RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Wafanyakazi wa hoteli ya kitalii ya Snowcrest ya jijini Arusha wameandamana nje ya hoteli hiyo kwa madai ya kutolipwa mishahara zaidi ya miezi tisa fedha za makato kuto wakilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii huku wakitakiwa kupunguzwa kazini bila malipo.
Wafanyakazi hao wamesema kwa zaidi ya miezi tisa sasa hawajalipwa mishahara huku uongozi ukiwataka wasiingie kazini bila kubainisha sababu wala walipo ya kiinua mgongo hivyo wamemwomba waziri anayehusika na wafanyakazi kuingilia kati mgogoro huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa muda mrefu kwenye hoteli hiyo wamedai kwa zaidi ya miaka mitatu fedha zao hazijapelekwa kwenye makato ya mfuko wa hifadhi ya jamii hali inayo hashiria mwisho mbaya wa maisha yao ambao tayari umeanza kuonekana.
Mkurugenzi wa hoteli ya Snowcrest Wiliam Mollel amesema hoteli iliweka utaratibu mzuri kwa watumishi wake lakini hali imekuwa tofauti na kuahidi kuwa atakutana na wafanyakazi hao siku ya jumamosi ili kuwalipa haki yao.