Wafanyakazi watatu TANESCO Watiwa Mbaroni Kufuatia Kifo cha Mfanyakazi Mwenzao Aliyenaswa na Umeme

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,399
2,000
Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Morogoro, wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa kutokana na kifo cha mfanyakazi mwenzao, Deo Elias (30), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa kunaswa na umeme juu ya nguzo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 asubuhi maeneo ya Mafiga, wakati Elias akiwa na wafanyakazi wenzake katika eneo la kazi.

Kamanda Matei alisema Elias alipokuwa na wenzake katika eneo hilo wakirekebisha umeme, alinaswa na kufa papo hapo.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi John Bandiye akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, alisema Elias alikuwa katika kazi za kawaida kama fundi na tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya.

Mhandisi Bandiye alisema mfanyakazi huyo alikuwa akirekebisha njia ya umeme ya Ngazengwa iliyopo eneo la Mafiga na ilikuwa imezimwa, lakini cha kushangazwa ilikuwa na umeme uliosababisha kifo chake.

“Kwa sasa shirika lina wafanyakzi wa muda wanaosaidiana na mafundi wakuu na hupatiwa mafunzo na wanatambulika, tofauti na maneno yaliyozagaa mitaani kuwa marehemu hakuwa mfanyakazi,” alisema.

Alisema mwili wake umesafirishwa kwenda kwao mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko.

Awali, Fundi wa TANESCO Morogoro, Deo Elias (30) mkazi wa Mazimbu Road ,alifariki dunia kwa kupigwa shoti ya umeme na kuungua wakati akifanya matengenezo ya laini kubwa ya umeme ya 11 KV katika eneo la Mafiga, Manispaa ya Morogoro.
4c0e15be-7096-44a1-bfa8-2b6656ce24e3.jpg
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,712
2,000
Poleni wafiwa,

Wajitahidi kuwa na mitambo ya kuhakiki kama kuna umeme kabla ya kuushika ingawa ni ajali ya kizembe au bahati mbaya only God knows
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,745
2,000
Usikute walimuwekea mtego, kama umeme ulikuwa umekatwa iweje mtu afe, polisi endeleeni kuwahoji hao vizuri mpaka watoe majibu yanayoeleweka
 

kalimaksi

Senior Member
Aug 18, 2014
127
195
We actually having a problem with most goverment organisations especially Tanesco!! In most department they work under memo recognitions ,,no matter how early and in need someone is!!! Notable example The main head quarter Rombo district!! Ni jipu!! Were is magufuli plz
 

asmaa80

JF-Expert Member
May 11, 2010
1,563
2,000
Usikute walimuwekea mtego, kama umeme ulikuwa umekatwa iweje mtu afe, polisi endeleeni kuwahoji hao vizuri mpaka watoe majipu yanayoeleweka
Kumuwekea mtego sio Rais ila kuna hiki kitu kinaitwa "UZEMBE" Ni kibaya sana, usiku kuna mtu aliuwasha bila kuwasiliana na wenzake site. dah inauma sana kijana mdogo sana.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
156,288
2,000
Bima itahusika na malipo na fidia lakini kama marehemu alikuwa kakatiwa bima
 

Bonesmen

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
932
1,000
Huyo meneja hio tittle ya muandisii ni sahihi kweli kaka? yani technical problem analichambua kama anaelezea siasa? eti ni bahati mbaya na kingine anadai line ilizimwa but wameshakaa kukuta umeme na kumpiga fundi aliepanda kweli? Hebu tupeni CV ya huyu meneja kwanza kabla hatujaanza kumlaumu kwa majibu yake mepesi ivo ...labda ni chambue safety gear na precautions ambazo zilipaswa kufatwa hapo na kwa vile hazikufatwa ndo maana imetokea hio ajali ya short circuit walau ingekuwa kuanguka kwa nguzo au kukatika mkanda au kuteleza kwa gefu but kwa vile ni short 100% pana uzembe apo Kwanini nasema ivo matengenezo ya umeme wa msongo wa kati yani medium voltage yani sheria zake formen ana play part huku linesmen nao wakicheza part zao kuhakikisha usalama upo tena mkubwa ,Kwanza ili line iwe dead yani haina umeme lazima Mafundi wahakikishe Substations au Load breaker ya iyo line imezimwa. na hio sehemu kufungwa na funguo kukabiziwa mafundi na anaepanda juu anatapanda na hio master key ya hio feeder anayoenda kuifanyia matengenezo kuzima peke hakutoshi kusema line iko dead hapo lazima tutest phase zote kama zina umeme au lah kwani unaweza zima mtu akawasha ka generator kake na kacharge line full kwa kupitia ktk transformer sasa tukitest line na kuhakikisha iko dead basi haitoshi pia tunafunga Earthing kila phase lazima tui ground yani hata atokee mlevi hapo sub awashe basi lineman hafikiwi na umeme coz phase zote zimezikwa ardhini hapo sasa ni salama kwa lineman kupanda juu kwa kuendelea na matengenezo shida ya Tanesco ni kufanya kazi kwa mazoea tu yani hakuna weledi tukichambua zaidi ata ndugu yetu marehemu ana makosa but wenzangu wa dini wanadai ni vibaya kumlaumu marehemu anyway Tuwe makini hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya ni uzembe tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom