Wafanyakazi wa Usangu Logistics wasomewa amshtaka 460 kwa masaa 6

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Katibu Mukhutasi wa Kampuni ya Usangu Logistics (T) Ltd, Tamal Ramja (24) na Meneja wa Kampuni hiyo, Salum Salim (37) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 460 yakiwemo ya kula njama, kughushi saini na kujipatia Sh428 milioni mali ya kampuni hayo.

Washtakiwa hao wamesomewa kesi ya jinai namba 58/2023 na jopo la mawakili wanne wa upande wa mashtaka wakiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga akisaidiana na Faraja Ngukah, Neema Moshi na Tumaini Maingu.

Ramja na Salim, wamesomewa mashtaka yao leo Aprili 13, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi.

Kesi hiyo iliyochukua saa sita kusomwa mashtaka hayo kuanzia saa 6:30 mchana Hadi saa 11:45 jioni na kuahirishwa hadi Aprili 14 kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Kati ya mashtaka hayo 460, mashtaka 229 ni ya kughushi saini; mashtaka 229 ni ya kuwasilisha nyaraka za uongo; shtaka moja ni la kula njama na lingine ni la wizi.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni shtaka la wizi, ambapo washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Desemba 23, 2020 na Novemba 11, 2022 eneo la Tabata Matumbi wilaya ya Ilala, wakiwa waajiriwa wa Kampuni ya Usangu Logistics (T) Ltd, waliiba Sh428 milioni iliyokana na matumizi mabaya ajira zao.
 
Halafu wanakuja hapa mtaani kwetu wanapaki magari yao kwa gulamu,wanatomba dada zetu,wanavimba na v8 kumbe kampuni ya wezi...
Wameikamua shule yao ya usangu imebaki na mapapai tu..
 
Back
Top Bottom