WAFANYAKAZI WAGOMA KUFANYA KAZI A-ONE MeTL

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,198
1,226
Kwa kile kinachooneka kuwa mwendelezo wa serikali kutowajali wananchi wake na kuwathamini wawekezaji, leo ni siku ya tatu wafanyakazi wa kampuni ya MeTL upande wa kitengo cha kuzalisha Maji na juice (A ONE) wamegoma kufanya kazi kufuatia kile kinachodaiwa na wafanyakazi hao kuwa wamekuwa wakijaribu kuushawishi uongozi wa kampuni hiyo kuweka hali bora za kazi kama vile NSSF,kupata ajira ya kudumu (kwani mpaka sasa waliopo wamefanya kazi kwa takribani miaka 10 wakiwa vibarua) na mambo mengi kadha wa kadha bila mafanikio,

Wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu bila vifaa vya kufanyia kazi, wamejaribu kushirikisha vyombo vya habari bila mafanikio hivyo kuwawia vigumu wafanyakazi kujua wafanye nini?

Wakuu nitawajuza kinachoendelea naenda piga picha muone hali halisi
 
ndugu yangu hivi hao wafanyakazi wa METL ni wa serikali pia au? mbona hoja yako hafifu sana.
au hujui kama kiwanda hicho sio cha serikali ila ni cha mtu binafsi?
 
Back
Top Bottom