Wafanyakazi Wengi Hawapendi Kazi Zao

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wana JF.Tunatumia theluthi ya maisha yetu yote duniani tukiwa kazini ni sawa na saa 90000 za ukadirio wa muda katika maisha yetu yote.

Tafiti zinaonesha asilimia 85%ya wafanyakazi duniani hawapendi kazi zao hawaoni umuhimu wowote wa kazi Ila hufanya tu kwasababu hakuna namna.

Je ni nini kinafanya wachukie kazi zao?

1. Boss (Mkubwa wa Kazi):
Boss ama mkubwa wa kazi ni moja kati ya sababu kubwa ya wafanyakazi kuchukia kazi zao. Ma boss wengi hawajui kuongoza wafanyakazi wao huwakaripikia na kuwawajibisha kwa kila kosa linalotokea katika kazi pasi kujua makosa ni kawaida kwa binadamu.

2. Aina ya kazi:
Aina ya kazi huwanyima furaha wafanyakazi.Wakati mwingine huna jinsi na unashindwa kuchagua kazi kutokana na kuwa unahitaji uingize mkono kinywani hakuna namna hautachagua utafanya yeyote.Kwa mfano Boss anakwambia anakupa kazi ya kuosha mbwa hutaipenda Ila itabidi ukubali ili upate chochote.

3. Maelewano na wafanyakazi wenza:
Wakati mwingine uhusiano wa mtu na wafanyakazi wenza inaweza kuwa sababu ya wewe kuichukia kazi kazini lazima kuna kupishana nauli kwasababu wapo wenye uzoefu na wengine wana uzoefu kidogo.

Lakini Je Unajiuliza ni Kwanini Hawaachi Hizo Kazi?

Wanashidwa kuacha hizo kazi kwasababu zifuatazo

1. Ugumu wa kupata kazi:
Kupata kazi nyingine ni ngumu hasa katika wakati huu ambao ajira zimekuwa za shida kutokana na ongezeko la wanaohitaji ajira tofauti na kipindi cha nyuma ambapo waajiriwa walikuwa wachache.

2.Kufungwa na mkataba:
Mikataba na makubaliano yake huwa na masharti magumu hivyo wakati mwingine huwafunga kutafuta kazi nyingine au hata huwa ya muda mfupi ambao ni muda usiotosha kwa mtu kujiaanda vyema kuwa na kazi nyingine au kujitegemea.

3. Majukumu waliyonayo:
Kutokana na majukumu waliyonayo waajiriwa inakuwa ngumu kwa kuacha kazi wasizopenda mfano ulipaji wa bill,ulipaji wa ada za watoto n.k.
Hivyo wanahisi pindi watakapoacha itakuwa ngumu kwao kuyamudu majukumu yao.

4. Uwoga wa kufail:
Waajiriwa wengi hushindwa kuziacha kazi zao wasizozipenda kwa kuwa wana uoga wa kuamua kwa kuogopa Ku fail endapo watajiajiri wao wenyewe au endapo watatafuta kazi zingine na wakashindwa kuzifanya kikamilifu.

5. Mshahara mzuri:
Wakati mwingine Unaweza kuwa huipendi kazi lakini ndiyo inayokulipa mshahara mzuri itakubidi uvumiliane na kila kitu na uifanye hivyo hivyo.

Kwa mfano unapenda kazi ya Benki Ila itakulipa mshahara wa 600000kwa mwezi na Boss mmoja amekuajiri kama Mhasibu wake wa duka na anakulipa 1000000 kwa mwezi.

Japokuwa hupendi kuwa mhasibu wa mtu ila kwasababu ya mshahara mzuri itakubidi ufanye.
 
Screenshot_20200918-222736.jpg
 
Back
Top Bottom