Wafanyakazi wa Bandari waandamana Wizara ya Sheria na Katiba leo

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Wafanyakazi Bandari.jpg

TAKRIBAN wafanyakazi 40 kati ya 992 waliopunguzwa kazi Bandari Januari 2008 leo hii wameandamana kutoka Mahakama Kuu ya Kazi, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi Wizara ya Katiba na Sheria wakilalamikia kucheleweshwa kwa kesi yao ya madai dhidi ya uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Wakizungumza na FikraPevu nje ya makao makuu ya wizara hiyo, wafanyakazi hao wamesema kwa miaka nane sasa wamekuwa wakifuatilia madai yao ya kupinga kupunguzwa kazini pamoja na kupunjwa mafao, lakini licha ya madai yao kuonekana kuwa ya msingi, kesi hiyo imeendelea kucheleweshwa.

ISOME ZAIDI HUKU...
 
Kumbe ni wastaafu, ni nimekuja mbio nikijua ni waliopo kazini. Wafanyakazi wa bandari, tra, tanroads, tanapa n.k kuandamana kwao ni sherehe, na mara nyingi huwa ni Mei Mosi.
 
Kazi kweli kweli makali ya maisha yanaumiza wasikilizwe na wapewe stahiki zao.
 
Wanabodi,

Nadhani wakati mwingine tusikimbilie kuhukumu, tunaweza kuwa tunakosea sana. Hawa ni wafanyakazi bado mpaka pale mahakama itakapohukumu vinginevyo kwa sababu moja ya madai yao ni kupinga kupunguzwa kazi bila kufuata sheria na taratibu za ajira, lakini pia wanapinga malipo waliyopewa.

Tunapaswa kujiuliza hata mazingira yaliyosababisha wao kupunguzwa kazi, kwa sababu yawezekana kuna hila, ama inawezekana kulikuwa na agizo la kuwapunguza. Ni muhimu kulifikiria.

Wafanyakazi 992 ni wengi sana kwa idara moja kupunguzwa kwa wakati mmoja. Je, nani anafanya kazi walizokuwa wanafanya? Ndiyo maswali ya msingi.

Hili lililowapata hawa Watanzania wenzetu linaweza kumpata yeyote - labda uwe umejiajiri - lakini as long as you're still employed or seeking employment, anything might happen.

Regards,
Daniel
 
Nyie mlikuwa mnaimba ccm ni ile ile sisi malofa hatuna ajira serikalini acha mnyooke, waambie na wenzako kazi zipo nyingi ata kule dampo zipo kazi za kuokota makopo sio lazima mfanye kazi serikalini
 
Back
Top Bottom