Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa geita wanyimwa kibali cha maandamano kupinga sheria mpya ya mafao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa geita wanyimwa kibali cha maandamano kupinga sheria mpya ya mafao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanta, Jul 27, 2012.

 1. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wafanyakazi wa MGODI WA DAHABU WA GEITA wamenyimwa kibali cha maandano yaliyokuwa yanatarajia kufanyika siku ya jumamosi tarehe 28/07/12 kwa ajili ya kupinga sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.Akitoa taarifa kwa wafanyakazi wa mgodi huo kwa njia ya mtandao, mratibu wa maanadamano hayao (jina limehifadhiwa) alisema kuwa RPC wa mkoa wa Geita amekataa kutoa kibali kwa madai kuwa siku ambayo imepangwa kufanyika kwa hayo maandamano kutakuwa na shughuli zingine za serikali. Aliongeza kuwa pia hawezi kutoa kibali kwa kuwa mkuu wa mkoa pamoja na RAC wa mkoa wa Geita hawapo. "Hatuwezi kutoa kibali kwa ajili ya maandamano ya jumamosi kwa sababu watu hawa wawili hawapo na kuna shughuli zingine za kiserikali, pia hatuna askari wa kutosha kwa ajili ya maandamano yenu hivyo ni bora mkaahirishe ili tupange siku nyingine ya kuwaruhusu mfanye maadamano" alisema RPC huyo mbele ya wawakilishi wa wafanyakazi wakiongozwa na katibu wa TAMICO tawi la mgodi wa Geita wsaliokwenda kufuatilia kibali hicho.

  Awali mkuu huyo wa polisi alijaribu kuwashawishi wawakilishi hao wasifanye maandamano eti kwa kigezo kwamba suala la sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii limerudishwa bungeni kwa ajili ya kwenda kufanyiwa marekebisho lakini walikataa na kumweleza kuwa yeye si msemaji wa serikali juu ya suala hilo nakwamba walichokuwa wanataka wao ni kibali kwa ajili ya mandamano ili wapaze sauti zao kwa wahusika.

  Nimeweka kiambatanisho cha barua ya mkuu wa polisi Geita kuwanyima kibali hicho wafanyakazi.

  Mtazamo wangu,

  Hizi ni hila za wazi za viongozi wa serikali juu ya haki ya watu kuandamana ambayo imeelezwa wazi kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanajaribu kuwaziba watu midomo ili wasihoji haki yao ya msingi ambayo inaonekana kuporwa na watawala. Ni vema serikali ikawa inawasikiliza wanachi wake ambao ndio walioiweka madarakani kuwatumiakia na si kujitumikia wao wenyewe, tutaendelea kupinga sheria hii kandamizi na kama hawatasikia maamuzi tunayo sisi wenyewe kwenye sanduku la kupigia kura muda utakapowadia.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Siku zote waanzilishi wa vurugu ni askari polisi. Wanataka vurugu na wataipata, watajuta.
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  ni mpuzi sana huyo RPC.......lazima mkuu wa mkoa awepo ndio waandamane???!!!
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,408
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Kana kwamba ndio mgeni wa heshima !
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,151
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Irene MD wa SSRA ni punguani kabisa nadhan anafikiri kwa kutumia 0713!! Sheria za kijinga kama hizi kwa mtu mwenye akili timamu hawezi support kabisa,ushauri kwa serikali warudishe pesa walizokopa kwenye mifuko na pia waliowadhamini nao warudishe fedha zetu,kuzuia fao la kujitoa ndio chanzo cha machafuko na pia kipoteza mapato coz watu wengi (wafanyakazi na waajiri) watakua wanacheat hili kupunguza makato ya ppf/nssf coz mtu anajua fika hatozipata,wafanyakazi wataacha kazi hizi na kutafuta nyingine ili wakafoji umri mtu anaanza na miaka 50!! Wabunge ebu jarini maslahi ya wapiga kura wenu,futeni huo upuuzi wa ssra hatutaki kuhusikia kabisa!
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Dawa ni kuanza luddism tu kuharibu mashine
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Ofisi ya OCD bado wanatumia typewriter kuandika barua zao. Hao wezi wa dhahabu zetu wameshindwa hata kuwahonga mashine ya kisasa ya kufanyia kazi.
   
 8. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  RPC Analinda kitumbua chake kisiingie mchanga Maskini. Umaskini mbaya sana.
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  wafanyakazi wamekubali?
   
Loading...