Wafanyakazi wageni 'vihiyo' wasakwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wageni 'vihiyo' wasakwa

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by BAK, Oct 9, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,115
  Likes Received: 32,721
  Trophy Points: 280
  na Edson Kamukara | Tanzania Daima | Oktoba 09, 2012

  SIKU chache baada ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, kuahidi kuwavalia njuga baadhi ya wafanyakazi wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha utaratibu na kufanya kazi bila vibali, msako mkali umeanza kwenye baadhi ya mahoteli jijini Dar es Salaam.

  Dk. Mahanga alitoa ahadi hiyo baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za kushamiri kwa wageni hao kwenye makampuni kadhaa ya kigeni na mahoteli makubwa jijini Dar es Salaam na kuajiriwa kufanya kazi za kawaida ambazo kwa mujibu wa sheria za nchi zinapaswa kufanywa na raia wa Tanzania.

  Katika mfululizo huo wa habari hizo, ilitajwa pia moja ya hoteli kubwa iliyoko eneo la Kunduchi pamoja na kampuni moja ya Kichina iliyoko eneo la Ubungo, ambapo wameajiriwa raia wengi wenye asili ya India na China ambao baadhi yao hawana vibali vya kazi wala ujuzi wa kazi walizoajiriwa kufanya.

  Hata hivyo, hatua hiyo ilielezwa kuwa inachangiwa na baadhi ya watendaji wa wizara za Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji na ile ya Kazi na Ajira ambazo hutoa vibali hivyo.

  Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwepo madai ya baadhi ya watendaji wanaotoa vibali kinyemela kwa wageni hao na hivyo kusababisha raia wa Tanzania wenye sifa kukosa ajira kwenye makampuni na mahoteli husika.

  Tuhuma hizo zilithibitishwa pia na mmoja wa viongozi wa juu wa hoteli moja iliyopo Kunduchi ambayo inalalamikiwa, akidai kuwa watendaji wa wizara hizo wameendekeza rushwa na hivyo hata wanapokwenda kuzikagua hoteli hizo, wanachukua kitu kidogo kutoka kwa wamiliki.

  "Mimi si msemaji wa hoteli kuhusu jambo hilo unaloliuliza lakini nikwambie kuwa anayeidhinisha sifa za wageni hao kama wana sifa au la ni mwajiri. Pili watu hawa wako nchini kihalali wakiwa wameidhinishwa na serikali.

  Kuhusu madai ya uongozi wa hoteli hiyo kutoa rushwa kwa maofisa wa serikali ili kuwalainisha wasiwasumbue wageni hao, alikiri kuwa ni kweli na kutamba: "Kama tunao uwezo huo wa kufanya hivyo kwa nini tusifanye?

  Kufuatia madai hayo, Naibu Waziri Mahanga, aliliambia gazeti hili kuwa apewe muda kidogo ili aweze kutuma wasaidizi wake kuzikagua kampuni na hoteli hizo kuona ukweli wa malalamiko hayo, huku akisisitiza kuwa vibali vya kazi kwa wageni ni vya miaka miwili na kwamba hakuna anayeruhusiwa kufanya kazi bila kuwa na kibali husika.

  Hata hivyo alikiri kuwepo kwa msigano baina ya wizara hizo mbili akisema kuwa wanaandaa muswada ili jukumu la utoaji vibali hivyo libakie chini ya wizara moja tofauti na sasa ambapo wizara ya kazi inamwidhinisha mgeni na kupeleka taarifa zake Idara ya Uhamiaji kumwombea kibali.

  Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinasema kuwa mara mbili katika wiki iliyopita, watendaji wa wizara hizo wamefika katika hoteli hiyo yenye wafanyakazi wa kigeni zaidi ya 29 na kufanya mahojiano na baadhi yao sambamba na kukagua vibali vyao vya kazi.

  Chanzo hicho kimebainisha kuwa mchakato huo hata hivyo umeingia dosari kutokana na wafanyakazi hao wengi wao kutimkia kujificha kusiko julikana kila maafiasa wa wizara wapofika hotelini hapo.

  "Watendaji wa wizara walifika hapa katikati ya wiki lakini wafanyakazi wengi walikimbilia kujificha na hivyo hawajahojiwa wala vibali vyao havijakaguliwa, zaidi tumeona uongozi wa juu ukijaribu kuwashawishi walimalizane," kilisema chanzo chetu.

  Pia kwa mara nyingine siku ya Ijumaa, watendaji hao wa wizara walifika hotelini hapo lakini wafanyakazi wengi wa kigeni wanadaiwa kukimbia wakikwepa kuhojiwa.

  Mbali na baadhi kujificha, mameneja watatu wa hoteli hiyo waliangukia mikononi mwa maofisa hao wa uhamiaji.Walionaswa na kuhojiwa ni meneja matunzo,meneja anayesimamia usafi na meneja wa mapishi.

  Waliofanikiwa kuwakwepa maafisa hao ni pamoja na mhesabu mashuka na taulo, mkagua bili, msimamizi wa baa, mpishi, fundi na wengine. Taarifa hizo ziliongeza kuwa baada ya ukaguzi, baadhi ya wafanyakazi hao waliokuwa wamekamatwa walibainika kuwa na vibali halali licha vibali hivyo kuwa na mashaka.
  "Waliobakia wawili hawakuwa na vibali, hivyo maafisa hao walikwenda nao ofisini kwao lakini baada ya takribani saa tatu walirudi kazini na kuendelea na kazi," chanzo chetu kilisema.

  Idadi ya wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini imekuwa ikiongezeka kwa kasi kiasi cha kutishia ajira za wazawa kwani kazi nyingi wanaoajiriwa kuzifanya zinaweza kufanywa na Watanzania.

  Msemaji wa mmiliki wa hoteli hiyo, alipohojiwa na gazeti hili alishindwa kufafanua ni kwanini raia hao wa India wanaletwa kufanya kazi za kawaida ambazo nyingine hazina utalaamu wowote.

  Badala yake, alitetea kuwa huo ni uamuzi wa mwenye hoteli kuajiri wafanyakazi atakavyo na kwamba wengi wao ni raia wa Tanzania wenye asili ya India.
  "Hao wanaolalamikiwa si wageni kutoka nje, wengi wao ni Watanzania wenye asili ya India, wanawahukumu kwa rangi zao. Wala hawafanyi kazi hapa hotelini wote, sisi tuna makampuni kama 18, sasa wakiwaona humu wanadhani wameajiriwa," alitetea.

  Akizungumza na gazeti hili jana, msemaji wa Idara ya uhamiaji, Abbas Irovya, alikiri kufanyika kwa msako huo akifafanua kuwa huo ni utaratibu wao wa kawaida ili kuwabaini wanokiuka sheria.

  Kuhusu baadhi ya wageni kuwapiga chenga, alisema hiyo ni hali ya kawaida kwa kila mwarifu na hivyo akaomba wazalendo kutoa ushirikiano ili wahusika wakamatwe.

  Abbas alikiri kusikia tuhuma za rushwa kwenye idara yao lakini akafafanua kuwa jambo la msingi ni wananchi kupewa elimu ya kutosha wakajua vyema majukumu ya idara ya uhamiaji.
   
 2. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,263
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo patamu. Haya ni mazingira ya rushwa kbs. Tumeona hii picha toka miaka ya mwanzoni mwa 2000.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,115
  Likes Received: 32,721
  Trophy Points: 280
  Hawako serious kabisa hawa katika kupambana na hili tatizo. Hawa watu wanazidi kuvamia nchi kila kukicha lakini uhamiaji wanachapa usingizi na pia wanaweka mazingira ya kupokea rushwa toka kwa watuhumiwa.

   
 4. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,391
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hawana lolote, waende mabank na sehemu nyingine, na cha ajabu hao wasaidizi wake wanapita hayo maeneno lakini mwisho wa siku wanapewa rushwa na mambo yarudi vile vile, inasikitisha sana watanzania walosoma wanakosa kazi na kazi hizo kuchukuliwa na wageni ambao imma wana sifa kama za hao au wamepitiliza zaidi ya hao! nchi yetu ni SHMBA LA BIBI ! nani asijua hilo? wahindi wapakistani tena cha ajabu hao hao wakishakuja hapa hawaTAKI KUONDOKA NA MATOKEO YAKE huwalete ndugu zao ! TUMESHUHUDIA NYUMBA MOJA WANAKAA WATU 18 NA WOTE HAWANA VIBALI , na wanajulikana ila wasaidizi wa waziri wanakula rushwa ! mpaka lini Tanzania?
   
 5. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,263
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 280
  Ukipata ajira uhamiaji, miezi 6 tu unaweza kufikiria kustaafu. Watu wanapiga pasi ndefu huwezi kuamini.
   
 6. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,263
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tatizo sio wenye hoteli, tatizo ni huko wizarani wanakotoa hivyo vibali kiholela, kwa sababu hata wakikagua wakakuta wana vibali halali ambavyo walipata kwa kutoa hongo watawafanya nini.... ukija kuangalia matatizo yote ya nchi hii yanaanzia serikalini ambayo inaongozwa na ccm
   
 8. Mnene 1

  Mnene 1 Senior Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio hivo tu mkuu, uhamiaji hawachapi usingizi ila wananuka rushwa. Mimi nafanya kazi katika kampuni moja kubwa hapa nchini, cha kusikitisha ni kwamba wageni kila kukicha wanaingia, vyeo vya ajabu ajabu vinatengenezwa ali mradi tu wageni wapate ulaji. Wakishafika wanawanyanyasa sana wazawa.
  Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, jana tuliingia ofcn kama kawaida, tukashangaa wote wenye ngozi nyeupe hawapo, kumbe walishaambiwa kua uhamiaji wangefika ofcn jana kukagua kwa kushtukiza. Kweli jana mida ya asubuhi, watu wa uhamiaji walifika ila walikuta wazawa tu ofcn, zaidi ya nusu ya wafanyakazi ni wageni ila hawakuepo.
  Kwa kufikiria ni kwamba, kuna mtu uhamiaji kule alikua anajua mpango wote na akaamua kuwasiliana na walarushwa kwenye hii kampuni na kufanya kazi kubwa ya kuwapigia na ku-organize mambo yote weekend(jpili hasa) kwa wageni wote.
  Tanzania inajengwa na wenye moyo na inaliwa na wenye meno. so sad, watanzania wenzetu ndio wanatuangusha katika hili.
   
 9. H

  Heri JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Idara ya Immigration ndiyo kweli inanuka rushwa lakini hili la wageni kupewa vibali vya kufanya kazi ni mapungufu ya sheria za nchi yetu.
  Kampuni au mtu yeyote yule mwenye certificate ya TIC (Tanzania Investment Centre), ana ruhusiwa kuajiri expartriate toka nje kuja kufanya kazi katika mradi wake. Na hawa wageni ndiyo wanatumia hii certificate. Idara ya Immigration au Labour hawana ubavu wa kuzuia hii. Pia hakuna audit inafanywa ili kuhakikisha je ni kweli hawa exparts. wanatija na wanasaidia kutransfer ujuzi kwa Watanzania.
  Bunge na serkali inabidi kupitia hizi sheria na kuzifanyia marekebisho.
   
 10. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,787
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii habari ilitoka kitambo sana kwenye Tanzania Daima!!
   
 11. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nendeni private school kiongozi st marys muone wazimbabwe ,waganda wakenya na warundi wanavyoruka ukuta wakisikia immigration ,kwenye yale mahostel yake full raia wa kigeni
   
 12. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hawa wamekurupukia wapi? Mbona hili wanalifaham sana na taarifa zote wanazo??? Walikiwa wapi? Kila kitu kinajulikana na wafanyakazi wasiokuwa na sifa na vibali vya kazi wapo engi, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa!
   
 13. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,965
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  dawa ya yote haya ni kwa serikali dhalimu ya magamba kuondolewa madarakani,period. total destruction of magamba is the only solution.
   
 14. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nchi hii ishakuwa shamba la bibi, sisi wenyewe ndo tunawasaidia wafanyakazi hawa vihiyo kuwapa working permit sasa leo eti tunawasaka ni aibu iliyoje.Kwani si waliingia kupitia viwanja vyetu vya ndege na mipaka yetu mingine na passport zao tukazigonga sie wenyewe iweje leo iwe vigumu kuwakamata mpaka tuanzishe misako. Kwa kuanzia huyo Makongoro aende kwenye migodi ya Barrick yote wamejaa kibao, aende kule Serengeti kwenye hotel ya Singita Grumeti Reserves wamejaa makaburu vihiyo mpaka aibu, aende hotel ya Serena kuna wahindi hawajui hata kukata kitunguu lakini wanaitwa eti head chef, aende migodi ya Tanzanite kuna makaburu kibao, aende TGT pale Arusha napo kuna kambi pale, aende na Songas na Ashant Gold.

  Mwambie kama hana cha kuongea kwenye TV na kuandika kwenye magazeti aachane na sisi walalahoi ambao ajira zetu zimechukuliwa na wageni wakati wizara yake inakula 10%
   
 15. H

  Hon.MP Senior Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kihiyo yeyote awe mgeni au mwenyeji, kamata na weka ndani apate adabu!
   
 16. Mkaguzi

  Mkaguzi JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waende saohil kule iringa wakaone maajabu walivyojaa. Hadi magardener wazungu wamepewa kazi za uinjinia. GM mwenyewe msanii wa kirusi! Yote ni sababu ya Rushwa. Wapo zaidi ya 20 huko
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Nchi yenyewe imejaa vihiyo wengi. Hili zoezi la kusakasaka ni kama kucheza makidamakida kwenye nyaya za umeme!
   
 18. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Kwenye mabenki napo wamejaa Wakenya na Wahindi hasa Barclays. Bank M kuna Chief Operation Officer Mhindi anaitwa Ganpath kazi anayofanya pale hata mwanafunzi wa form iv anaweza lakini analipwa mil RG
   
 19. k

  kfatherd Member

  #19
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Baada ya kusoma posti mbalimbali kuhusu swala la wageni kuingia nchini na kujipenyeza kwenye taasisi nyeti hapa nchini ningependa kuomba mod anazishe sub-group ya watu kuwaanika watu wazamizi wa nje na kuwezesha vyombo vyetu kupata clues on whereabouts..... Hii itasaidia wao kuwafuatilia kama hawapo nchini kinyume na taratibu. Kila mtu akifanya hivi pale alipo tutasaidia sana!
   
 20. Msingida

  Msingida JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2013
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 3,370
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Hi wizara angepewa Magufuli au Mwakyembe,usingeona mauzauza haya.Kwenye mashule kuna Walimu vihiyo toka nchi jirani mpaka basi.Ilimradi anaongea Kiingereza ka ajiriwa.Arusha karibu shule zote za private zina wageni "wazungumza Kiingereza" wengi na kuwanyima ajiira wazawa.
  Hawana uchungu na elimu ya Tanzania huku wakaguzi wakiwa wamelala usingizi wa pono wakisubiria posho.Watanzania Tumekwisha
   
Loading...