Wafanyakazi Waendelea Kujiua Kwenye Kampuni ya Simu ya Ufaransa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi Waendelea Kujiua Kwenye Kampuni ya Simu ya Ufaransa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 29, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kampuni ya simu ya Ufaransa, France Telecom imekumbwa na wimbi la wafanyakazi wake kujiua
  Tuesday, September 29, 2009 5:42 AM

  Mfanyakazi mwingine wa kampuni ya simu ya Ufaransa, France Telecom ambayo imekumbwa na wimbi la wafanyakazi wake wengi kujiua, amejiua kwa kujirusha toka kwenye daraja.

  Mfanyakazi mwingine wa kampuni ya simu ya Ufaransa, France Telecom amejiua na kuacha ujumbe akisema kwamba shinikizo la kazi za kampuni hiyo ndio sababu ya yeye kujiua.

  Mfanyakazi huyo mwenye umri wa miaka 51, baba wa watoto wawili, mkazi wa mji wa Annecy alijiua kwa kujirusha toka kwenye daraja linalopita juu ya barabara kuu ambayo iko bize muda wote.

  Alimwachia mkewe barua akimuelezea kwamba ni mazingira ya kazi katika kampuni yake ndiyo yaliyomsukuma aamue kujiua.

  Msemaji wa kampuni hiyo alikiri kujiua kwa mfanyakazi wao ambaye ameifanya idadi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo waliojiua ndani ya miezi 18 kufikia 24.

  Wiki tatu zilizopita katika kukomesha wimbi la wafanyakazi wa kampuni hiyo kujiua, mkuu wa kampuni hiyo alitoa risala ndefu kwa wafanyakazi wake ili kuwafanya wasiwe na mawazo ya kujiua.

  Lakini siku moja baadae mfanyakazi mwanamke wa kampuni hiyo mwenye umri wa miaka 32 alijirusha toka ghorofa ya nne ya jengo la kampuni hiyo lililopo jijini Paris na kufariki dunia.

  Kifo cha mwanamke hiyo kilitokea ikiwa ni wiki chache baada ya mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo mwenye umri wa miaka 57 kujiua nyumbani kwake na kuacha barua akiilamu kazi yake kwa kumfanya aingie kwenye dipresheni.

  Wiki hiyo hiyo, fundi mitambo wa kampuni hiyo alijichoma kisu tumboni kwenye mkutano wa wafanyakazi akilalamikia mazingira ya kazi.

  Kampuni hiyo ambayo awali ilikuwa ya serikali, ilibinafsishwa mwaka 1998 na ndipo wamiliki wake wapya walipoamua kufanya mabadiliko kwenye kampuni hiyo kuongeza ufanisi na kupunguza gharama.

  Mwaka 2000 walijiua wafanyakazi 28 wakati mwaka 2002 wafanyakazi 29 waliamua kujitoa roho zao wenyewe.

  Kampuni hiyo yenye wafanyakazi laki moja nchi nzima imelaumiwa na umoja wa wafanyakazi kuwa hatua yake ya kuwahamisha hamisha wafanyakazi na kuwapunguza kazi wengine katika hatua zake za kupunguza gharama ni miongoni mwa sababu zinazochangia wafanyakazi wake kujiua.

  Wamiliki wa kampuni hiyo wameamua kusimamisha mipango yote ya mabadiliko waliyoipanga awali ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama katika kampuni hiyo.  Source: AFP
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani mbona hii kali ,Hivi mazingira ya kazi yanaweza kukufanya ujiue?????
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huamini we kazi za huko sio kitoto bongo huku si tambarare ukishikwa hapa unashika pale ujanja ujanja mwingi watoto hawalali na njaa huko kwa wenzetu eh ikiwa tight ni tight kweli....depression kibao!!
   
Loading...