Wafanyakazi wa mwendokasi ni kero

Koala

Member
Aug 28, 2011
97
107
Habarini za mchana wana jamvi.Naombeni niilete hii kama kero. Na siku zinvyozidi kwenda naona inakuwa kero kubwa. Kwa wale wanaotumia usafiri wa mwendo kasi hapa Jijini Dar nadhani wameshawaona hawa wafanyakazi wa vituoni ambao wanakaa ktk mageti ya kuingilia na kutokea vituoni.

Wafanyakazi hawa hukaa ktk zile mashine za ambazo tunascan card au tiketi.

Mwanzoni wakati huduma hii inaanza walikuwa msaada kwa wengi ambao walikuwa hawajui matumizi.

Ila kwa sasa naona wanakuwa kero.Ksbb. kwanza wanaziba mahali pa kuscan maana wanaweka viti na kukaa ktk kijisehemu cha kuscan na kuingia kituoni.

Pili watumiaji wengi wanajua matumizi ya scanner, tatu hii ajira yao ni ya muda gani,maana kama ni ya kudumu Je,shughuli yao milele itakuwa kukaa hapo na kusaidia kuscan card za usafiri.

Wahusika naomba mlifanyie kazi jambo hili maana imekuwa usumbufu.
 
mkuu shida yako wale watu waondoke kwakuwa wa2 washajua matumiz ya scanner au ajira yao isitishwe kwa kuwa hawana umuhim tena ?
Yote mawili.Watu washajua matumizi ya scanner na hata kama mtu akikosea abiria mwenzake anamsaidia.Pia ajira isitishwe haina umuhimu tena kwa wananchi zaidi ya usumbufu kwa abiria tu.
 
Yote mawili.Watu washajua matumizi ya scanner na hata kama mtu akikosea abiria mwenzake anamsaidia.Pia ajira isitishwe haina umuhimu tena kwa wananchi zaidi ya usumbufu kwa abiria tu.
poa mkuu watasikia kilio chako
 
Mkuu sisi tunaotoka Mbekenyera tukija huko mjini nani atatusaidia kuscan mkiwaondoa hao watu?
Mkuu,ukisema hivyo basi hii isemwe kama ni ajira ya kudumu na pia wawawekee mazingiraa mazuri ya kazi yasiyoleta kero kwa wasafiri.Pia hv sasa watu wengi mpk wanafunzi wa shule za msingi wanajua kutumia hizo scanner,kwa hiyo kwa nyie wa Mbekenyera hamuwezi kushindwa kupata msaada.
 
Tuwaonee huruma jamani,tukumbuke na wao wana familia zinawategemea,muhimu tuwashauri wajibu wao ikiwezekana waongeze juhudi lakini kuwatoa itakuwa sio jambo zuri
 
Yote mawili.Watu washajua matumizi ya scanner na hata kama mtu akikosea abiria mwenzake anamsaidia.Pia ajira isitishwe haina umuhimu tena kwa wananchi zaidi ya usumbufu kwa abiria tu.
Wengine hatujui.matumizi ya hizo.mashine.

Waachwe tafadhali

Ila watafute namna ya kukaa isiyokera abiria
 
Back
Top Bottom