Wafanyakazi wa Serikali pamoja na Taasisi kaeni chonjo, Rais Samia anawaangalia kwa"Jicho la Tai

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
595
1,000
Waraka mfupi kwa wafanyakazi wote wa Serikali na Taasisi zote Nchini

Toka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea kijiti ameanza na jambo moja la msingi nalo kurudisha mifumo ifanye kazi

Kwahiyo watendaji wote ambao ni wabadhirifu wa pesa za Umma na ambao walizoea kufokewa zama hizo watambue hii awamu ya Rais Samia imekuja kivingine

Rais Samia anaitaji kila mmoja kwa nafasi yake ajitume, awe mbunifu na kila mmoja kutimiza wajibu wake

Pindi panapotea ubadhilifu wowote wa mali za Umma utambue kuwajibika haraka huku Takukuru wakitimiza wajibu wao Mkuu...

Kwahiyo watendaji wote wa Serikali na Taasisi watambue Mh Rais Samia Suluhu sio mpole au madhaifu bali anaitaji kila mtu atimize wajibu wake na mifumo ifanye kazi

CAG mwako ujao atamkabidhi Mh Rais Taarifa ya Fedha ya kipindi chake cha mwaka 2021na 2022 na hapo ndio wengi mtamjua vizuri Mh Rais Samia Suluhu Hassan...

Alex Fredrick
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom