Wafanyakazi wa makampuni ya simu mliopigwa chini njooni mlete mrejesho!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Wale wafanyakazi waliopigwa chini kutokana na mdororo wa uchumi, hasa hawa wa makampuni ya simu, tunawaombeni hapa mje mlete mrejesho jinsi mnavyo cope na maisha ya uraiani!
Kama mlivyomsikia Mh Nape juzi aliposema kuwa maisha lazima yaendeleee, hata sie wenzenu tulivuka hiyo mitihani mnayopitia.
Mimi mwenyewe kibarua changu kilipoota nyasi, huyooo, nilifungasha virago vyangu na kuanza maisha ya kitaaa. Nilichukua kiinua mgongo changu NSSF nikaongezea kwenye vibiashara vyangu, since then down the lane, its two years nayasongesha maisha kitaaa....
Yale mambo sijui ya kutembelea gari la kampuni 24/7 nishayasahau na sasa ni muumini mzuri tu wa public transport na boda boda...
Karibuni kama kuna sehemu mnakwama jinsi ya kuanza kuyajenga ya kitaa msisite kuomba msaada!
 
maisha lazima yaendelee binafsi niligombana na branch manager wangu NMB kanda ya ziwa huko kwa tabia zake za upendeleo kwa wanawake.. kazi nika resign 24 hours nikaenda zangu nssf nikachukua changu na kuongeza nguvu biashara yangu ya kutengeneza mabango.. nashukuru maisha yanaendelea..

sina hamu ya kuajiriwa tena
 
Daaah sema hata sisi tuliokwenye gem la Biashara toka kitambo naona mambo hayaendi kabisa sijui tutakimbilia wap, ila nahisi mwisho wa siku inabidi niwe machinga tu, maana hizi kodi sijui kama ntaweza kuzilipa
 
Back
Top Bottom