Elections 2010 Wafanyakazi wa New Habari kumpigia kura Dr Slaa

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Jamani hii nimepata kali sasa hivi: Jamaa yangu kutoka New Habari (inayomilikwa na fisadi RA) sasa hivi kaniarifu kwamba wafanyakazi wote pale wameamua kumpigia kura Dr Slaa siku ya Jumapili – na hiyo wanaifanya siyo siri tena.

Wanasema wamechoshwa kucheleweshewa mishahara mara nyingine baada ya siku 60 au zaidi ndiyo wanalipwa, tena nusu nusu.

Wanasema magazeti hayauzi kwa sababu ya headline zisizokwenda na wakati na RA mwenyewe hata haonyeshi kujali hilo.

Wanasema RA mwenyewe ana watu wake pale kama watatu tu ndiyo wanaoweka stori anazopenda yeye.

Mambo hayo!!!
 
wao wakapige kura sio kuleta umbea na majungu

wanatumika kama madaraja na wanafaidi wengine
 
Kura zao ni siri, hata wakisema saizi ni kama kujikosha tu. Kama ni kweli basi ni uamuzi wa busara.
 
Mimi najua kuna wapiganaji wengi pale ila wanalazimika kukubaliana na upuuzi wa RA na vibaraka wake MUHINGO na BALILE ili kulinda unga wao. Najua asilimia kubwa ya waandishi na wahariri pale NHCorp. watampigia kura Dr Slaa, kama ambavyo wengi tuliopevuka tutafanya.
 
Ndiyo tatizo la kutumia mafisadi. Kama kuna wazalendo wa kweli hapo ni lazima wataacha kazi manake kufanya kazi za kitumwa kama hizo kunapunguza raha ya kazi.

Tunawashukuru sana wafanyakazi kwa uamuzi wenu wa kumwaadabisha kiongozi wa mafisadi kwa kumnyima kura kura rafiki yake mkwele siku ya Jumapili tarehe 31.
 
Zak Heshima mbele mzee!

Ninachelea kuamini hii story kwa sababu mbili:- 1) Hili gazeti bila kificho ni ANT-SLAA na CHADEME na hiyo iko wazi kwa mtoto mdogo, kitu kilichopelekea mauzo kushuka sana, kwa sababu ya propaganda. 2) New Habari Corp SI mali ya serikali, ni kampuni binafsi.
 
kimsingi mambo yote wafanye waandike lakini wakumbuke taifa kwanza maana hata wao wamo humo ktk taifa hilo hilo... tafadhali kura kwa slaa pekeeeeeeeeeeeee. msiogope mabadiliko jamani:bowl:
 
Wajilipue after all RA hatakuwa nyuma yao kuwaudit kama wamekipigia chama chake au sio
RA nae mihera yote iyo analeta ubahiri
 
Jamani hii nimepata kali sasa hivi: Jamaa yangu kutoka New Habari (inayomilikwa na fisadi RA) sasa hivi kaniarifu kwamba wafanyakazi wote pale wameamua kumpigia kura Dr Slaa siku ya Jumapili – na hiyo wanaifanya siyo siri tena.

Wanasema wamechoshwa kucheleweshewa mishahara mara nyingine baada ya siku 60 au zaidi ndiyo wanalipwa, tena nusu nusu.

Wanasema magazeti hayauzi kwa sababu ya headline zisizokwenda na wakati na RA mwenyewe hata haonyeshi kujali hilo.

Wanasema RA mwenyewe ana watu wake pale kama watatu tu ndiyo wanaoweka stori anazopenda yeye.

Mambo hayo!!!

Wakati muafaka wa kufanya mabadiliko ukiwadia huwa ni vigumu mno kuyazuia.:peace:
 
Back
Top Bottom