Wafanyakazi wa atcl wavamia ofisi za waziri mkuu


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
Wafanyakazi walioachishwa atcl kwa manufaa ya umma wamevamia ofisi za waziri mkuu leo hii kudai mafao yao baada ya kuachishwa,..hali hii imetokea leo pale ofisi za magogoni karibu na ikulu nikiwa napita kwenye shuguli zangu na mke wangu kufanya shopping nikaona kundi la watu wamejazana mlangoni huku wengine wakiwa na camera,
sikusita kushuka na kwenda kuuliza nini kinaendelea kama wajibu wangu wa Jf nikapata kijana mmoja ambae alinipa maelezo kabla ya hapo alijaribu kuniuliza ni nani natokea wapi baada ya hapo nikaungana nae kujua hali halisi
wafanyakazi hao wapatao 80 walikuwa wamefura getini mwa ofisi ya waziri mkuu huku FFU wakiomba kusogea na kupisha watu wengine waingie,....
Kijana huyo alianza kwa kusema kaaka atupendi kuwa hapa sisi tumefanya ATCL na ukafika muda lazima uondoke tukakubali kuondoka kwa shingo upande kutokana na pesa waliamua kutulipa wizara ya miundo mbinu ikiongozwa na Katibu mkuu wake Chambo ambae aliweka wazi wasipoondolewa mi nafuta kampuni,..swala hili liliwafanya wafanyaakazi wakaanza kutengana na viongozi wao wa chama cha wafanyakazi mpka ilipofika muda na siku watu waakakabidhiwa barua zao,...akukuwa na ubishi ila utata umekuja pale kwenye mafao yetu ya PPF
tulipokuwa tukipewa barua tuliambiwa ndani ya mwezi mmoja na nusu tunapata hela yetu ikapita tukaanza kufwattilia ndipo tukaja kukuta kampuni aijapeleka pesa za wafanyakazi mwaka mmoja na nusu,..hili lilitushtua ikabidi tuanze kukutana na kujipanga nini cha kufanya,tumejaribu kwenda kwa waziri wa miundo mbinu kulalamika kwa nini PPF haki ya mtu inazungushwa,..je ni haki pesa ya PPF kufanyia kazi zingine kwa maslahi ya kampuni,..chambo alijibu waziri yuko busy na hana muda wa kuonana na nyie ndipo tukaona hali sasa twende mbele ndipo umetuona hapa,...wiki jana tumeenda wakatuambia twende leo hivi naonge viongozi wako ndani atujui kinachoendelea mpaka sasa
ila ni masikitiko sana
nikikwambia ndugu mtu amefanya miaka 31 anapewa million 10 siku ya mwisho huku amemalizia ujana wake huu si uhaini kweli???
hawa watu nakwambia Mungu lazima awaadhibu....hakuna ambae alipenda kupokea zile cheki lakini tufanyeje,..ukienda kwa katibu mkuu anadiriki kusema mi nawaambia kama sio mimi kampuni ingekufa hii baraza la mawaziri wote limepitisha kuflisiwa hii kampuni mi na waziri tukamfwata waziri mkuu...kwa hiyo tunaamini wazir mkuu huyu huyu ndie mtetesi wetu

Nili jaribu kuonyeshwa huyo mama na wenzake waliofanya miaka zaidi ya 25 na kupewa hizo million 10 kwa kweli maombi ya hawa watu ipo siku tutasikia vitu vya ajabu ATCL...muda si mrefu.....

Swali langu najaribu kuuliza PPF wanacheza na maisha ya watu ama??
kuna sheria wameonyesha mwajiri akishindwa kulipa miezi miwili adhabu yake mitatu nini cha kufanya iweje wamekaa mwaka na nusu bila kulipa na wameachiwa kimya,...swali hili na mengineyo ntwaletea majibu kesho ntakapoamka na kulekea PPF kujua kulikon matatizo haya???

Tunaitaji kuanzisha chombo cha kutetea wafanyakazi,..hivi vyama vimekuwa vikinunuliwa kwa pesa ndogo sana na mwisho kuua utu wa watu,..mtu anadiriki kukubali kuondoa watu huku akipewa hata million 1 aifiki
tunaitaji kuwa na vyama vingine visivyofungamana na upande wowote,....kweli inaumiza ndio maana binafsi nilishaapa sitofanya kwa mwajiri zaidi ya miaka 6 ama saba kukimbia hii aibu,..huu ni uhaini...

tunawapa pole waliofikwa na matatizo tunawaombea mungu awajallie mlipwe mapema ni kweli hili kosa kama nchi za nje menejiment nzima inanukia maharage ya segerea kabla ya kwenda kujieleza.....lakini kwakuwa mko Bongo poleni sana haki ya mtu ni ngumu kupatikana bongo....
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
31
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 31 0
Safi sana ingawa sina hakika kama kwenda kwa Waziri Mkuu ni sahihi ama la.
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
Safi sana ingawa sina hakika kama kwenda kwa Waziri Mkuu ni sahihi ama la.

mkuu nilijaribu kuongea na jamaa wangu mmoja wa chama cha wafanyakazi akanieleza kuna procedure unafwata kukiwa na migongano moto unaelekeza kwa waziri mkuu hapa ni baada ya kukaa na menejiment husika amwelewani,waziri wa wizara husika/hakuna maelewano waziri mkuu akuna maelewano mahakama ya kazi/hakuna haki ujue nao ni binadamu hawa wanaitaji watoto wao waende ****** /maahakama ya rufaa ya kazi baada ya hapo matekelezo,..sasa kama wanashinda amna matekelezo wanaomba kukazwa ukumu hapo ndipo unawasikia wajomba zangu

MAJEMBE AUCTION MART ni nani

ila walahi kesho lazima nipate jawabu kwa nini hii kampuni wameachiwa mwaka mzima awajalipa PPF je pesa zinaingia mifukoni mwa wakubwa ama wanakula na viongozi wa PPF..tusiwasemee moyo
mvumilivu hula mbivu
ni napicha nilipga najaribu kuzituma inshalla zikiingia ,kwanza nimetuma msg kwa kiongozi wao kuomba ruhusa ya kuziweka akikataa sina jinsi
 

Forum statistics

Threads 1,236,244
Members 475,030
Posts 29,251,507