Wafanyakazi walalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi walalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jul 29, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wafanyakazi walalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 28 July 2011 21:34 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Gedius Rwiza na Patricia Kimelemeta
  BAADHI ya wafanyakazi wa umma wamelalamikia nyongeza ya mishahara iliyoanza kulipwa na mwisho wa Julai, mwaka huu.Uchunguzi wa gazeti hili kutoka kwa wafanyakazi wa kada mbalimbali za utumishi wa umma ambao tayari wamelipwa mshahara wa mwezi Julai, umebaini kuwa kiasi kilichoongezwa ni kati ya Sh10,000 na Sh70,000.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wafanyakazi hao walisema wameshindwa kujua vigezo vilivyotumika kuwaongezea viwango hivyo ambavyo havikidhi mahitaji ya sasa kimaisha.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Kilimo ambao ni maofisa ugani, walisema kiwango chao cha elimu ni stashahada, ambao awali walikuwa wanapata Sh 230,000 baada ya makato, sasa walisema wanapata Sh300,000.

  Mfanyakazi mmoja ambaye yupo katika sekta ya afya ambaye ni muuguzi, alisema ana miaka 11 kazini na ameongezewa Sh40,000 ambazo alisema ni kudogo.

  “Ni kweli tumeongezewa mshahara, lakini ni sawa na kutoongezwa ikilinganishwa na gharama za maisha zilivyopanda,” alisema mfanyakazi mwingine.Kwa upande wa walimu waliohojiwa na gazeti hili, walisema baadhi yao wameongezewa Sh 20,000 na wengine Sh60,000 na kwamba, Serikali imeshindwa kukifikisha kiwango cha kima cha chini kilichopendekezwa,.

  “Kwa mfano, walimu wa stashahada tunabakiwa Sh 250,000 baada ya makato wakati tulitegemea kima cha chini kuwa Sh350,000, hivyo kwa ngazi yetu tungepata tungepata zaidi,” alisema mmoja wa walimu hao.

  Kauli ya CWT
  Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema kitendo cha Serikali kushindwa kufikisha kima cha chini cha Sh350,000, kitaleta mgogoro kati yake (Serikali)na wafanyakazi.

  Mukoba alisema: “Unajua, Serikali inawakejeli wafanyakazi, kwani kumwongezea mfanyakazi Sh30,000 ni kitendo cha kumfanyia kejeli, kwani kutokana na halu maisha ilivyo sasa, hata kima cha chini kilichopendekezwa hakitoshi,”alifafanua Mukoba.

  Msimamo wa Tucta
  Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limesema nyongeza hiyo mpya ya mishahara ni ndogo na haikidhi mahitaji ya wafanyakazi nchini.
  Akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya, alisema nyongeza hiyo ni ndogo ikilinganishwa na hali ya maisha ya sasa.

  Mgaya alisema, mwaka 2007 Tucta ilpendekeza kuwa kima cha chini kiwe Sh315,000, lakini Serikali imeshindwa kuongeza hadi sasa, badala yake imeongeza asilimia 11 hadi 12 ya mishahara

  “Sasa hivi tunasubiri walaka wa mishahara mipya ili tuweze kuangalia nyongeza hiyo, lakini tunavyojua ni ndogo na kwamba, haiwezi kukidhi mahitaji ya wafanyakazi, kutokana na hali hiyo hiyo Serikali inapaswa kuliangalia suala hilo kwa undani ili kuondoa migogoro ya wafanyakazi.Alisema baada ya hapo watakusanya maoni kutoka kwa wafanyakazi wenyewe na kutoa tamko kulingana na nyongeza hiyo ili waweze kuangalia hatua zitakazofuata.

  Kwa mujibu wa Mgaya, migogoro ya wafanyakazi inatokana na viwango midogo na kwamba jambo hilo limechangia wafanyakazi kushindwa kufanya kazi kwa bidii na kukithiri kwa rushwa katika uwajibikaji.

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alipoulizwa na gazeti hili kuhusu vigezo vilivyotumika kuongeza mishahara alisema kuwa, kwa sasa yeye hawezi kuzungumzia suala hilo na kuongeza kwamba, viongozi wa vyama vya wafanyakazi walishiriki katika mchakato huo.
  “Unajua, viongozi wa vyama vya wafanyakazi walishirikishwa katika mchakato wa kuongeza mishahara, hivyo unaweza kuwahoji watakupa jibu sahihi,” alisema Ghasia.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  0 #2 Mshahara Bongoooooo 2011-07-29 03:03 Amakweli ukimzoea Mmbwa atakufuata Msikitini baba.Naona Da Hawa kaamua kuwa hiyo kitu,sasa anawafuata hukohuko waliko.Kudadeki Mgaya,msala huo jitishe,siulish iriki mchakato?We Mshahara ulioongezwa ni Maandazi ya Watoto wa Da Hawa asubuhi!tehe tehe tehe
  Quote

  0 #1 kinyero 2011-07-29 02:27 hapa naona ishakuwa issues sasa, waswahili wanasema ukicheka na mbwa atakufuata hadi msikititini sasa viongozi wa wafanyakazi wamekaribishwa ikulu haya ndio matunda yake waziri anasema kina mama mgaya,mkoba,kiw enge wanajua swala hili haaaaaaaaaalaaa aaaaaaa sasa hiii itawatokea puani.
  Quote  Refresh comments list

  [h=4]Add comment[/h] Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
  Name (required)
  E-mail

  7000 symbols left
  Notify me of follow-up comments

  [​IMG]
  Refresh
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h]


  #6 rutashubanyuma 2011-07-29 08:14 tuna serikali ambayo inajidai inawalipa wafanyakazi na wafanyakazi nao wanajidai kufanyakazi wakati pande mbili zote ni ulaghai mtupu.............
  Quote

  0 #5 jackob enock 2011-07-29 07:20 Mishahara hii kwa 'digits/figure' ni mikubwa sana. Kinachotakiwa ni kwamba serikali itadhibiti vipi mfumuko wa bei na kuhakikisha bidhaa zote muhimu zinashuka bei ili kuipa thamani fedha/mishahara.
  Kinacotakiwa ni kuibana serikali ishushe bei za bidhaa zinazosababisha mishahara yenye 'figure' isiwe na thamani. tunaweza kudai leo mishahara kima cha chini kiwe 350,000.00 halafu kesho serikali ikaongeza kodi kwenye nishati ili kupata fedha ya kufikia hiyo 350,000.00. Je kwa staili hiyo tutafika? Nadhani inabidi tubadili namna ya kudai maisha bora ni sio kwa staili ya nyongeza kubwa ya mishahara itakayokuja kuongeza shida katika uchumi na maisha kwa ujumla.
  Quote

  0 #4 Joe 2011-07-29 07:18 mnadai kuongezewa mishahara kwa kipi mnachozalisha??muda wote mnashinda kwenye mitandao,facebo ok,twitter then mnataka kupewa mishahara mikubwa? zalisheni kwanza kama wenzenu wa asia,ulaya na america ndio mdai mishahara mikubwa
  Quote

  0 #3 nyodi 2011-07-29 06:53 akili na utashi upo au ndio maneno ya JAKAY A KIKWETE YA MEI 2 2010.???????????? tunaenda barabarani kudai mishahara yetu !!!!!! mkiweza mtuue kwa kuandamana.
  Quote

  0 #2 Mshahara Bongoooooo 2011-07-29 03:03 Amakweli ukimzoea Mmbwa atakufuata Msikitini baba.Naona Da Hawa kaamua kuwa hiyo kitu,sasa anawafuata hukohuko waliko.Kudadeki Mgaya,msala huo jitishe,siulish iriki mchakato?We Mshahara ulioongezwa ni Maandazi ya Watoto wa Da Hawa asubuhi!tehe tehe tehe
  Quote

  0 #1 kinyero 2011-07-29 02:27 hapa naona ishakuwa issues sasa, waswahili wanasema ukicheka na mbwa atakufuata hadi msikititini sasa viongozi wa wafanyakazi wamekaribishwa ikulu haya ndio matunda yake waziri anasema kina mama mgaya,mkoba,kiw enge wanajua swala hili haaaaaaaaaalaaa aaaaaaa sasa hiii itawatokea puani.
  Quote  Refresh comments list
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  Ni lini serikali na vyama vya wafanyakazi vikakaa chini na kutathmini mbinu za kuongeza tija badala ya hoja zisizo na mashiko za kushinikiza mishahara kuangalia kigezo kimoja tu cha gharama za maisha katika kuipandisha......................................gharama za maisha pekee haziwezi kuongeza uzalishaji kama uzalishaji wenyewe ni sifuri.......................................mwisho wake utakuwa ni kuitupilia mbali shilingi yetu na kujikita kwenye dola kama Bw. Mugabe alivyolazimika kufanya................
   
 5. F

  FLORID Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wafanyakazi wenzangu hakuna mshahara utakaotosha, kuna maneno yanasema kadiri pesa yako inavyoongezeka ndivyo na walaji wanavyoongezeka. Ningeshauri hivi tujiondoe ktk kundi la wanaoilalamikia serikali tujiingize ktk kundi la wanaofikirisha akili zao kutafutanjia mbadala ili kuinua pato ulilo nalo.
   
Loading...