonayo kama hakusoma mambo ya Leadership and Management kwenye somo la Development studies.
Kama uwezi kuwai acha kazi.
 
Vizuri sana

Wamekuwa wavivu wengi wao

Nimependa hii, kama hawawezi kuwahi kazini wawaachie wanaoweza wachukue kazi zao.
 
Wavivu utawajua tu! Lzma ilalamike
Shnz typ nyie mlishazoea kuingia kazini saa nne asubuhi. ...pumb@--f zenu

Unafananisha MTU anayepewa gari na nyumba, na yule aliyepanga maji matitu? Si kila anayechelewa amependa kuchelewa
 
CWgVBQHWcAAoeWs.jpg
 
we inaonekana unaishi vijijini na hujaajiriwa foleni ya daq unaijua vizuri kweli?

Nadhani kwenye mikataba yao hawakuambatanisha na barua inayosema watakuwa wanachelewa kufika kazini kutokana na foleni.
Usitete ujinga. Mbona wa private wanawahi
 
Back
Top Bottom