Wafanyakazi wa Vodacom na NSN mmejiponza wenyewe. Msitafute mchawi wenu. Ni nyinyi wenyewe.

Kweli mfumo CCM wa wizi, ubinafsi na ufisadi umetapakaa kila kona ya nchi. Inahitaji mjadala wa kitaifa ili siku moja wabongo tuje kuaminiana. Ile kitu inaitwa Jikombe Ukombolewe ndio inaleta usaliti mkubwa walionao wabongo wengi. Hata mimi bora niongozwe na Mzungu kuliko mbongo mwenzangu, nishaumwa na nyoka
 
Ungefupisha maelezo yako. Si kila mtu ni mpenzi wa kusoma maelezo mareeeeeefu yasiyokuwa na umuhimu kwake.
Kama hujasoma yote utakuwa umekosa uhondo na ufahamu. Nakushauri isome yote mpaka mwisho, usibakishe chochote halafu utaona utamu wake
 
Pole wote mnaohathiriwa na swala hili na pole zaidi kwani linalowakuta is just a tip in the icerge. Tanzania ya leo vijana ambao walitakiwa waonyeshe njia maana wamepata elimu wametokea kuwa kituko. Ukweli kwamba all the affected have failed to understand their enemy and rally around one philosohy and encounter the enemy is another but serious problem than being laid off as it appears hata mkishikapunguzwa inaonesha uraiani hamtashirikiana ili kuondeleana ukali wa maisha. Katikati ya matatizo yote haya ni unafiki wa Watanzania. Lakini unafiki mbaya zaidi unapojikita kwenye wasomi na watu wenye upeo. Na hili haliko VTL-NSN peke yake bali kote public sector na private sector. Mtanzania kwanza amekubali kipindi hiki kujirahisisha kwa wageni hasa weupe kuliko maneno. Wengi walioko VTL-NSN walitokea TRITEL iliyokuwa na ubia wa Malaysians na VIP Engineering ya Wazawa na Wahindi. Malaysians as majority share holders walikuwa wanaunda management na walikuwa wanaonyesha dhahiri uporaji wa faida wakipeleka kwao njia mbalimbali-kuleta wafanyakazi waliokuwa hawajui chochote na wenye vyeti vya kuunga, likizo zilizokuwa zikichota hela nyingi pamoja monetary repatriation kwa kigezo cha shareholders fee, kushindwa kulipa kodi kwa mamlaka husika na interconnection. Lakini hawakufanya haya peke yao bali walishirikiana na Watanzania wenzetu ambao walikuwa wanapewa kitu kidogo. Kwa kutumia udhaifu wetu waliunda vikundi vya kuwapelekea habari na majungu kaisi kwamba kila kilichokuwa kikifanyika walikuwa wanajua. Walimnyima local shareholders haki zake na wakamjengea uadui kwa staff kiasi staff wakawa wanamuona local sharehoder kama adui. Wakala mtaji wote bila kuwekekeza (network expansion) kama masharti ya regulator yalivyokuwa yanataka. Siku ilipofika wakatakiwa na mamlaka au wafunge biashara au wafate masharti wakaamua kufunga huku wakiwaacha wafanyakazi hawajui hili wala lile lakini wakati wanafanya hivyo wafanyakazi wakaunda kikosi kazi ili kifatitirie kujua hatima yao. Kila mkakati uliokuwa ukifanywa na wafanyakazi kuna Watanzania wenzetu walikuwa wanapeleka habari na hivyo kuwapa nafasi ya wao kukimbia nchi kwa kutumia chartered flight mpaka Nairobi walipoingia kwenye ndege kubwa asubihi wafanyakazi wanaingia ofisini wao walishafika Kuala Lumpur huku wakitamba kuwa Watatznania hatutumii akili.

Pole kwa yale yanayowakuta lakini yote ni matunda na ubinafsi na unafiki. Haya mambo yakiwa ndani ya mioyo ya watu na huku kuna kigezo kuwa whiteman never does wrong, matokeo yake ndio kama haya. Tunatakiwa kujifunza na makosa na wakuwa wakweli kama kweli tunataka kuendelea na kuiona nchi yetu inaendelea. Penye haki na ukweli tuwe wakweli na tusitafute mchawi
 
Yaani hii nchi imefikia hatua tunawaamini wageni kuliko wazawa wenzetu.
 
Baadhi ya Vodacom staff au NSN imefika mahala hadi wanaogopa kupata misiba kwa maana ya kwamba misiba inaumbua na kukufanya ujulikane ulivyo. Kuna msiba mmoja mabosi wa kizungu walihudhuria na wakashtuka sana kuona mfiwa amejenga hekalu ambalo gharama zake hazielezeki kwa staff wa Voda. Inasemekana kwamba wazungu wale wakasahau kwamba wako msibani wakaanza kujadili ukubwa wa jumba lile na kujiuliza alikopata mfiwa pesa za kulijengea!

Haikupita miezi miwili yule mfiwa akahamishwa idara akapewa "idara hewa" ya watu watatu tu wanaoripoti kwake. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa huyo jamaa kuhama Vodacom, na kweli ndani ya miezi minane akaacha kazi na sasa hivi ana bonge la kampuni yake anaendesha biashara nisiyotaka kuitaja kwani wengi Vodacom/NSN mnamfahamu na biashara yake si siri mnaifahamu.


Mkuu NokiaSiemens,
Umeeleza ukweli ambao Watanzania tulio wengi tunaukwepa kwa manufaa yetu binafsi. Mifano ipo mingi sana ya Ndugu zetu wazawa kupewa Dhamana ya Uongozi na kujisahau.

Huyo jamaa kwenye nyekundu hapo si ndio Mwenye ile kampuni ya ving'amuzi vya kulipia bili na Luku? Kitu kikubwa kinachoshangaza hata huo U-Aggregator wa Vodacom sijui aliupataje? Ila ukihoji mambo ya kimsingi Kama haya utaambiwa una wivu. Big up NokiaSiemens kwa uthubutu wako.
 
Du hii kali sana ila nasikitika wameshaanza kuilaumu CCM,
'Kweli mfumo CCM wa wizi, ubinafsi na ufisadi umetapakaa kila kona ya nchi. Inahitaji mjadala wa kitaifa ili siku moja wabongo tuje kuaminiana. Ile kitu inaitwa Jikombe Ukombolewe"

Wafanyakazi wote hata wale wenye makampuni yanayolinda minara ni matajiri sana, wako wengi wamenunua majumba na magari na wapo vyama vingine lakini kwenye uhujumu uchumi Wanaitwa CCM
 
usipo iba wanakuita mzubafu ukiiba unaambiwa fisadi,lipi jema kwa jamii.!
 
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

When the Nazis came for the communists,
I remained silent;
I was not a communist.

When they locked up the social democrats,
I remained silent;
I was not a social democrat.

When they came for the trade unionists,
I did not speak out;
I was not a trade unionist.

When they came for the Jews,
I remained silent;
I wasn't a Jew.

When they came for me,
there was no one left to speak out.

By Martin Niemöller
 
Kulikua na haja ya ku_reply maelezo yote hayo? Tumia kichwa kufikiri na si kufugia nywele tu.
Message delivered.Baadhi ya Watanzania mna wivu sana hasa mnapoona wenzenu wanafanya mambo ya maendeleo.Akijenga nyumba nzuri au akinunua gari la kifahari mnasema kaiibia kampuni.Utajiri au kujenga nyumba nzuri ya kifahari si mpaka uwe umetokea au kukulia kwenye familia kama za kina Makamba nikimnukuu mleta mada hii hapa JF.Fungukeni macho hivyo vitu kama kujenga nyumba nzuri,kununua magari ya kifahari vinafanywa na mtu yoyote na si mpaka vifanywe na watoto ambao ni wa vigogo wa serikalini ni juhudi yako tu binafsi ya kujituma na kuwa na mikakati na malengo ya maisha.
 
I suspected...kuna mtu kapigwa chini akaanzisha ile thread. Kila kitu kina muda wake na kusema ukweli, kampuni ya mtu si yako ni yake tu. Kama inawezekana tuwe wajasirimali zaidi kuliko kutegemea kulalamikia kampuni za watu.
 
Kitu kimoja unataka kunishangaza NokiaSiemens ni madai yako kwamba ile barua ya malalamiko iliyopelekwa wizarani na kusambazwa kwenye mitandao na JF ikafika kwamba itatupotosha kwakuwa hatuujui ukweli wa huko kwenu Vodacom/NSN.

Unataka kutuaminisha kwamba hakuna member wa JF ambaye ni mfanyakazi wa Vodacom/NSN? unadhani hatuna ndugu zetu, wake zetu, wadogo zetu, mama zetu, baba zetu ama rafiki zetu wanaofanya kazi huko kwenu na hizo habari zenu tunazifahamu hata kabla hamjaanza kuzifikisha kwenye mitandao?

Usiwe shallow minded kiasi hiki ulichojaribu kukionyesha hapa. Sitaki kuamini kwamba wewe ni mfanyakazi mzawa na kama ni mzawa basi wewe ni msaliti ndio maana umetumwa/umejituma kuja kuwatetea hao wahindi wako. Yani waswahili kutajirika kupitia ajira zao za vodacom/NSN imekuwa nongwa? wewe ulitaka waendelee kuwa makapuku ndipo uridhike?

Mbona hao makaburu wa Vodacom wana vikampuni vyao na wamekuwa wanavipa tender nyingi tu na kuwatajirisha lakini haujalalmikia hilo? au unataka nikwambie kwamba hata kampuni ya mobax ni kampuni ya hao makaburu wa vodacom wametega mirija yao hapo ili wapate pa kutajirikia? Jipange mazee hapa hauna hoja sana sana umeamua kuwapiga majungu wazawa wenzako, pengine umeahidiwa kulipwa chochote kitu kutokana na usaliti unaowafanyia wenzako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nimekusoma mia ya mia hakuna cha kuongeza umoja ndio kila kitu ukipewa nafasi yakujieleza sema pale pale huli wakusome lasivyo unakuwa mnafiki tu kama wazungu walitoa muda wakashindwa kutoa dukuduku uo ni wehu
 
Swali dogo kwa wadau wa NSN/Vodacom, hapo kwenu nimeambiwa hakuna chama cha wafanyakazi kutokana na kurubuniwa na makaburu hadi mkaamua kujitoa/kukisusia chama hivyo kikafa kutokana na kukosa wanachama.

Kama kingekuwepo haya mambo yasingefika hapo yalipofika kwani wao wangechukua nafasi ya kukaa na management kwenye meza kujadiliana hatma ya wafanyakazi kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wowote. Kwakuwa mlikubali wenyewe kukiua chama ambacho kingewatetea sasa mnaona mnavyoburuzwa?
 
Technology siku zote itaendelea punguza watu wa kufanya kazi. Always be advanced with technology
 
Tatizo wabongo wanafuatiliana sana pamoja na kujikomba kwa haoa Wazungu.Unafikiri hao wazungu hawana Kampuni zao binafsi? Tena ni matajiri kuliko hao wabongo.Mimi nilipata taarifa kuna kampuni moja ya wawekezaji hapa nchini mzungu alikuwa anawahadithia Wabongo kwamba amenunua nyumba ya kifahari kwao na pia amenunua na anamiliki ndege huko kwao wakati anafanya kazi ya aina moja na hao wabongo hapa nchini Tanzania.Je angekuwa ni mbongo amenunua nyumba ya kifahari na hiyo ndege mpaka kwenye magazeti mngeandika kwamba hiyo pesa kaiba lakini kwa sababu ni Mzungu mnakaa Kimya.Acheni mawazo finyu hata hao wazungu wameajiriwa kama wabongo na wanatafuta pesa kama hao wabongo kama ni wizi nao wanaiba na kuanzisha kampuni huko kwao na ni matajiri wa kutupwa huko kwao na walikuja huku wakiwa watu wa kawaida tu.
 
Swali dogo kwa wadau wa NSN/Vodacom, hapo kwenu nimeambiwa hakuna chama cha wafanyakazi kutokana na kurubuniwa na makaburu hadi mkaamua kujitoa/kukisusia chama hivyo kikafa kutokana na kukosa wanachama.

Kama kingekuwepo haya mambo yasingefika hapo yalipofika kwani wao wangechukua nafasi ya kukaa na management kwenye meza kujadiliana hatma ya wafanyakazi kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wowote. Kwakuwa mlikubali wenyewe kukiua chama ambacho kingewatetea sasa mnaona mnavyoburuzwa?

Nyie Magwanda si ndiyo huwa mko mbele kuwatetea wanyonge. Sasa mbona kwenye hili la Voda. mko nyuma na kujifanya kuanza kuulizia chama cha wafanyakazi? Au huwa wema wenu unaonekana tu mkisikia mtu ametekwa na kutupwa Mapwepande? Onyesheni roho yenu nzuri kwa hawa jamaa basi ili muonekane kuwa nyie ni watetea haki za wanyonge wa ukweli.
 
Vodacom wote wazungu na waswahili wanapiga dili
Afriking ilianzishwa na kaburu mkewe akawa aiendesha, sasa inaitwa brand fusion. fikiria kampuni inafanya mambo ya sales na marketing ya Voda lkn kila kitu inalipiwa na Voda, kuanzia magari, wese mpaka pango la hiyo kampuni. Mlioko Voda hebu tupeni news zaidi kuna mtu alinitonya eti huyo dietlof alinunua vichwa 250 vya scania akaanzisha kampuni ya uchukuzi hapa bongo. Procurement na warehouse huko vocha zilivyookuwa zinaibwa na kuuzwa mtaani hata kabla hazijawa activated, wakati ule wa Vodafasta iko juu kuna jamaa walipiga billions pale, wakati ule wa simu ya watu jamaa mmoja mtaalam wa simu ya watu akishirikiana na jamaa wa IT&billing wakatengeneza line kibao wakiziita vimondo wakawapa watu mtaani zikawa hazi bill kwenye ssystems za voda wakawagawia watu na kila wiki wakawa wanakwenda kukusanya kil kwa hao watu, wakawa mpaka na containers zao za kupigisha simu wakatengeneza billions of money, huko property nako khaaa mlango wa kilo tano unatengenezwa kwa million mbili, partitions za ofisi kwenye majengo nazo zimewatoa watu vibaya mnoo watu matajiri bana huko VTL. it&billing nako jamaa kaniambia kuna kampuni iko outsourced pale inafanya kazi na Voda wanalipwa cheki moja matata sna kwa mwezi, mmiliki wake alikuwa na ndoto za kuwa director wa IT&billing, lkn akahama akaenda benki moja ya makaburu pale posta ya zamani. Jamanin wa Voda mfunguke basiii mie nilizozipata huko nashea na nyie. customer care nako duuu ntakuja tena ngoja nile njaa inaniuma
 
Safiii......tatizo bongo siku hizi mjanja ni mwenye hela,kazipataje watu hawaangalii.....kwahiyo hawa jamaa pale wamekutana wazungu majambazi na wabongo vibaka.......ila kwakweli pale watu walikuwa wanpiga dili kwenda mbele.........Renee Meza kawazibia watu kinoma

Vodacom wote wazungu na waswahili wanapiga dili
Afriking ilianzishwa na kaburu mkewe akawa aiendesha, sasa inaitwa brand fusion. fikiria kampuni inafanya mambo ya sales na marketing ya Voda lkn kila kitu inalipiwa na Voda, kuanzia magari, wese mpaka pango la hiyo kampuni. Mlioko Voda hebu tupeni news zaidi kuna mtu alinitonya eti huyo dietlof alinunua vichwa 250 vya scania akaanzisha kampuni ya uchukuzi hapa bongo. Procurement na warehouse huko vocha zilivyookuwa zinaibwa na kuuzwa mtaani hata kabla hazijawa activated, wakati ule wa Vodafasta iko juu kuna jamaa walipiga billions pale, wakati ule wa simu ya watu jamaa mmoja mtaalam wa simu ya watu akishirikiana na jamaa wa IT&billing wakatengeneza line kibao wakiziita vimondo wakawapa watu mtaani zikawa hazi bill kwenye ssystems za voda wakawagawia watu na kila wiki wakawa wanakwenda kukusanya kil kwa hao watu, wakawa mpaka na containers zao za kupigisha simu wakatengeneza billions of money, huko property nako khaaa mlango wa kilo tano unatengenezwa kwa million mbili, partitions za ofisi kwenye majengo nazo zimewatoa watu vibaya mnoo watu matajiri bana huko VTL. it&billing nako jamaa kaniambia kuna kampuni iko outsourced pale inafanya kazi na Voda wanalipwa cheki moja matata sna kwa mwezi, mmiliki wake alikuwa na ndoto za kuwa director wa IT&billing, lkn akahama akaenda benki moja ya makaburu pale posta ya zamani. Jamanin wa Voda mfunguke basiii mie nilizozipata huko nashea na nyie. customer care nako duuu ntakuja tena ngoja nile njaa inaniuma
 
Back
Top Bottom