Wafanyakazi wanadai haki nje ya vyama vya wafanyakazi, wananchi tulifanye nini bunge letu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wanadai haki nje ya vyama vya wafanyakazi, wananchi tulifanye nini bunge letu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WATANABE, Feb 1, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Baada ya miaka mingi ya mfumo wa vyama vya wafanyakazi kuonekana kushindwa kabisa kutetea maslahi ya wafanyakazi wa kada mbali mbali hususan katika kipindi hikli cha mfumuko mkubwa wa bei; hivi karibuni wafanyakzi wa kada mbali mbali wamejitokea kudai haki zao ikiwemo kutumia migomo nje ya utaratibu wa vyama vya wafanyakazi.

  Mifano hai ya hali hiyo ni madereva wa magari makubwa ambaokwa mingi wamekuwa wakinyanyswa kwa kufanya kazi pasipo mikataba, kulipwa ujira na posho ndogo za kujikimu wawapo nje ya vituo vyo vya kazi, kunyanyaswa na waajiri n.k.

  Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita madereva hawa wamewahi kugoma mara mbali chini ya asasi ya kiraia (NGO) Chama cha Madereva wa Magari makubwa Tanzania (CHAMAMATA) badala ya kutumia Chama cha wafanyakzi sekta ya usafirishaji (COTWU). Aidha hivi sasa madakatari wapo katika mgomo chini ya chama cha Madakatari (MAT) kilichounda kamati ya mpito kusimamia mgomo huo badala ya kutumia Chama cha wafanyakazi sekta ya afya (TUGHE).

  Badala ya wadau ndani ya vyama vya wafanyakazi kukaa chini na kutafakari hali hii mpya ina maana gani kwa mustakabali wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini, Shirikisho a Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) lilikurupuka na kupitia Katibu Mkuu wake Ndg Nicholas Mgaya na kutangaza kuwa mgomo wa madaktari ni batili.

  Je ni nini kimepelekea wafanyakazi nchini Tanzania kupoteza imani ya mfumo rasmi wa vyama vya wafanyakazi kiasi cha kutumia njia na majukwaa mbadala kudai haki zao?

  Je kama ambavyo wafanyakazi wameonyesha kupoteza imani ya mfumo wa vyama vya wafanyakazi, wananchi nao wanaweza kupoteza imani na mhimili wa bunge ikizingatiwa kuwa kadrisiku zinzvyoongezeka mhimili huo unonyesha kuwa kushindwa majukumu yake ya kuwa wawakilishi wa wananchi katika kuisimamia serikali na badala yake wanaungana na wafujaji wa fedha na raslimali za umma walioko katika mhimili wa serikali kwa kujitwalia mikopo mikubwa mikubwa kwa kutumia dhamana zitokanazo na kodi za wananchi, kujilundikia kiasi kikubwa cha posho ya kukaa kutenda kazi ambzo wanalipwa mishahra kuzitenda n.k

  Tukifika hapo nini hatma ya Tanzania?
   
 2. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...Mimi nadhani mbinu wanazotumia akina Nichols Mgaya wa TUCTA kudai haki zimechuja/zimepitwa na wakati hivyo hazinauwezo wa kukabiliana hawa waajiri vichwangu.Madaktari wameliona hilo ndo maana wameamua kuchagua njia hii kwahiyo sasa ni wakati wa akina Mgaya kujitathimini kama kweli bado wanachama wao wanufaika na uwepo wa hivi vyama vya wafanyakazi.Labda ni muulize Mgaya serekali imekiuka mara ngapi makubaliano kati yake na wafanyakazi?,najua unalo jibu la kwamba ni mara nyingi serekali imekuwa ikiuka makubaliano ambayo wewe ni shaahidi.Sasa unaposema mgomo wa madaktari ni batili nakuwa sikuelewa unamaana gana kwa kutokuona ubatili wa serekali kuyakalia madai ya madaktari bila kuyafanyia kazi miaka nenda miaka rudi,umeshidwa kuuona ubatili wa serikali kupitisha posho ya 200,000 kwa watu wanoenda bungeni kulala lakini ikashindwa kuwaongeza ata senti moja hao unaojidai unawaongoza ktk kudai tija ya kazi wanazofanya!...MADAKTARI SHIKILIENI HAPO HAPO MPAKA HAKI YENU IPATIKANE!...
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Historia ya nchi nyingi duniani inaonyesha kwamba wafanyakazi ndio kwa kiwangi kikubwa wamekuwa wakisababisha na kuleta mabadiliko ya uongozi katika nchi husika, mfano hai ni Zambia vyama vya wafanyakzi ndio vilianzisha vuguvugu la kubadili uongozi wa juu wa nchi, Je kuna somo lolote watanzania wapenda mabadiliko tunaweza kujifunza na badala ya kutegemea vyama vya siasa kuhamasisha na kuleta mabadiliko wafanyakazi wakachukua nafasi yao kwa kushirikisha wakulima kuleta mabadiliko ya uongozi wa nchi?
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Nicholas Mgaya na wengi wa viongozi ktk vyama vya wafanyakazi ni kada moja na hawa waliopo madarakani. Maarifa,busara na hekima ya kusoma kizazi hiki kinataka nini,waongozwe vipi hawana! Tutaona madudu zaidi kadri siku zinavyosonga na utawala huu ukizidi kuporomoka.
   
Loading...