Wafanyakazi wa gazeti la Uhuru wagoma

Kitungamirwa

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
344
105
Wafanyakazi wa gazeti la CCM linaloitwa uhuru wamegoma kufanya kazi baada ya kudhurumiwa mishahara yao kwa muda wa miezi mitano mfululizo.

Wafanyakazi hao wameamua kugoma baada ya kutolipwa mishahara yao na CCM kwa muda wa miezi mitano mfululizo.

Moja ya wafanyakazi wa gazeti hilo amesema anasikitishwa sana na uongozi wa chama hicho kushindwa kuwalipa mishahara kwa muda wa miezi mitano wakati chama hicho tawala kinapokea zaidi ya bilioni 1.3 kwa mwezi pesa ya ruzuku.

Mfanyakazi huyo aliendelea kuongea kuwa pesa hizo zinaliwa na viongozi wa juu wachache wanajenga majumba ya kifahari na magari ya kifahari huku sisi wanatuambia tuandike habari za propoganda za kuichafua UKAWA wakati huo hatulipwi mishahara hii ni haki?alihoji mfanyakazi huyo.

Lakini wafanyakazi hao waliwarushia lawama nyingi baadhi ya viongozi wa chama kuwa wanatumia madaraka yao vibaya kuendesha taasisi hiyo kama ya kwao binafsi.

My take:

Kama CCM ina uwezo wa kuwadhurumu wafanyakazi kwenye chama chao, Je itakuwaje kwa wafanyakazi wa serikali?

Kama wafanyakazi wa CCM wamedhurumiwa wewe mkulima ulikopwa mahindi na serikali ya CCM.

Je utalipwa?polisi na wanajeshi wastafu mtapata haki zenu kweli kama tu chama tawala kinadhurumu haki za wafanyakazi wa cham chake?

Sasa wewe kijana ambaye hela tu ya kununua MB za internet umeomba kwa wazazi unaishabikia CCM ata bila kujua ccm ina madhara gani endelea utajuta siku ukiwa na majukumu.
 
Na wagome tu si viongozi wao wako bize kutafuta U-Rais. bei ya Dar- Dodoma ya Msaka u Rais mmoja kuchukua fomu inatosha kuwalipa wafanyakazi wa mishahara ya miezi miwili.Duuu hiki Chama kwisha kazi.Hata Mwenyekiti wa chama chenu munayemwandika vizuri hata Safari ya Matumaini imekataa kuwalipa mishahara yenu? Na kumbuka mwaka 2005 mliandika sana Maisha Bora Kwa KILA Mtanzania,sisi tunasota na njaa nzetu nyinyi wa karibu na rangi ya kijani nanyi mnagoma? Mwiteni MAKONDA atamaliza matatizo yenu.
 
Tatizo la wafanyakazi hawa ni kukosa ubunifu, wengeliwapa moyo watia nia zaidi na kufikia 100 then katika hizo wangelipata japo 50% yake ambayo ni kama 50,000,000/- si zingetosha mishahara!?
 
Ndio waache kuandika propaganda za uongo juu ya vyama vingine. Wakiamua kuandika ukweli watalipwa tu. Maana hawa viongozi watawaheshimu. Kwa sasa wanwadharau kwa sababu wao wenyewe hawajitambui. Kutwa kuandika habari nyepesi nyepesi na za kukisifia chama hata kinapoboronga.
Wakome!
 
Mimi nilivyosikia kuna mgogoro wa wahariri wanaomuunga mkono Lowassa na wanaompinga. Mhariri mtendaji, Joseph Kulangwa anamuunga mkono Lowassa amefukuzwa kazi na kina Nape ndio ndipo baadhi ya waandishi wakagoma.
 
Wameishiwa maneno ya kukipamba chama ndo maana hawalipwi! endelee hivo hivo kutowalipa maana habari zenyewe za upotoshaji tu
 
Wana laana ya kupotosha jamii, na wasilipwe tu hadi ufahamu uwapate.
Hao wanaopotoshwa ni asilimia ndogo sana, nasikia circulation ya magazeti yao ni kati ya nakala 1,500 na 5,000 siku mambo yakiwa mazuri. Na nyingi ya hizi ni zile zinazokuwa delivered kwenye maofisi hasa ya umma.

 
Ndio waache kuandika propaganda za uongo juu ya vyama vingine. Wakiamua kuandika ukweli watalipwa tu. Maana hawa viongozi watawaheshimu. Kwa sasa wanwadharau kwa sababu wao wenyewe hawajitambui. Kutwa kuandika habari nyepesi nyepesi na za kukisifia chama hata kinapoboronga. Wakome!
Au ununuzi wa magazeti yao umeshuka sanaa?
 
Kwani gazeti la uhuru limeanzishwa mwaka gani?
Kwani toka lilipoanzishwa walikua hawalipwi?
Na kutokulipwa miezi mitano waliwezaje kwenda kazini?
Kama mshahara ndo chanzo cha kuwafanya waishi mjini hao waandishi
kwa nini wasingetafuta kazi hata kujiajiri kwingine?
Hivi inaingia akilini usilipwe basic yako kwa miezi 5 mfululizo ukaendelea kufanya kazi?
Wenye uzoefu wa kufanya kazi bila kulipwa waje hapa kuchangi,!
Mimi naona SIO KWELI, HAKUNA UKWELI KABISA MIEZI 5 Hapana jamani!
 
Mimi nilivyosikia kuna mgogoro wa wahariri wanaomuunga mkono Lowassa na wanaompinga. Mhariri mtendaji, Joseph Kulangwa anamuunga mkono Lowassa amefukuzwa kazi na kina Nape ndio ndipo baadhi ya waandishi wakagoma.

Kumbe yule Joseph kulangwa kafukuzwa kazi? hatari san hii!! kisa anamuunga mkono Lowassa?
 
Back
Top Bottom