Wafanyakazi watano wa TPA na CRDB wafikishwa Mahakamani kwa Kuhujumu Uchumi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Benki ya CRDB wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashitaka 28, likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya Sh bilioni 5.1.

Wafanyakazi wa TPA ni Valentine Sangawe (40) ambaye ni mhasibu, na makarani wawili Leticia Massaro (33) na Christina Temu (37), wakati wale wa Benki ya CRDB ni Eva Vicent (33) na Joseph Ndulu. Washitakiwa wote walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali, Faraji Ngukah alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 28, likiwemo la kugushi nyaraka ambazo ni risiti za malipo wakionesha ni halali zilizotolewa katika mfumo wa malipo wa TPA.

Mashitaka mengine ni ya wizi kuisababishia TPA hasara ya Sh 1,119,839,78.28 na kutakatisha Sh 5,119,839,758.28.

Ilidaiwa mahakamani kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Julai mwaka 2014 hadi Aprili mwaka 2015 katika maeneo ya jijini Dar es Salaam, ikiwemo bandari kavu ya TRH.

Ilidaiwa kwamba kati ya Julai 2014 na Mei 2015, maeneo ya bandari kavu ya TRH jijini Dar es Salaam, washitakiwa kwa pamoja walisababishia TPA hasara ya Sh 1,119,839,78.28. Pia alidai kuwa washitakiwa wakiwa watumishi waliiba Sh bilioni 5.1.

Katika mashitaka ya tatu hadi 13, mshitakiwa Sangawe anadaiwa alighushi nyaraka akionesha kuwa Kampuni ya Smart Clearing & Forwarding iliilipa TPA kupitia Benki ya CRDB wakati akijua si kweli.

Katika mashitaka ya 14 hadi 15 ya kughushi ambayo yanamkabili Massaro, Temu wanakabiliwa na mashitaka saba ya kughushi nyaraka mbalimbali. Ngukah alidai Januari 21, 2015 na Januari 22, mwaka huo Vicent aliiba Sh 14,801,238 mali ya TPA.

Pia inadaiwa kati ya Oktoba 30, 2014 na Novemba Mosi 2014, washitakiwa Sangawe, Ndulu na Temu walitengeneza nyaraka za uongo yenye thamani ya Sh 39,992,142.69 kuonesha Kampuni ya Smart imelipa fedha hiyo kwa TPA kupitia Benki ya CRDB wakati si kweli.

Mshitakiwa Ndulu anadaiwa Septemba 29, 2014 na Oktoba 13, 2014 mwaka huo alijipatia Dola za Marekani 8,717.69 mali ya TPA.

Washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa walitakatisha Sh bilioni 5.1 wakati wakifahamu kuwa fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na uliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshitakiwa Temu alidai kesi hiyo si mgeni, kwani walishitakiwa tangu Desemba mwaka jana na kwamba upelelezi wa kesi hiyo ulianza tangu 2015.

Alidai yeye ni mama ambaye ameacha familia akiwemo mtoto wa mwaka mmoja, na amesimamishwa kazi hivyo hana kipato chochote anachoingiza hali inayosababisha maisha ya watoto wake kuwa magumu.

Hakimu Shaidi aliutaka upande wa mashitaka, kushughulikia malalamiko ya washitakiwa, kwani wao ni binadamu kama wengine na haipendezi kusikiliza malalamiko kila siku.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 23, mwaka huu itakapotajwa.

Washitakiwa walirudishwa rumande, kwa kuwa mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Chanzo: Habari Leo

Zaidi, soma:
Tuhuma zilizowekwa JF kuhusu wizi huu wa watumishi wa TPA na CRDB
 
Dah Leticia Mungu awafanyie wepesi maana hii case imemsumbua sana 2015 hadi sasa ni mda mrefu sana
 
Mungu amfanyie wepesi mwizi? Unajua kadhulumu haki za wangapi kwa kuiba?
Mkuuu..anaweza akawa hata hajahusika directly...haya Mambo we waache TU...
Kuna Watu wanafanya yao..huko alafu Wewe huna hili Wala lile umesign document...ukijua Ni halali..unaishia kukaa jela Miaka 5ukisubiria kesi iishe.
 
Kwa bandari nakataa, nawajua vizuri sana watu wa huko. Ingekuwa sehemu nyingine ningekubali hilo laweza kutokea
Mkuuu..anaweza akawa hata hajahusika directly...haya Mambo we waache TU...
Kuna Watu wanafanya yao..huko alafu Wewe huna hili Wala lile umesign document...ukijua Ni halali..unaishia kukaa jela Miaka 5ukisubiria kesi iishe.
 
Unasumbuliwa na wivu na chuki dhidi ya watu wenye majina kama hayo, aliye juu atabaki juu tu tuhuma haziwez kuwashusha
Mkuu mbona umetoa povu sana. Wivu kisa wameiba ama inakuwa je Dada.
Ni nani aliyekuambia kuwa aliyeko juu atabaki kuwa juu ndugu ama unamtia hofu kuwa asikufikie. Hivi Unajua kulikuwepo na dola nyingi na kubwa sana duniani na Leo hii hazipo kaka sijui Dada.
Kwa uchache Roman empire,Ottoman empire, Mali empire ya mansa Musa na akina mfalme Suleiman mbona hawako juu mpaka Leo hii ama koo zao. Ila tumeona akiibuka marekani akina Jeff Benzos mpaka akampita Bill gates, Akina mark zurkebang Wa fb, madogo Wa twita wana Hela na hawakuwa na kitu kaka.
Vipi Yule mmasai laizee Wa bilioni 7.8 aliyeuza Tanzanite kule mererani imekuwa je. Kwani hajakupita ama bado Uko juu yake.

Eti aliyeko juu atabaki juu haya endelea kujifungia na kaimani kako hako sijui umekatoa nchi gani mana waafrika kwa kukopi hamjambo mpaka majina yenu hamyataki.

Eti aliyeko juu atabaki kuwa juu. Ivi Unajua kuwa bukoba saivi vijana hawasomi kama babu zao walivyokuwa wakisoma.
Saivi wapo wanaokuja juu kwa kasi sana na ndo Hao saivi umeona wamejazana na wanateuana.

Mana zamani kulikuwepo na wasomi wachache Wa maeneo Fulani ndo walishikilia kila ofisi ya umma afu wakaibaje eti wanajidai kuwa ni wajanja kwa kuiba. Saivi hawajapewa hata teuzi nusu wanajilizaje eti nchi haiwezi enda bila ya wao utadhani wamekuwa Mungu.

Cheki kinachotokea Ethiopia waliozoea kuiba serikali saivi hawajapewa nafasi wameamua kuingia vitani mana aliyeko hajawapendelea mana walizoea kupendelewa saivi mirija imekata. Roho inawaumaje yaani mtenda akitendwa ama mkuki kwa nguruwe kwa binadamu unaumaje.

Tunabadili katiba tunampa atawale mpaka afe na atarithiwa na makonda ili awanyooshe waliozoea dili,ujanja ujanja Wa kukwepa kodi.
Tuone walivyo watafutaji sasa waendele kutafuta tuone.
Mana ulikuwa ukipitisha mzigo wako TPA tokea China ama kwingineko ushuru juu ila kama walikuwa wamejazana huko waliwaachia ndugu zao wakawa wanasumbua watu kariakoo ila wengine ushuru mkubwa mpaka haurudii awamu nyingine kufuata mzigo.

Afu unaonekana kama sio mtafutaji na huku mwenzako akapita kodi akalipa kidogo ila wewe unalipa 100 times ya alicholipa
 
Bado unasumbuliwa na wivu someni/somesheni la sivyo mtaishia kulalama tu
 
Uamuz Ni wako Kama utaamua kusoma au kuchunga mbuzi na kucheza na chatu
 
Bado unasumbuliwa na wivu someni/somesheni la sivyo mtaishia kulalama tu
Yaani ume block kichwa chako mkuu.
Nimekuambia kuwa watu ama nchi zinanyanyuka. Wa mwisho anakuwa Wa kwanza.
Nimeuliza kuwa roman empire Iko saivi. Jibu lako liko jepesi kama mwanaidi na mwajuma wanaimba taarabu.
Walichunga mbuzi miaka iyo kaka. Kwani saivi hauoni kuwa hata familia ama Ukoo una wasomi Wa kuongoza nchi nzima ama huoni. Unajua MTT Wa Dada alikuwa wapi, saivi director tiss, TRA,cag ,TPA, madini hauoni Hao baba zao waliochunga ngombe waliwasomeshea saivi wameshikilia vitengo ndugu.
Tiss yote na cdf na jeshi lote kiujumla yaani nakuambia kuwa wewe mu omoro,Amhara ama mtigray bweka uone mana silaha zote tunazo.
 
umeongea upupu gani paragraph ya mwisho mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika kwa HISIA SANA....

Ngojea niisome tena kwa mara ya 3....😁😁

Back
Top Bottom