Wafanyakazi wa Migodi Kanda ya Ziwa watangaza Vita na Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa Migodi Kanda ya Ziwa watangaza Vita na Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Sep 24, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wametangaza kutokuwa na imani na waziri wa kazi Bi.Gaudencia Kabaka pamoja na mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi. Irene Kisaka.
  Ni katika muendelezo wa kupinga utekelezaji wa sheria mpya ya mafao ya kujitoa inayowalazimu wanacahama wa mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF kutochukua mafao yao hadi watakapotimiza umri wa miaka 55. Pia wamedai waziri aliudanganya umma kupitia bunge alipokuwa akitolea ufafanuzi madai yao ya kupinga sheria hiyo.

  Walikuwa wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha wawakilishi wa Jumuiya za wafanyakazi wa migodi ya kanda ya ziwa.
  Wameitaka serikali kuandaa risasi za kutosha, mabomu ya kutosha, makaburi ya kutosha na magereza ya kutosha kwakuwa katika bunge lijalo la mwezi wa 11 kama sheria hiyo haitasitishwa nao hawatakubali kamwe kunyimwa mafao yao kwa kutumia sheria kandamizi.

  Source ITV.
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Moto umewaka tena!!!

  Mimi pia naungana nao kupinga hiyo sheria ya SSRA
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  mbona serikali imekubali kuirejesha bungeni hiyo sheria?
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwezi huo wa 10 lazima kinuke! Wasipoondoa huo upuuzi wao tutaenda hadi The Hague.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aisee ntaungana nao! Ssra wanataka kutufanya sie wajinga
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nasubiri CHADEMA ilaumiwe kuwa iko nyuma ya huu mgogoro!!!!
   
 7. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanaleta siasa kwenye hela zetu. Kama wanataka hela za uchaguzi watafute za kwao.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kutangaza vita na serikali ni kuitambua serikali! Dawa ni kutoitambua kabisa hii serikali ya kihuni kihuni inayongozwa na kiongozi muhuni muhuni!
   
 9. M

  Murrah Senior Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kweli hawa huwakufanya utafiti kabla ya kuleta hizi pumba mbele ya jamii. DC akisema watu wanakuja juu lakini kuna mifano hai kama huu hapo. Wakuu vijana wa hapo Vijijini wanakufa kabla ya miaka 50 pesa zao zitakuaje! Asahau ubunge Tarime
   
 10. r

  raymg JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Me cjaelewa ina maana hii sheria inawahusu watu wa migodin tu? Mbona wafanyakazi wa sekta zingine hawaungan kutetea haki yao? TZ bhana unafki tu......kila kheri wachimba madn wa Geita, tupo pamoja!
   
 11. commited

  commited JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Serikali inacheza na maisha ya watu wake, maana pesa zetu hizo ndizo zinafadhili masafari ya jk, na ndiyo hayo yanayojenga daraja la kigamboni, pesa zetu zinawekezwa kwenye miradi mikubwa yenye kutengeneza faida lakini sisi wachangiaji wa hiyo mifuko wala hatunufaiki na hiyo faida. Katika mapungufu mengi ya hii serikali ni kutokuwa makini na wafanyakazi, anzia walimu, ni mgogoro, madaktari shida, sasa hivi ni matatatizo katika sekta zoote yani ni bora liende. Mtu utakuwaje mazalendo wakati serikali haikujali..... Jk anamaliza vibaya sana wakati wake
   
 12. S

  STIDE JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  CHADEMA AT WORK!!!

  Mh!! Hii serikali hii, Vasco analo!!
   
 13. S

  STIDE JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wasi wasi wangu wasije saritiana kama Madocs!!! Atherwise kila la kheri!!
   
 14. k

  kilaboy Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  Nalisubiri kwa hamu sana bunge lijalo, sababu kubwa ni kusikia juu ya wabunge wasaliti wa wananchi wataizungumziaje sheria hiyo
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nadhani suala hilo lilishatolwa ufafanuzi bungeni na Serikali kuahidi kurudisha bungeni musuada wa sheria ili kurekebisha hali hiyo. Labda kama wafanyakazi hao hawakuwa wakifuatilia vikao vya bunge katika bunge lililopita
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Watanzania wengi ni waoga na wanafiki.

  Wafanyakazi wengi wa Tanzania ni waoga na wanafiki. Wakati wenzao wa migodi wakipaza sauti, sekta nyengine zimetulia kama vile hawahusiki na sheria hii.
  Utaona tofauti yetu na wakenya walimu (Kenya) wamekomaa hadi serikali imekubali kutekeleza madai yao kwa mkupuo mmoja wakati hapa kwetu Mukoba na Oluoch wanawachezesha achimenengule walimu wa Tanzania.

  Katika hili wafanyakazi wa migodi waongoze mapambano ili kuwanusuru 'kunguru' wengi.
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwa uwelewa wangu hilo lilishamalizika kwamba sasa wafanyakazi wataruhusiwa kuchukua chao wakati wowote
   
 18. Root

  Root JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,244
  Likes Received: 12,964
  Trophy Points: 280
  JK ni rahisi
   
 19. mungelehumphrey

  mungelehumphrey Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwanza naunga mkono 100% maana kama serikali imeishiwa watuambie lakini siyo kung'ang'ania pesa zetu hiyo miaka 55 nani atakuwepo kwa kizazi hiki cha sasa kwanza kazi za migodi ni risk tupu mda wowote unaumia au kufukuzwa kazi yaani waache mchezo kabisa na pesa za watu hata mungu atawalaani.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mifanyakazi migine iko iko tu pamoja na viongozi..
   
Loading...