Katika hali isiyokuwa ya kawaida mpaka kufikia leo tarehe 24 December 2008, wafanyakazi wa serikali hawajapata mishahara yao.Wengi wanaonekana kukerwa na hatua hii ya serikali,huku wakihoji kwa nini serikali imewafikisha hapo huku ikijua wazi kwamba kesho ni mwanzo wa sikukuu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo,yaani Christmas."Mwezi uliopita serikali ilipa mishahara kuanzia tarehe 19, iweje mwezi huu washindwe?Huu ni uzembe tu!" Walionekana wakilalama wafanyakazi."Serikali haijali kabisa wafanyakazi wake,sasa katika hali kama hii, ufisadi utakwishaje?'',waliendelea.Ninaunga mkono kwa asili mia moja hoja za wafanyakazi hawa,hasa ikizingatiwa kwamba mimi mwenyewe ni mfanyikazi wa serikali.Si busara kwa serikali kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara yao mapema hasa katika kipindi "sensitive" kama hiki,yaani kipindi cha Christmas,tena bila maelezo yeyote.Sasa wafanyakazi waieleweje serikali yao,ni kuwakomoa au vipi?