Wafanyakazi wa supermarket huko Moshi waandamana kupinga rushwa ya ngono wanayoombwa na boss wao

Texas Tom.

JF-Expert Member
Jun 8, 2013
510
273
WAFANYAKAZI wa Supermarket ya Nakumatt, iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wameulalamikia uongozi wa duka hilo kwa madai ya kuwanyanyasa na kuwaomba rushwa ya ngono.

Wafanyakazi hao ambao tayari walishafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama walidai wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono na Meneja Mkuu na na msaidizi wake.

Walisema imekuwa kawaida kwa kila msichana anayefika kuomba nafasi kazi, lazima aombwe rushwa ya ngono huku wanaume wakitakiwa kinyume na maumbile: "Kila msichana anaefika hapa kuomba nafasi ya kazi, anaombwa rushwa ya ngono ndipo apatiwe kazi huku wanaume wakiingiliwa kinyume na maumbile," walisema.

Aidha walisema sababu iliyowafanya wafikie maamuzi ya kuandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa


kutaka msaada ni kukithiri kwa vitendo hivyo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Meneja wa Nakumatt Moshi, Alfrick Milimo alikanusha tuhuma hizo na kudai kwamba zote hizo ni njama za kupakana matope za watu wasiolitakia mema duka hilo.

Alisema kumekuwa na watu wanaozunguka kuwashawishi wafanyakazi huku akikumbushia matatizo yalitokea kipindi cha nyuma kati ya uongozi na wafanyakazi wake na kuwa tayari wameshabaini njama hizo.

Alisema katika duka lake kuna wafanyikazi wa Kenya na Tanzania lakini mara nyingi tatizo linatokea pale wanapowalazimisha Watanzania kufanya kazi maana wengi hawapendi kufanya kazi bila kushurutishwa:

"Niko hapa kwa ajili ya kuwafundisha, kuwaonya na kuwaelekeza lakini inaonekana kuwa unapofanya hivyo unaonekana kuwa wewe ni mbaya na wanafika kazini na mavazi yasizoendana na maadili ya kazi pia wanasinzia kazini," alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi hao na kuahidi kuyashughulikia.


Alisema tayari ameshaagiza Idara ya kazi kulifuatilia suala hilo kwa karibu na kutoa taarifa mapema ikiwa ni pamoja na idadi kamili ya Watanzania na Wakenya wanaofanya kazi katika duka hilo.

SOURCE: nimeyaokota huko mpekuz

 
Wizara ya kazi ni MFU vitendo wanavyofanyiwa wafanyakazi wa secta binafsi ni vya kutisha.
Mfano wahudumu wa ndani mpaka leo ni mshahara wa 15000 mpaka 40000/- kwa mwezi na manyanyaso juu je hawalioni hili.
 
Jamani serikali iangazie swala hilo mapema kuwanusuru na maovu hayo ama basi hata ukweli ujulikane!
 
Ndio maana yake.

Na mimi kuna mkenya nataka kumuajiri kwenye shamba langu lazima nimle kiboga, haiwezekani wawabandue wachaga ambao ni shemeji zangu halafu mimi nimchekee huyu mkikuyu

Thubutu; mchagga wa wapi atakubali kuliwa kiboga? Nenda kaulize utakuta men zinazijiachia ni wakutoka nje ya Knjaro
 
Kazi ni Kazi.... Hivo hata wakenya wamegundua kuwa tunaSinzia kazini ? Wasije kuchukua nchi yote kuipeleka kwao kama kimada!!
 
Utajichafua bana, achana naye tu

Nitamkodia hata sosoliso ampige kiboga, siwezi kuacha hii nafasi, lazima Watanganyika tusawazishe bao kwa huyu Mkikuyu. Tena nitataka ampinde kweli kweli ili ajue kuwa kuna Watanganyika mbavu nene wenye misuli inatisha mbaya
 
Last edited by a moderator:
mbona malalamiko hayana ushahidi,ilitakiwa waweke mtego live kisha watoe malalamiko hayo!ila kiukweli wakenya wamechukua nafasi nyingi za kazi tanzania kwa sasa,mahoteli,maduka,mabenki,kampuni za insurance,utalii,mashule zimeajiri wakenya kwa wingi kuliko watanzania.Watu wa uhamiaji mpo huyo kakiri kuajiri wakenya katika duka jee sheria zinaruhusu kada ya shopkeeper kuwa foreigner?Duu hapo kwenye wanaume kuombwa kabaang ili apate ajira ndiyo leo naisikia ni kali ingekuwa na tego ingependeza zaidi au hata record ya huyo meneja akiomba hiyo tiGO
 
malalmiko yanaweza kuwa ya kweli au la. Ila kuna kaukweli kuwa wa Bongo ni wavivu kazini!!! Hata Unilever hapa Dar walianza na waBongo lakini kila mara ruksa nimefiwa na mke wa mpwa, naumwa huku dalili hazionyeshi mtu kuumwa etc. Wakaleta waKenya wachapa kazi kila jioni ikifika maboxi ya sabuni hayooo yanajaa godown.

CDM mkiingia madarakani muanze na hili la uvivu na utor kazini. Mtu ni lazima ale jasho lake..ebo!
 
Tatizo la sisi WaTZ ni kweli ni wavivu na watu wapenda Majungu ya kutaka kujua fulani kala nini jana leo fulani amevaa nini! Wakenya watatupiga bao tu tupende tusipende!

My take: Naunga mkono hii hoja! Kwani kazi ni baba yako!

Alisema katika duka lake
kuna wafanyikazi wa Kenya
na Tanzania lakini mara
nyingi tatizo linatokea pale
wanapowalazimisha
Watanzania kufanya kazi
maana wengi hawapendi
kufanya kazi bila
kushurutishwa:
 
mbona malalamiko hayana ushahidi,ilitakiwa waweke mtego live kisha watoe malalamiko hayo!ila kiukweli wakenya wamechukua nafasi nyingi za kazi tanzania kwa sasa,mahoteli,maduka,mabenki,kampuni za insurance,utalii,mashule zimeajiri wakenya kwa wingi kuliko watanzania.Watu wa uhamiaji mpo huyo kakiri kuajiri wakenya katika duka jee sheria zinaruhusu kada ya shopkeeper kuwa foreigner?Duu hapo kwenye wanaume kuombwa kabaang ili apate ajira ndiyo leo naisikia ni kali ingekuwa na tego ingependeza zaidi au hata record ya huyo meneja akiomba hiyo tiGO


Kama hataki achape lapa. Toa kabang upate kazi.
 
Tatizo la sisi WaTZ ni kweli ni wavivu na watu wapenda Majungu ya kutaka kujua fulani kala nini jana leo fulani amevaa nini! Wakenya watatupiga bao tu tupende tusipende!

My take: Naunga mkono hii hoja! Kwani kazi ni baba yako!

Alisema katika duka lake


Kwahiyo uvivu wao utisha kwa kuombwa utamu?
 
wachunguzwe haraka, ile intelejensia ya polisi hapo ndo sehemu yake, nanyi msije kamatwa na rushwa kwa hili
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom