Wafanyakazi wa BoT waliochana noti za Tsh. Bilioni 4.6 hali tete

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,352
8,034
Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabiliwa washtakiwa 13, wakiwemo waliyokuwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bado haujakamilika. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matano, likiwemo kuharibu noti 4.6 milioni kwa kuzichanachana na hivyo kuisababishia benki hiyo hasara ya zaidi ya Sh4.6 bilioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga ameieleza Mahakama hiyo, leo Oktoba 12, 2022, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Mwanga ameieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendeela hivyo wanaomba terehe nyingine kwa ajili ya kutwaja

Hakimu Kabate ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 9, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mariagoreth Kunzugala maarufu kama Bonge, Henry Mbowe maarufu kama Mzee wa Vichwa, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanaheri Omary wote walikuwa wafanyakazi wa BoT na wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Wengine ambao sio watumishi wa BoT ni Alistides Genand, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Rutabilwa. Katika hati ya mashitaka inadaiwa, kati ya Januari 2017 hadi Septemba 30, 2019, washitakiwa wakiwa Watumishi wa BoT, kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Pia inadaiwa, Genand, Mchegage, Chengula, Chihipo na Ishengoma wakiwa si watumishi wa BoT, kwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kwa makusudi, waliwezesha kutendeka kosa la uhalifu wa kupanga.

Katika shitaka la tatu, washitakiwa wote bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo, waliharibu noti 460,000 za Sh10,000 kila moja kwa kuzikatakata zenye thamani ya Sh4.6bilioni Katika shitaka la nne, siku na maeneo hayo, kwa mawasilisho ya kilaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli washitakiwa wote walijipatia faida ya Sh 1.5 bilioni kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo BoT.

Katika shitaka la tano washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia BoT hasara ya Sh 4.6bilioni. Awali, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka sita, lakini Juni 18, 2021, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Slyvester Mwakitalu aliwafutia shtaka la kutakatisha fedha na hivyo kubaki na mashtaka matano.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Decemba 14, 2020.

MWANANCHI
 
Hii tabia ya watanzania ya kuwashangilia na kuwaona wezi wa fedha za umma ni watu wajanja na waliotoboa ndio inaumiza hii nchi.

Jamii ibadilike, mwizi wa fedha za umma ni aibu na fedheha sana huko America ulaya na asia mwizi wa kitu cha umma akigundulika huwa ni fedheha kubwa sana na mara nyingi wanajiuwa wenyewe kabla hata hawajahukumiwa..

Hapa kwetu mtu akiiba fedha za umma mtaani anaogopewa na anapata heshima kubwa sana.
 
Hii tabia ya watanzania ya kuwashangilia na kuwaona wezi wa fedha za umma ni watu wajanja na waliotoboa ndio inaumiza hii nchi.

Hapa kwetu mtu akiiba fedha za umma mtaani anaogopewa na anapata heshima kubwa sana.
Unawasema CCM au? Wezi pekee wanaotamba na kuogopwa ni CCM!
 
Hizi pesa zinazoliwa hivi ni za umma yaani za Watanzania. Kwa vile sasa hivi wananchi wanachangia pesa zao nyingi kwa njia ya kodi kama TOZO, VAT, REA na nyingine kama hizi, hawa wanaoziiba wasipochukuliwa hatua stahiki na haraka SIKU SI NYINGI WANANCHI WATAWACHUKULIA HATUA WANAOWASISITIZA KUCHANGIA PESA.
 
inadaiwa, kati ya Januari 2017 hadi Septemba 30, 2019, washitakiwa wakiwa Watumishi wa BoT, kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu.
Shilingi 4,600,000,000÷ noti 10000= noti 460,000.
Noti 460,000 kwa kuzichana na mkono ingewachukua siku nyingi sana, hapa inaonekana wakawa wanatumia paper cutter ili ku save time.

Mabwege sana hawa
 
Shilingi 4,600,000,000÷ noti 10000= noti 460,000.
Noti 460,000 kwa kuzichana na mkono ingewachukua siku nyingi sana, hapa inaonekana wakawa wanatumia paper cutter ili ku save time.

Mabwege sana hawa
Halafu kuna noti nyingine zenye thamani ya 1.5 bln hawakuzichana wakagawana, ila kwenye mawasilisho pale BoT wakadanganya wamezichana
 
Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabiliwa washtakiwa 13, wakiwemo waliyokuwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)...
Kwenye hilo kundi la wezi asingeweza kukosekana Muhaya na mchaga!

Huu uchunguzi kwa nini unachukua muda mrefu,wanachunguza nini wakati ukweli upo wazi? Noti zilichanwa? Hapa kuna watu wanataka kuharibu ushahidi tu
 
Kwenye hilo kundi la wezi asingeweza kukosekana Muhaya na mchaga!!
Huu uchunguzi kwa nini unachukua muda mrefu,wanachunguza nini wakati ukweli upo wazi?noti zilichanwa??hapa Kuna watu wanataka kuaribu ushahidi tu
Pale BoT tuko na wachaga wengi kuna wengine waliingia kimagumashi wakaanza kutafuta vyeti kwa kujiendeleza wakiwa palepale

Acha tu turudi kwenye mada: HAWA WEZI INATAKIWA WAWAJIBISHWE LIWE FUNDISHO
 
Kuna upigaji mwingine umekua ukifanyika Kwa muda Sasa na unaendelea. Iko hivi, benki zinapopeleka pesa zao BoT, zinakua zimehesabiwa na kufungwa vizuri kabisa, lakini wakiziacha pale BoT baadae inakuja debit note kwamba pesa zilipungua Kwa kiasi flani, na hiyo hua Haina mjadala, akaunti ya benki yenu unatolewa pesa kufidia huo upungufu.

Katika miaka yote nimekua benki, haukuwahi kutokea wakasema pesa zimezidi, wao ni kutoa taarifa tu kwamba zipo pungufu.
 
Kuna upigaji mwingine umekua ukifanyika Kwa muda Sasa na unaendelea. Iko hivi, benki zinapopeleka pesa zao BoT, zinakua zimehesabiwa na kufungwa vizuri kabisa, lakini wakiziacha pale BoT baadae inakuja debit note kwamba pesa zilipungua Kwa kiasi flani, na hiyo hua Haina mjadala, akaunti ya benki yenu unatolewa pesa kufidia huo upungufu.

Katika miaka yote nimekua benki, haukuwahi kutokea wakasema pesa zimezidi, wao ni kutoa taarifa tu kwamba zipo pungufu.

Umeona eee pesa huwa haizidi ila kwao huwa inapungua tu. Huwa hawana mjadala zaidi ya kuwahitaji mlipe
 
Kuna movie inaitwa MADMONEY,mambo haya haya ya kuchakata noti mbovu..

Aisee pesa tam hata iwe chafu vipi
 
Kama hizo zilizochanwa zingekuwa ni zile za Tozo mitandaoni pasingetosha😁

Mwigulu! Mwigulu!😆
 
Back
Top Bottom