Wafanyakazi, Walimu na Wajasiriamali watengenezewa fursa ya kuneemeka

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
d03d5e8c-d24a-4e62-a84f-ebcff3a4906c.jpg

Rais Samia Suluhu yupo Mkoani Kagera katika ziara ya kikazi, lakini upande mwingine juhudi za kuendelea kumuunga mkono zimekuwa zikifanyika.

Wafanyakazi, walimu na wajasiriamali wametengenezewa njia ya kukopeshwa vifaa vya ujenzi ili kufikia kumiliki nyumba na kuboresha makazi yao kwa bei nafuu.

Neema hiyo imeelezwa kuwa imetolewa na Mwalimu Commercial Benki ambao wameeleza kuwa watafanikisha hilo kwa baada ya kuanzisha huduma mpya ya kutoa mikopo ya vifaa vya ujenzi ya Jenga na Mwalimu.
477e0dd5-97a4-4e2d-8fd2-a70bfcb17b1a.jpg

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Abdallah Kirungi akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa FMJ Hardware Limited, Fatina Said baada ya kutangaza bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK.

Kaimu Meneja Biashara wa benki hiyo, Sabina Mwakasungura amesema huduma hiyo itatolewa kwa kushirikiana na Kampuni ya FMJ Hardware Ltd.

"Huduma hii pia inalenga kusaidia wafanyakazi kuunganishwa na huduma za umeme. Na katika kuhakikisha usalama wa vifaa hivyo, Mwalimu Benki itaviwekea bima ya uharibifu wowote katika kipindi cha usafirishaji wake hadi pale popote alipo," alieleza.

Alisema wanatambua kuwa kasi ya Serikali ya awamu ya sita kuboresha maisha ya watumishi wa umma hususani walimu.

Alisema Mwalimu Benki ni benki ya kipekee iliyojikita kutoa huduma za kifedha kwenye ikolojia ya elimu ikilenga wanafunzi kwenye vyuo vya elimu, walimu, shule, taasisi za elimu, Wizara ya Elimu, TAMISEMI, Watumishi wa Umma na taasisi binafsi na wadau wote wanaotoa huduma kwenye sekta ya elimu pamoja na huduma kwa Wajasiriamali.

Alisema moja ya maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kuwa na bidhaa zinazolenga moja kwa moja mahitaji ya Watumishi wa Umma, Walimu na taasisi binafsi katika kujiinua kiuchumi na kuleta tija kwenye jamii.

"Benki yetu mpaka sasa ina matawi mawili yaliyopo Dar es salaam (Samora na Mlimani) na tunavyo pia vituo vya huduma tisa katika mikoa ya (Morogoro, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha, Rukwa, Kigoma, Mtwara na Arusha).

Matarajio yetu ni kuwa na vituo hivyo katika mikoa yote ifikapo mwaka 2025," alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya vifaa vya ujenzi ya FMJ Hadrware, Fatina Senzota aliitaka benki hiyo itanue wigo zaidi na kuwafikia wafanyakazi wakiwemo walimu binafsi kwa kuwa na wao wanahitaji pia huduma za mikopo kama hiyo.

Alisema kampuni yake ina matawi nchi nzima ikiwemo nchi za Congo na Rwanda hivyo huduma hiyo itakuwa ni rahisi kuwafikia watu wote watakaojiunga nayo.

Kaimu Mkurugenzi wa Mwalimu benki Abdallah Kirungi alisema pamoja na kwamba benki hiyo inahudumia walimu katika mikoa yote 26 lakini pia ina mpango wa kuwafikia watumishi wengine wa umma na binafsi pamoja na wafanyabishara.
 
Back
Top Bottom