Wafanyakazi wa NMB wahukumiwa kifungo cha miaka 28 jela

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka 28 jela kila mmoja wafanyakazi wa Benki ya NMB.
Wafanyakazi hao, Mtoro Midole na Daudi Kindamba wamehukumiwa leo Jumatatu Oktoba Mosi, 2018 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka ya wizi, utakatishaji wa fedha na kuisababishia benki hiyo hasara ya Sh1.03 bilioni.



Hukumu hiyo imeandaliwa na hakimu mkazi mwandamizi, Godfrey Mwambapa na kusomwa leo na hakimu Mkuu, Wanjah Hamza.
Akisoma hukumu hiyo, Wanjah chini ya sheria ya kanuni ya adhabu aliamuru washtakiwa hao mbali na adhabu ya vifungo hivyo pia walipe kiasi cha hicho cha fedha.



John Kikoka aliyekuwa miongoni mwa washtakiwa hao, aliachiwa huru baada ya mashahidi 21 wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ya jinai namba 118 ya 2014, kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.



Hakimu Wanjah akiisoma hukumu hiyo, amesema washtakiwa Midole na Kindamba wamekutwa na hatia katika shtaka la wizi ambapo aliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja.
Katika shtaka la kutengeneza miamala ya uongo, ambalo linamkabili mshtakiwa Midole pekee, Hakimu Wanjah amesema atatumikia kifungo cha miaka 10 jela.


Katika mashtaka ya utakatishaji wa fedha, Hakimu Wanjah amesema mshtakiwa Midole na Kindamba wamekutwa na hatia katika shtaka moja moja, kati ya mawili mawili yanayowakabili hivyo kila mshtakiwa atalipa faini katika kosa moja Sh500 milioni hivyo katika mashtaka mawili kila mshtakiwa anapaswa kulipa Sh1 bilioni ama kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.



Hakimu Wanjah katika shtaka la kusababisha hasara ya Sh1.03 bilioni kwa benki ya NMB, aliamuru kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh5 milioni ama kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.



Awali, kabla ya Hakimu Wanjah kusoma hukumu hiyo, wakili wa Serikali mwandamizi Kishenyi Mutalemwa aliieleza mahakama hiyo kuwa hana kumbukumbu za makosa ya nyuma ya washtakiwa hao.



Wakili Kishenyi ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu ya kiwango cha juu kwa washtakiwa hao, katika kila kosa walilotiwa hatiani kama Matakwa ya sheria yanavyotaka.



Amebainisha lengo la kuomba adhabu hiyo ni mshtakiwa wa kwanza ambaye ni mfanyakazi wa benki ya NMB na amekasimiwa na kuaminika kutunza fedha za wananchi na kwamba kosa la wizi na utakatishaji wa fedha imekuwa ni tishio kwa uchumi nchini hasa ukizingatia kiwango kikubwa cha fedha kilichohusika katika kesi hiyo.



Pia, ameiomba mahakama itoe amri kwa washtakiwa hao kurudisha fedha walizoisababishia hasara benki ya NMB.
Hakimu Wanjah alipowataka washtakiwa hao waongee chochote kabla ya kupewa adhabu hizo, Midole ameiomba Mahakama iwafikirie kwani wamekaa mahabusu kwa miaka minne kwa sababu mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili ni miongoni mwa mashtaka yasiyo na dhamana kwa mujibu wa sheria.



Pia, ameiomba mahakama impatie nakala ya mwenendo wa shauri hilo na nakala ya hukumu kwa sababu anakusudia kukata rufaa.


Kindamba aliomba mahakama iangalie muda waliokaa mahabusu huku akiomba kupatiwa mwenendo wa shauri hilo na hakala ya hukumu kwa kuwa anakusudia kukata rufaa.
 
CAG akiiona hii ataomba kesi nyingine za upotevu mkubwa wa fedha za umma kupelekwa mahakamani haraka sana.
 
Wazazi tuangalie haya majina tunawapa watoto jamani......MTORO MIDOLE!!!!
 
Back
Top Bottom