Wafanyakazi wa ndani

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Wafanyakazi wa ndani ni watu muhimu sana katika familia zetu. Hushughulika na kupika, kufua, na unakuta ndie anabaki na mtoto ikiwa baba na mama wanafanyakazi. Ni vizuri tukawaheshimu na kuwafanya kuwa ni sehemu ya familia yetu.

Familia zinatofautiana, zipo familia zinaaowaona wafanyakazi wa ndani kama watumishi. Kwa upande wangu ninalaani kitendo hicho. Tuwape haki. Si kuwatumikisha bila kuwapa ajira yao. Walipwe kulingana na makubaliano walioekeana baina yao. Wakati mwingine wafanyakazi wa ndani huwa ndio wa mwisho kula na hata kulala. Wao ni binadamu kama wengine huwa wanachoka na wanahitaji muda wa kupumzika.

Swali: Je hayo yanatokea kwenye familia zetu.
Ni nini kifanyike?
 
Hawa watu wana mabaya yao na mazuri yao!I had one of them and I treated her like family and she betrayed me.She started bringing men into the house and doing lots of nasty things including kuiba and exposing the family skeletons.She was a headache!Once anapojua mji kwisha habari yake!
Ni bora kuwatreat kama Wahindi wanavyofanya maana heshima itakuwepo!
 
nakuunga mkono kevo! hakuna watu wabaya kama hawa tena wa siku hizi ni balaa! utamtreat km ndugu mwisho wa siku unalia!mm nilikua na wangu anaiba, analeta wanaume ndani tukitoka tu hivo hadi unarudi mtoto hana alichofanyiwa kisa anashinda na bwanake ndani yaani alitengeneza familia ndani ya familia, kutaamaki mtoto anadhoooooooooofu, nae ana ujauzito! nashukuru mungu malipo duniani kwani kijana alompa mimba ni choka mbaya, yeye hausgel ndo alikua anamlea kwa pesa zangu! sasa kaletwa na wazazi wake kuishi na familia ya huyo kijana ! anajuta..anataka kumzoea wasasa ili amfundishe kale kamchezo kakuiba vyakula kuwapa majirani, mikaa..mafuta yaani nilikua nalisha familia kama 3 kisa hausgel!
 
Changamoto zinazokuja na hawa watumishi wa ndani ni nyingi lakini ukweli unabaki kwamba ni watu muhimu. Nini kifanyike?
1. Chagua mtumishi kwa uangalifu sio kumkubali kila anayeletwa ili mradi ni binti
2. Weka masharti na taratibu wazi pale anapoanza kazi na endelea kuzifuatilia
3. Mshitukize(ambush) mara kwa mara nyumbani kuhakikisha anafanya kama mlivyokubaliana
4. Mheshimu na mlipe vizuri na pia umpe prospects za kumfikisha hatua bora kama vile utamsomesha akikaa nawe miaka kadhaa, utamfungulia biashara n.k Hivi ndivyo vinavyompa matumain ili anedelee kukutumikia na si vinginevyo
5. Muoneshe kwamba unamjali kama mwanafamilia
6. Ukiona halekei kuwa kama unavyomtaka mtimue kabla hajakusumbua!!!!
 
Well ni binadamu kama sisi na kweli hatulingani ... wengi leave horrible scars in many families like i read sometime in the news papers kwamba house girl mmoja alimuambukiza mtoto ukimwi kwa makusudi

Huwa tunaumia because wengi wetu hatujui backgrounds za wafanyakazi hao na walikotoka .. so wanakuwa na shida ya kazi na kama kawaida mtu anakuwa na ulazima wa kuwachukuwa ...maana in most cases bila wao then you are rendered helpless ... so unajikuta kwaajili ya shida unamchukuwa mtu ambaye humjui background yake .. most of them wanaongopa where they come from hata jina wanabadilisha ... akikuibia unaenda kwa aliyemleta pia anakuambia kwamba hakumjua vizuri ... in the long run unabaki kuchanganyikiwa

Lakini all in all this doesnt give one a ticket kuwatesa .. treat them well because ameshikilia roho zenu wote .. imagine anapika yeye .. akikuwekeeni sumu mkafa nyumba nzima .. wengine pia huhamisha mashambulizi kwa watoto .. ukiondoka tu mtoto anapigwa kama punda ... hapa kitakacho kulinda ni kumtendea wema .. maana kuna wakati utamsuta atasita kufanya ubaya zaidi ... just be human with them because wengine wanakuwa wazuri mpaka tunawaozesha kwenye familia zetu
 
Wale wanaosema ni wafanyakazi wa kazi za nyumbani ni muhimu hawajakosea, na wale wanaosema hawa watu ni wabaya sana pia hawajakosea. Kila mmoja anazungumzia kutokana na yaliyomkuta.

Lakini kwa kifupi hawa watu wanapochukuliwa huko makwao huwa ni watu safi wasio na kasoro. Kasoro zinakuja kutokana na majirani huku tunakoishi. Mimi nilikuwa na binti mmoja alikuwa binti mwenye adabu sana na mwenye bidii ya kazi na nilikuwa namlipa vizuri na kwa wakati muafaka. Nikitoka nilikuwa namuacha na mwanangu ambaye anasoma.

SAFARI YA KWANZA: Alikuja kijana mmoja wakati mimi sipo akamhadaa kwamba angemuoa ili aachane na mateso ya kufanya kazi za ndani. Ingawa mwanzoni aliwahi kunieleza kuwa hana ndugu hapa mjini ilifika wakati akawa anaaga kwamba anaenda kumtembelea shangazi yake. Nikawa namruhusu. Baada ya muda akaniomba nimruhusu aniletee mgeni anayetaka kumuoa. Kwanza sikutaka kushangaa nikamkubalia. Kijana akafika pale nyumbani, nilipomsaili yule kijana nikagundua ni muongo sana. Lakini sikutaka kuyaweka peupe mapungufu yake. Alipotoka nikamkalisha yule binti na kumpa ukweli kwa kile nilichogundua kwa kijana yule. BINTI alipinga vikali akatamka kwamba namuonea wivu. Nikamruhusu ili aende akayaone.

MIEZI SITA BAADAYE: Baada ya miezi sita kupita akiwa ni Mrs wa yule kijana siku moja nikiwa nyumbani saa mbili usiku niligongewa mlango kufungua nikaona ni yule binti. Nikamkaribisha ili nisikie baada ya kumuona amekwisha sana nikajua lazima kuna jambo limemkuta. Akaketi na kunihadithia yote. Nilikaa kimya nikimsikiliza. Alipomaliza nilimjibu kwa neno moja tu "UNAMSINGIZIA" kama ambavyo yeye alivyoweza kunijibu kwamba ninamuonea wivu.

NAMSAMEHE: Hata hivyo nilimsamehe nikampokea.

JARIBU JINGINE: Safari hii kulikuwa na mpangaji mpya nyumba ya jirani, yeye alikuwa ni mtu wa kutimua wafanyakazi wa ndani kila baada ya muda mfupi. Alipoona mimi nimepata binti wa kufanyakazi za ndani alianza kuwa karibu nami. Kipindi chote hiki huyu jirani yangu alikuwa hajawahi kumuona binti wa kazi pale nyumbani kwangu zaidi ya mdogo wangu niliyemuomba aje kunisaidia wakati huyu binti alipoenda kuolewa.

HADAA NYINGINE: Huyu jirani yangu alifanya kitu kibaya tena kwa kumuandalia sendoff feki binti huyu kwamba angeweza kumsaidia akaolewa na kijana fulani jirani yetu. Wakamhadaa kwamba wangemfanyia send-off nzuri akaolewa kuliko kufanya kazi za ndani binti kama yule. Nilipopata habari hizi sikutaka kumshawishi binti juu ya hadaa ile nilimvaa moja kwa moja jirani yangu kwamba anachofanya si vizuri, kulitaka kutokea ugomvi kati yangu na jirani yangu. Nilichofanya ni kumsafirisha huyu binti kwao, cha ajabu baada ya siku tano binti akawa pale mitaani. Akaolewa na kijana ambaye pia alikuwa hamfahamu vizuri. Siku moja kijana alikwapua simu ya mtu akakimbizwa hadi kwao ambapo ni pale alipokuwa akiishi na yule binti. Kwa kweli kama si sisi majirani kusuluhisha basi yule kijana angeweza kuuliwa na wananchi wenye hasira kali. Kwa kuwa nilikuwa nimemuonya juu ya kutokukurupukia maisha ya ndoa kwa mtu asiyemjua binti huyu alibakiakilia na kutamka kwamba huenda hana bahati. Lakini ukiangalia ukweli ni kwa sababu ya ULIMBUKENI TU. Hivyo hawa watu zaidi ya dhiki pia kinachochangia ni kutokuwa na msmamo.
 
Kama kuna masalia ya biashara UTUMWA Nchi hii inafanywa kwa hawa wanaoitwa WAFANYAKAZI wa NDANI. "Mishahara" duni; mazingira magumu sana ya kazi; manyanyaso ya kila aina (yakiwemo ya kijinsia) toka kwa Mama,Baba wenye nyumba;ndio wao wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala; AJIRA za WAZAWA bado ni mbaya sana.
 

mtumishi/mfanyakazi wa ndani ni kipimo tosha cha kupima uwezo wako wa kumuongoza binadamu mwenzako. Take it as a challenge. Ujuzi pekee alionao huyo (mara nyingi) binti, mara nyingi ni basic house chores. kazi uliyonayo ni kuhakikisha anaelewa majukumu yake,wajibu wake na mipaka ya kazi zake.

utakuta (hasa) kina mama wengi, ma house gal wao ndio 'punching bags' za kutupia stress zao. Kutukanwa, kusimangwa, kuwa overworked, kukatwa 'kamshahara', na kunyimwa mapumziko kila wiki, bila sababu za msingi kunapelekea resentment fulani baina ya huyo binti na mama mwenye nyumba.

Experiences mbaya nishazisikia hawa mabinti pindi wanapoamua kulipiza (hasa) kwa infants wanaowalea, ikiwemo kukogeshwa maji ya chooni, kunyimwa chakula ama kulishwa chakula moto, kufinywa au makonzi, na hata wengine wamefikia kuwaua watoto, kama yule mama alokuta mwanae katika oven, au yule alokuwa overdosed, kisa; ...housegal apate muda wa kumaliza kazi anazotwishwa na 'madha-house'

...'to err is human', na kosa linapojirudia rudia tukumbuke tumetofautiana uwezo, hawa watu huo ndio uwezo wao wa kung'amua mambo, la sivyo nao wangekuwa maofisini wakichapa kazi.

Wengine wanaonyanyasika ni madereva wa mabosi, bosi yupo kwenye kilabu/gesti mpaka tisa alfajr, dereva yupo nje anapigana na mbu, na kesho yake 12alfajr awe kazini.

"usimfanyie binadamu mwenzio lile ambalo usingependa kufanyiwa"!
 
Jamani, kama mtu hujawahi kuishi na mtumishi wa ndani usinyooshe kidole kumsema mwingine kuhusu mtumishi wake. Wengi huwa wanawa-treat hawa wasichana kufuatana na jinsi wao aktik maakuzi yao walivyoishi na wasaidizi wao. Ila mara nyingi hakuna formula ya kueleweka.

wengine tume-burn through miles of Housegirls mpaka tukachoka. Ila watu tukubali ukweli, wengi wetu tumekuwa tukiwachukua wasichana wa rika linalofanana sana na ndio maana matatizo tunayoyapata yanafanana sana. Hawa wasichana unakuta wako katika adolesence what do you expect? Unatoa binti kwa wazazi wake akiwa katika rika hilo, maana yake unajiweka katika viatu vya wazazi wake kumlea kwenye kipindi kigumu kama hicho ambacho wao wanahitaji kujitambua.

Ushauriwa bure, nilishaachana na wasichana wakazi walio chini ya miaka 20. Sitaki kuwasikia wala kuwaona. Nikipata msichana kitu cha kwanza ni;

1. una umri gani?
2. Mipango yako ya maisha ni yapi?
3. mategemeo yako ya kutafuta ajira hii ni nini?
4. Una mipango gani na maisha yako ya badaye?
5. Sheria zangu za kazi ni hizi, je utaweza?

Haya maswali hayawezi kujibiwa na mtoto wa miaka 16-18. Wengi wetu tunabaki kuwaahidi maisha mazuri, mavazi, matunzo n.k n.k. Kwa sababu ndicho kinachotafutwa. Nimefanya kazi vizuri na wasichana wa umri kuanzia 23 kwenda juu na sipati matatizo ya kijinga japokuwa kuna wengine wana matatizo yao. Ila kulingana na expectations zangu, sipati mtu wa kuleta wanaume ndani, wala wa kudanganywa na majirani. Mara nyingi majirani wananishangaa kwa kuweza kuishi na watu katika umri huo.

Of recent nilipata binti ambaye ni form 4 leaver, she was the best kwa kweli. Hadi tukawa tunaenda kazini pamoja yeye anaenda kwenye chuo kusomea computer course, akitokea huko anapitia mtoto shuleni. It was wondeful. Na sasa ni sawa na ndugu yangu ame-reseat mitihani yake ya form 4 na kupata credits zake, anajiandaa na mitihani ya A-level. Na kwa kipindi hicho anahangaika na hayo, I had a 40 year old woman and I enjoyed every bit. Sikuwa na haja ya kupiga makelele. So rethink your strategies.

Mara nyingi ni kazi kupata msichana, ila mtu uwe tayari kumlipa vizuri na umheshimu. kazi yako itaenda vizuri bila tatizo.
 
Hapa mimi upande wa matatizo ya hawa watumishi wa ndani yanasababishwa na maboss wao ambao wanaishi nao kwa sababu hii hapa;-
Ukiona yule binti kaanza kwenda kinyume na matakwa yako mwambie pale pale hiki hakikuleta hapa mjini fanya hivi na hivi badala ya kuanza kufoka na kumtukana sijui umekuja hapa hata suruali hujui kuvaa,umekuja na khanga moja hapa sasa ya nini haya??kwani yeye alijua atazikuta suruali hizo.
Hapo mtumishi avunje bilauli au sahani mama yangu we acha tu.
Kama mtumishi kakosea mweleze pale pale akirudia mpe warning kisha last warning akikosea mrudishe kule kule uliko mchukua tafuta binti mwingine hii ndo solution.
Ukimrudisha kule uliko mchukua utakuwa umemwokoa yeye pamoja na maisha yake.
 
Kwa ufupi hawatabiriki.Mfanyie vizuri atafanya kinyume chake,ila si wote,japokuwa wanaofanya vizuri ni wachache sana. Cha muhimu sisi tutimize wajibu wetu kwa kuwatendea vizuri kama binadamu wenzetu. Lingine kuna baadhi yetu tunawatenda vibaya.
 
Back
Top Bottom