Wafanyakazi wa Faidika Limited kizimbani kwa wizi wa Tsh Milioni 700

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
WAFANYAKAZI watatu wa Taasisi ya fedha ya Letshego maarufu kama Faidika Limited, wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la la wizi wa sh milioni 700.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Elisha Tengeni , Donald Kwaya na Elisha Mboka.

Akisoma shitaka hilo, wakili Ngukah aludao alidai kati ya Januari mwaka 2016 hadi Septemba mwaka 2017 washitakiwa waliiba sh milioni 700 mali ya Kampuni ya Letshego Tanzania Limited maarufu kama Faidika fedha ambazo zilifika kwao kutokana na nafasi zao za uwajili.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha mahakamani fedha taslim au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 350.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Juni 30 mwala huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa maabusu.
 
KESI YA 2017 HADI LEO UPELELEZI BADO?
MMEWAPELEKAJE MAHAKAMANI KAMA UPELELEZI BADO?
 
Hela kama izo wanaibaga kidogo kidogo,ndani ya miaka mingi wanajikuta imekua nyingi ivo ya kutosha,na unakuta ata wezi wenyewe awajafanya cha maana kimaendeleo binafsi unajiuliza uyu mtu ela kapeleka wapi
 
sasa sijaelewa apo kwann wasishtakiwe na wamili wa letshengo lkn wanashtakiwa na serikali apo wakili wa serikali anawashtaki kwann
 
Hela kama izo wanaibaga kidogo kidogo,ndani ya miaka mingi wanajikuta imekua nyingi ivo ya kutosha,na unakuta ata wezi wenyewe awajafanya cha maana kimaendeleo binafsi unajiuliza uyu mtu ela kapeleka wapi
Kabisa bwashee ,maana sometimes unadokoa vilakilaki ukija kupigiwa hesabu unaambiwa umeiba million 50 wakati hata passo umeshindwa kumilik
 
Hela kama izo wanaibaga kidogo kidogo,ndani ya miaka mingi wanajikuta imekua nyingi ivo ya kutosha,na unakuta ata wezi wenyewe awajafanya cha maana kimaendeleo binafsi unajiuliza uyu mtu ela kapeleka wapi
Ndio shida ya kuiba kidogo kidogo jioni unaenda kuzinywea bia na washkaji, kuchukua milupo na kwenda tripu magoroto. Mambo yamesanuka huna akiba haya mia, hupati ata mtu wa kuja kukusalimia lupango achilia mbali kukuwekea dhamana, unaenda zako kunyea debe..!!
 
Hela kama izo wanaibaga kidogo kidogo,ndani ya miaka mingi wanajikuta imekua nyingi ivo ya kutosha,na unakuta ata wezi wenyewe awajafanya cha maana kimaendeleo binafsi unajiuliza uyu mtu ela kapeleka wapi
Wafanyakazi wa Letshego wana tabia ya kutengeneza wakopaji feki halafu wanachukua wenyewe pesa.
 
Wezi wengi ndiyo walofanikiwa mjini hapa. Ukitaka halali utasubiria sana

I hope they create a lasting success. What I see around is a vicious circle. Hakuna maendeleo yale tunayoimba yanayotokana na wizi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom