Wafanyakazi wa umma wanaongezewa mishahara. Je, mimi mwananchi wa kawaida nitafaidi nini na fedha za Serikali yangu?

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Wapendwa, hongereni kwa kazi.

Najaribu kufikiri kwa kina, kisha naishia kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Najiuliza;

Fedha au mali za umma ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti yoyote. Je, Wafanyakazi wa umma kuongezewa mishahara kwa fedha za umma na Watanzania wengi zaidi ya 59,500,000 kubaki katika Dimbwi la umaskini bila kufaidi keki ya Taifa, hiyo si kugawa watu wa Taifa moja katika matabaka kadhaa?

Lakini pia najiuliza; ni kigezo gani kinachotumika kupanga kiwango cha mishahara ya Wafanyakazi wa umma?

Ahsante.
 
Mbona unataja mishahara yao tu na husemi chochote kuhusu kazi wanazofanya zinazopelekea kulipwa hiyo mishahara!? Unaposema keki ya taifa, KWENYE KUITENGENEZA KEKI HIYO KABLA HAIJAANZA KULIWA/KUGAWIWA UNACHANGIA NINI!?
 
Kuna njia kuu tatu za wewe kunufaika na hili ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma kama zifuatavyo.....

1) Kupitia bidhaa au huduma utakazokuwa unawauzia hao watumishi wa umma....

2) Kupitia kuwapiga mizinga watumishi unaojuana nao au kuwa karibu nao....

3) Kupitia shuga mama ambaye ni mtumishi wa umma aliyenufaika na ongezeko la mshahara......
 
Acha roho ya korosho, wakiongezewa mzunguko wa pesa utaongezeka na watu wengine wote watafaidika ikiwemo wafanyabiashara kuongeza mauzo, ajira zisizo rasmi maeneo mbalimbali ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa sababu yote hayo yataongezeka........sasa wewe subiri hapo kunung'unika wenzio wakikamata fursa ili wavune pesa kutoka kwa hao wafanyakazi.
 
Wapendwa, hongereni kwa kazi.

Najaribu kufikiri kwa kina, kisha naishia kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Najiuliza;

Fedha au mali za umma ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti yoyote. Je, Wafanyakazi wa umma kuongezewa mishahara kwa fedha za umma na Watanzania wengi zaidi ya 59,500,000 kubaki katika Dimbwi la umaskini bila kufaidi keki ya Taifa, hiyo si kugawa watu wa Taifa moja katika matabaka kadhaa?

Lakini pia najiuliza; ni kigezo gani kinachotumika kupanga kiwango cha mishahara ya Wafanyakazi wa umma?

Ahsante.
Mlaume baba yako kutokukusomesha waache waliosoma na kutembea kwenye umande wale raha siyo lazima serikali imridhishe kila mtu hususani wewe mbumbumbu
 
Ila watumishi wa umma wanapiga kazi,acha tu waongezewe mishahara..nina mwanangu hapa toka mwezi wa 3 napambana naye a,e,i,o,u nimepiga nimechoka dogo halielewi tu...sasa nikawa nawaza ningekuwa mwalimu wa shule ya msingi,nafundisha darasa lenye wanafunzi 120 kati ya hao 80 nda wawe hii type yangu..duh
 
Wapendwa, hongereni kwa kazi.

Najaribu kufikiri kwa kina, kisha naishia kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Najiuliza;

Fedha au mali za umma ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti yoyote. Je, Wafanyakazi wa umma kuongezewa mishahara kwa fedha za umma na Watanzania wengi zaidi ya 59,500,000 kubaki katika Dimbwi la umaskini bila kufaidi keki ya Taifa, hiyo si kugawa watu wa Taifa moja katika matabaka kadhaa?

Lakini pia najiuliza; ni kigezo gani kinachotumika kupanga kiwango cha mishahara ya Wafanyakazi wa umma?

Ahsante.
Jitahidi uwe mfanyakazi wa serikalini pia kama na wewe unaona unataka uzifaidi directly. Ukienda kupiga ramli chonganishi unaweza kuzifaidi.
 
Wapendwa, hongereni kwa kazi.

Najaribu kufikiri kwa kina, kisha naishia kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Najiuliza;

Fedha au mali za umma ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti yoyote. Je, Wafanyakazi wa umma kuongezewa mishahara kwa fedha za umma na Watanzania wengi zaidi ya 59,500,000 kubaki katika Dimbwi la umaskini bila kufaidi keki ya Taifa, hiyo si kugawa watu wa Taifa moja katika matabaka kadhaa?

Lakini pia najiuliza; ni kigezo gani kinachotumika kupanga kiwango cha mishahara ya Wafanyakazi wa umma?

Ahsante.
Wewe umeshajengewa madarasa kwa hela za mkopo kutoka IMF! Kilichobakia kwako ni kuendelea tu kufyatua.
 
Back
Top Bottom