Wafanyakazi washinikiza FAO la kujitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi washinikiza FAO la kujitoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 23, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  WAFANYAKAZI wa migodi wametaka Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) irudishwe bungeni kwenye mkutano ujao ili kipengele cha fao la kujitoa kiondolewe mara moja.

  Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jana, wafanyakazi hao walisema kuwa kupelekwa sheria katika Bunge lijalo kutasaidia kupata haki na si kusubiri miaka 55 wakati migodi mingine imeanza kufungwa.

  Mwakilishi wa Katibu wa Chama Wafanyakazi wa Migodi na Viwanda Tanzania (Tamiko), Benjamin Dotto, alisema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa wafanyakazi wa migodi huku fedha yao ikitumika kutekeleza miradi ya serikali ambayo haina faida kwa wafanyakazi.

  Dotto alisema kuwa wafanyakazi wa migodi wanafanya katika mazingira magumu hali ambayo fedha zinaweza kuwasaidia katika maisha kutokana na athari zinazotokana na sumu ya migodi, kwamba hawana uwezo wa kufika miaka hiyo kama sheria inavyosema.

  Aliongeza kuwa msimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii atokane na wafanyakazi ili aweze kusimamia haki na sheria zinazomnufaisha mfanyakazi.

  “Wafanyakazi wa migodi wako katika mazingira magumu kutokana na kazi wanazofanya ambapo hawawezi kusubiri miaka hiyo ambayo sheria hiyo inataka huku wakiwa wameathirika na migodi,” alisema Dotto.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Wachimba Migodi, Joseph Mgire, alisema kuwa amani itatoweka kama sheria hiyo haitatekelezwa katika wakati muafaka.

  Mgire alisema kuwa wafanyakazi wa migodi wako katika mikataba ambayo haieleweki kutokana na makampuni hayo wakati wowote yanaweza kufungwa na kulazimika kusubiri miaka 55 kuweza kupata mafao yao.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni wakati muafaka kwa wafanyakazi wote nchini kuungana pamoja kupinga sheria hii ya kipuuzi.
   
 3. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  sijui tunangoja nini! na kilaaniwe chama cha mafisadi! nangoja kipenga kilie, nitakuwa wa kwanza barabarani
   
 4. m

  mdunya JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hawa jamaa ni vichwa nazi, mpaka magari yao yachomwe moto ndo wataelewa
   
 5. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  Alafu nikimwangalia mwangalia hivi kabaka, naona kama analipepo la kutokubali sheria hii irudi. Yupo tayari kuipigania mpaka tone la mwisho la damu. Kwa hiyo hii sheria ikirudi labda 2015.
   
 6. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mbona ,wafanyakazi wa Migodi ndiyo wanalalamika peke yao, Wafanyakazi wa idara zingine vip?
   
 7. fishengoma62

  fishengoma62 Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  wawakilishi wetu, wabunge, hawakuwa makini katika kupitisha sheria hiyo. pili, baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya wafanyakazi katika nchi hii walichomeka vipengele ambavyo havikuwemo awali na wameonekana mashujaa!!!!!!!!
   
 8. papason

  papason JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Binafsi siku ya jana nimesikitika sana!

  Yaani wafanyakaza wa migodini tuu ndiyo waliojitokeza kutetea fao la kujitoa ?tena kwa kuchangishana

  Yaani wafanyakazi wa Tanzania huu unyonge na uoga ktk kutetea maslahi yetu sijui utaisha lini?
   
 9. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ccm na serikali yake wasiporejesha fao la kujitoa watashuhudia maandamano ambayo hawajawahi kuyaona. watajuta. Maandamano yakigoma yatafuatwa na migomo ya wafanyakazi. wasituchezee.
   
 10. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu nilimsikia mnyika JJ akisema jamaa walichomeka kipengele hicho baada ya kupitishwa bungeni na kupeleka kwa mkulu kumwaga wino,
  viongozi wetu ndo wanatusaliti.
  hapa inabodi wafanyakazi wote tokamae watupe haki zetu.

  mbona fao la wabunge hawasubir miaka 55? wao miaka 5 tu wanachukua!!!!!!!!
   
Loading...