Wafanyakazi wa gazeti la Uhuru wagoma

Pesa za mishahara hazipo lakini za ziara za Kinana na baby wake Nape zipo!

Kwa kuwa wamekuwa wakitumika kama kondom nashauri wasilipwe mishahara yao kabisa.

Kidumu chama cha majambazi.

Waendee na propaganda zao za kupotosha umma,kwani walikuwa hawajui kama mshahara wa dhambi ni mauti......mchuma janga hula na wakwao
 
* VURUGU KUBWA OFISI ZA GAZETI LA UHURU

* KATIBU WA BODI DANIEL CHONGOLO AKIONA CHA MOTO.......

* WAFANYAKAZI WAMFUKUZA NAPE OFISINI..

Leo katika hali isiyo ya kawaida katika ofisi za gazeti la Chama cha Mapinduzi (Uhuru) kumekuwa na vurugu za kila namna hali iliyopelekea polisi kuitwa ili kutuliza ghasia hiyo....

Hali hii imetokea baada ya jana Katibu Mwenezi wa CCM, Nape kumfukuza kazi Mhariri wa gazeti hilo Ndugu Joseph Kulangwa....

Ndugu Kulangwa kwa muda mrefu amekuwa katika mvutano na Katibu wa Bodi Ndg. Daniel Chongolo ambaye ni mpambe mkubwa wa NAPE.... Hii ni kutokana na Kulagwa kuungana na wafanyakazi wenzake katika kudai mshahara ambapo ni zaidi ya miezi mitano (5) wafanyakazi hao wa gazeti la Uhuru hawajalipwa.... Kitu ambacho kinawapelekea kuishi maisha magumu sana mitaani

Leo majira ya mchana Mwenezi wa CCM, Nape alipohudhuria alikutana na hasira za wafanyakazi hao ambapo kama siyo juhudi za askari polisi kunusuru hali hiyo vurugu zaidi zingeweza kutokea..... Hali hiyo ilimfanya katibu wa bodi Daniel Chongolo kukimbia na kutoka nje kupitia mlango wa nyuma ili kunusuru maisha yake dhidi ya hasira za wafanyakazi hao.....

Haya yanatokea huku kesho Kamati Kuu ya dharura inatarajiwa kukaa na kwa taarifa za awali moja ya agenda ni hizi vurugu za gazeti la Uhuru....

Mytake:... Katika kipindi hichi CCM kinapoelekea kwenye uchaguzi wa ndani, ni wazi madai wa wafanyakazi hao yakapata ufumbuzi ili kuondoa sintofahamu katika jamii....
 
wafanyakazi wa uhuru hawajalipwa mshahara wa miezi mitano kwasababu gazeti linaandika upumbavu hakuna mteja ananunua huo uchafu ndiomaana kampuni haina pesa. Nape Nnauye toa pesa mfukoni ulipe wafanyakazi wa gazeti la mandazi.
 
wafanayaki wa uhuru hawajalipwa mshahara wa miezi mitano kwasababu gazeti linaandaika upumbavu hakuna mteja ananunua huo uchafu ndiomaana kampuni haina pesa.
Dah! Mkuu umeniwahi nilikuwa najiandaa kuandika comment kama hii ya kwako. Kwaufupi hapo hakuna mchawi,bali wachawi ni wao wenyewe.
 
* VURUGU KUBWA OFISI ZA GAZETI LA UHURU

* KATIBU WA BODI DANIEL CHONGOLO AKIONA CHA MOTO.......

* WAFANYAKAZI WAMFUKUZA NAPE OFISINI..

Leo katika hali isiyo ya kawaida katika ofisi za gazeti la Chama cha Mapinduzi (Uhuru) kumekuwa na vurugu za kila namna hali iliyopelekea polisi kuitwa ili kutuliza ghasia hiyo....

Hali hii imetokea baada ya jana Katibu Mwenezi wa CCM, Nape kumfukuza kazi Mhariri wa gazeti hilo Ndugu Joseph Kulangwa....

Ndugu Kulangwa kwa muda mrefu amekuwa katika mvutano na Katibu wa Bodi Ndg. Daniel Chongolo ambaye ni mpambe mkubwa wa NAPE.... Hii ni kutokana na Kulagwa kuungana na wafanyakazi wenzake katika kudai mshahara ambapo ni zaidi ya miezi mitano (5) wafanyakazi hao wa gazeti la Uhuru hawajalipwa.... Kitu ambacho kinawapelekea kuishi maisha magumu sana mitaani

Leo majira ya mchana Mwenezi wa CCM, Nape alipohudhuria alikutana na hasira za wafanyakazi hao ambapo kama siyo juhudi za askari polisi kunusuru hali hiyo vurugu zaidi zingeweza kutokea..... Hali hiyo ilimfanya katibu wa bodi Daniel Chongolo kukimbia na kutoka nje kupitia mlango wa nyuma ili kunusuru maisha yake dhidi ya hasira za wafanyakazi hao.....

Haya yanatokea huku kesho Kamati Kuu ya dharura inatarajiwa kukaa na kwa taarifa za awali moja ya agenda ni hizi vurugu za gazeti la Uhuru....

Mytake:... Katika kipindi hichi CCM kinapoelekea kwenye uchaguzi wa ndani, ni wazi madai wa wafanyakazi hao yakapata ufumbuzi ili kuondoa sintofahamu katika jamii....
Nape amezidi ujuaji wangemchapa bakora!gazeti gani la chama kunawatukana makada wote wanampinga membe kudadadeki wauaji kabisa
 
wafanyakazi wa uhuru hawajalipwa mshahara wa miezi mitano kwasababu gazeti linaandika upumbavu hakuna mteja ananunua huo uchafu ndiomaana kampuni haina pesa. Nape Nnauye toa pesa mfukoni ulipe wafanyakazi wa gazeti la mandazi.

Uko sahihi kabisa..... Gazeti limekuwa likiandika upumbavu kisa tu Nape.....

Li Nape limetanguliza maslahi yake binafsi kuliko hata ya chama.... Uhuru saizi limekuwa gazeti la kumnadi Membe
 
Wafanyakazi wa gazeti la CCM linaloitwa uhuru wamegoma kufanya kazi baada ya kudhurumiwa mishahara yao kwa muda wa miezi mitano mfululizo.

Wafanyakazi hao wameamua kugoma baada ya kutolipwa mishahara yao na CCM kwa muda wa miezi mitano mfululizo.

Moja ya wafanyakazi wa gazeti hilo amesema anasikitishwa sana na uongozi wa chama hicho kushindwa kuwalipa mishahara kwa muda wa miezi mitano wakati chama hicho tawala kinapokea zaidi ya bilioni 1.3 kwa mwezi pesa ya ruzuku.

Mfanyakazi huyo aliendelea kuongea kuwa pesa hizo zinaliwa na viongozi wa juu wachache wanajenga majumba ya kifahari na magari ya kifahari huku sisi wanatuambia tuandike habari za propoganda za kuichafua UKAWA wakati huo hatulipwi mishahara hii ni haki?alihoji mfanyakazi huyo.

Lakini wafanyakazi hao waliwarushia lawama nyingi baadhi ya viongozi wa chama kuwa wanatumia madaraka yao vibaya kuendesha taasisi hiyo kama ya kwao binafsi.

My take:

Kama CCM ina uwezo wa kuwadhurumu wafanyakazi kwenye chama chao, Je itakuwaje kwa wafanyakazi wa serikali?

Kama wafanyakazi wa CCM wamedhurumiwa wewe mkulima ulikopwa mahindi na serikali ya CCM.

Je utalipwa?polisi na wanajeshi wastafu mtapata haki zenu kweli kama tu chama tawala kinadhurumu haki za wafanyakazi wa cham chake?

Sasa wewe kijana ambaye hela tu ya kununua MB za internet umeomba kwa wazazi unaishabikia CCM ata bila kujua ccm ina madhara gani endelea utajuta siku ukiwa na majukumu.

Hakuna chama pale; CCM kama taasisi kilikufa siku nyingi ndio maana viongozi wa gazeti hilo nao wameamua kukomba kilichosalia!
 
Uko sahihi kabisa..... Gazeti limekuwa likiandika upumbavu kisa tu Nape.....

Li Nape limetanguliza maslahi yake binafsi kuliko hata ya chama.... Uhuru saizi limekuwa gazeti la kumnadi Membe
Nape Nnauye ameshiriki vema kuleta ukata kwenye hilo gazeti la mandazi hakuna namna zaidi ya kumtosa.
 
Last edited by a moderator:
Uko sahihi kabisa..... Gazeti limekuwa likiandika upumbavu kisa tu Nape.....

Li Nape limetanguliza maslahi yake binafsi kuliko hata ya chama.... Uhuru saizi limekuwa gazeti la kumnadi Membe
Mpuuzi sana Huyu jamaa kazi yake kutanguliza tumbo kwa Membe na Gotham nakuhakikisha gazeti la chama kinampamba membe ushenzinzi mtupu Jakaya sijui huwa anashauriwa na nani kuteua mtu kama Nape
 
Mfanyakazi huyo aliendelea kuongea kuwa pesa hizo zinaliwa na viongozi wa juu wachache wanajenga majumba ya kifahari na magari ya kifahari huku sisi wanatuambia tuandike habari za propoganda za kuichafua UKAWA wakati huo hatulipwi mishahara hii ni haki?alihoji mfanyakazi huyo.

Propaganda za UKAWA ,, yaani hata kijificha hamuwezi .. sintoshangaa ukinambia chanzo cha hii habari ni weye mwenyewe
 
Usicheze na nguvu ya umma, wao si walilifungia mwanahalisi, sasa wananchi tumelisusa gazeti lao, litajifungia lenyewe, hii haihitaji baraza la vyombo vya habari wala George Mkuchika.
 
Back
Top Bottom