Wafanyakazi wa TPA watakiwa kushiriki maandamano ya kumpongeza Magufuli

Kweli aisee, utasema walikua viziwi wakati viongozi wa upinzani wakiimba ngonjera za kuangalia mikataba ya kinyonyaji iliyosainiwa na serikali ya ccm., hii sio double standard tu ni unafiki wa hali ya juu
 
Kuna watu watafukuzwa kama hawatashiriki hayo maandamano ya lazima.

Ikiwa yameandaliwa sawa sawa na ukashindwa kuhudhuria ni sawa tu hata mtu wa namna hiyoakifukuzwa kazi. Kwani ili uweze kufanya kazi si lazima ziwepo rasilimali vitu na fedha au? Sasa watu wanapigania hizo rasilimali wewe unaona hayakuhusu kwa kujifanya "msomi"! Unapuuza mchakato wa kudai vyako vilivyotumbuliwa kihovyohovyo na "makupe" wa Uropa na Marekani kwa kuwaachia "wasiosoma na "maskini" (waliosemwa na TWAWEZA kuwa ndio mashabiki wa Magufuli).

Kwa Wakiristo Wayahudi waliokuwa wamemkubali Yesu waliandamana tena watu wakitandika matawi ya mitende barabarani (ingekuwa leo watu wangeweka Khanga na mazulia ili apite juu yake na Farasi wake) kama ishara ya kumkubali.Maandamano yalibarikiwa na hata Yesu.Na ndiyo maana Viongozi wa Kiyahudi walipojaribu kuwanyamazisha waandamanaji wale Yesu akawaambia hawa watu hata mkifanikiwa kuwanyamazisha basi mawe yataimba na kufanya zoezi hilo badala yake.Sasa Wewe unaweza kuyafanya nini mawe? Unaweza kuyapiga maji ya washawasha au ?

Kwa hiyo tumakinike na jambo hili.Hivi wale walioandamana kuunga mkono azimio la Arusha,Azimio la Musoma,na mengineyo wakati ule walikuwa wajinga ila sisi ndio wasomi sana "tuliotukuka?"
 
Nyie wtu mbona wanafiki sana chochote atakachofanya Mh Rais hamna kitu hcho chenu chenye kitu kikowapi mlichofanya mbona hatukioni? Acheni unafiki km hamuwez kpongeza kaeni kmya tu
 
Si maandamano yalizuiwa ama kwa serikali ni sawa ila kwa upinzani ni haramu?? Je intellijensia haijaona dalili za viashiria vya umwagaji damu???
Kama kungekuweko na hicho unachokiita intelijensia msuaji ya rufiji ingekuwa ni historia na watu wasingekufa wengi vile
 
Nyie wtu mbona wanafiki sana chochote atakachofanya Mh Rais hamna kitu hcho chenu chenye kitu kikowapi mlichofanya mbona hatukioni? Acheni unafiki km hamuwez kpongeza kaeni kmya tu
Hahahaahahaha kwahyo hapa wanapinga magufuli kupongezwa au wanapinga hilo tangazo??? Kwanini iwe lazima taasisi za serikali kumsifia magufuli??? Yaani wanatoa order kwani ni lazima?? Je ni haki ya wafanyakazi kuburuzwa kma ng'ombe??? Kma haya unayoysema ndio mawazo ya watanzania wote basi maendeleo tutayasikia rwanda pekee
 
Nyie wtu mbona wanafiki sana chochote atakachofanya Mh Rais hamna kitu hcho chenu chenye kitu kikowapi mlichofanya mbona hatukioni? Acheni unafiki km hamuwez kpongeza kaeni kmya tu
Rais alipiga marufuku maandamano na mikutano. Hawa kwanini wanataka kumjaribu rais?!
 
Kesho asubuhi ni muda wa usafi.

Yaani tz sasa hivi siasa imeshika kasi hata nyimbo za wasanii na filamu zimepotezwa na maigizo ya wanasiasa

Yaani wanasiasa ni wataalamu wa kuigiza na kila siku wanatoa episod mpya.
Na walivyokuwa wataalamu kila episod inayotoka ni kali kushinda iliyopita.

Yaani nikiishiwa bando nakosa raha
 
Ikiwa yameandaliwa sawa sawa na ukashindwa kuhudhuria ni sawa tu hata mtu wa namna hiyoakifukuzwa kazi. Kwani ili uweze kufanya kazi si lazima ziwepo rasilimali vitu na fedha au? Sasa watu wanapigania hizo rasilimali wewe unaona hayakuhusu kwa kujifanya "msomi"! Unapuuza mchakato wa kudai vyako vilivyotumbuliwa kihovyohovyo na "makupe" wa Uropa na Marekani kwa kuwaachia "wasiosoma na "maskini" (waliosemwa na TWAWEZA kuwa ndio mashabiki wa Magufuli).

Kwa Wakiristo Wayahudi waliokuwa wamemkubali Yesu waliandamana tena watu wakitandika matawi ya mitende barabarani (ingekuwa leo watu wangeweka Khanga na mazulia ili apite juu yake na Farasi wake) kama ishara ya kumkubali.Maandamano yalibarikiwa na hata Yesu.Na ndiyo maana Viongozi wa Kiyahudi walipojaribu kuwanyamazisha waandamanaji wale Yesu akawaambia hawa watu hata mkifanikiwa kuwanyamazisha basi mawe yataimba na kufanya zoezi hilo badala yake.Sasa Wewe unaweza kuyafanya nini mawe? Unaweza kuyapiga maji ya washawasha au ?

Kwa hiyo tumakinike na jambo hili.Hivi wale walioandamana kuunga mkono azimio la Arusha,Azimio la Musoma,na mengineyo wakati ule walikuwa wajinga ila sisi ndio wasomi sana "tuliotukuka?"
Walilazimishwa au akili yako haifanyi kazi vizuri?
 
Wasanii wajipange safari hii game ngumu tuwapigie kura sasa wawe wanaingia top twenty ya clouds na radio nyingine
 
Kuna video moja ya Idd Amin ngoja niisearch...alikua analazimisha watu wampende...
 
Walilazimishwa au akili yako haifanyi kazi vizuri?

Akili kutofanya kazi "vizuri" kunaweza kukawa kumeletelezwa na sababu kadhaa.Aidha, Mhusika ni mgonjwa ama Mhusika hajala kwa muda mrefu au jambo jingine lolote ambalo huwa lina-enterfere nervous system za mhusika. Akili kutofanya kazi "vizuri" ni tofauti kutofanya kazi "kabisa" au kufanya kwa maruweruwe mithili ya Computer iliyovamiwa na Virusi.Mimi naweza kuwa katika kundi la akili kutofanya kazi vizuri.Ila Mtu yeyote (anayeunga mkono au anayekerwa) asiyeona umuhimu wa maandamano yaliyoratibiwa vizuri kushirikisha watumishi (na ambao pia ni wafanyakazi) huyo kwa vyovyote yuko kundi la pili la akili iliyotafunwa na virusi.Tangazo halisemi wanalazimishwa bali wanaalikwa.
 
Kwa sasa kila nikisikia ndiooooooo bungeni nakumbuka makinikia siwaheshimu wabunge kama zamani
 
Akili kutofanya kazi "vizuri" kunaweza kukawa kumeletelezwa na sababu kadhaa.Aidha, Mhusika ni mgonjwa ama Mhusika hajala kwa muda mrefu au jambo jingine lolote ambalo huwa lina-enterfere nervous system za mhusika. Akili kutofanya kazi "vizuri" ni tofauti kutofanya kazi "kabisa" au kufanya kwa maruweruwe mithili ya Computer iliyovamiwa na Virusi.Mimi naweza kuwa katika kundi la akili kutofanya kazi vizuri.Ila Mtu yeyote (anayeunga mkono au anayekerwa) asiyeona umuhimu wa maandamano yaliyoratibiwa vizuri kushirikisha watumishi (na ambao pia ni wafanyakazi) huyo kwa vyovyote yuko kundi la pili la akili iliyotafunwa na virusi.Tangazo halisemi wanalazimishwa bali wanaalikwa.
Kweli utakuwa na virus kichwani, unakumbuka ulichokiandika mwanzo?
 
Back
Top Bottom