Elections 2010 Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete

Huyu Shigongo ni wa kumpuuza. Anajipendekeza kwa JK baada ya kushindwa katika kura za maoni akiwa na lengo la kutaka ateuliwe kwenye nafasi 10 za uteuzi za raisi. Lakini amebugi step kwa sababu sehemu kubwa ya wafanyakazi wamechoshwa na usanii wa Kik-wete na Kapu-ya wake and when it's all said and done, ni Dr Slaa ndiye ataibuka mshindi. Kwa hiyo Bw. Shigongo kama utapata huu ujumbe, nakushauri ungeanza kujigonga kwa Dr. Slaa pengine utapata moja ya hivyo viti 10 vya kuteuliwa.
 
Sasa nimeamini CCM inaharibu akili za watu.

Shigongo nilifikiri anauwezo wakufikiri kumbe sivyo.

Kaifanya Tz iwe ya kiudaku daku.

Nani wa kukiokoa CCM ?

Shigongo = Hiza Tambwe

Hiza T= Makamba

Wote ni wana CCM

Hivyo CCM HUHARIBU AKILI ZA WATU
 
:playball:HAO SI WAFANYAKAZZI BALI NI MAMLUKI WALIOPEWA PESA ILI KUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA, WAFANYAKAZI HAWAWEZI KUWA MAJUHA KIASI HICHO,TENA HAKO KABINTI KWENYE PICHA NAHISI KAMEHONGA RUSHWA YA NGO..... NDO KAKAPEWA KAZI LAZIMA KAMSIFIE ALIYEKAPA KAZI,PIA WAANDISHI WA HABARI WENGINE NI FORM FOUR,WANASUBIRI WAENDELEZWE LAZIMA WAJITOKEZE KUSIFIA,
 
Shigongo ameamua kutuletea picha gani hizi zinafaa kwenye magazeti yake si humu.
 
Bill karibu ningeanguka kiharusi nikifikiri ni wewe umeandika. Kumbe umeidaka kwa mnafiki mlokole Shigingo?? Wataleta kila kitu, wasubiri wapinzani waanze kampeni zao. Shigongo umelipwa ngapi na magazeti yako ya udaku? Njaa tu uzalendo huna!!
 
Jana mgaya alitoa tamko na kukana habari iliyoandikwa na TAnzania daima kuwa "TUCTa yamjibu Kikwete"

Kataika gazeti la leo Nipashe Mgaya amesema Jk amesikiliza kilio cha japo hajafikia lengo lao

Mgaya amesema hapo kawajali wafanyakazi kura watampa
Mgaya sasa amekuwa muelewa.aendelee hivyohivyo
 
s5kavs.jpg

Rais Jakaya Kikwete


Na Waandishi Wetu
Wakati Shirikisho la Vyama vya Wanyakazi nchini (TUCTA) likidaiwa linajipanga kutoa tamko la kuwataka wafanyakazi wote nchini kutompigia kura Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, inaonekana mambo ni kinyume.

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wanaeleza kufurahishwa na utawala wa JK, hivyo kuwa tayari kumuongezea kipindi kingine cha uongozi cha miaka mitano (2010-2015).

Wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili kwa wiki nzima iliyopita, Dar es Salaam, walieleza kufurahishwa na kazi ya JK aliyoifanya Ikulu kwa miaka mitano, hivyo wanaamini ataendeleza mazuri endapo ataongezewa kipindi kingine.

Walisema kuwa Rais Kikwete ameweza kuonesha moyo mzuri kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mara kwa mara pia kukabiliana na ufisadi, hivyo hawaoni sababu ya kuliunga mkono TUCTA endapo litasema JK asipigiwe kura.
Baadhi ya maoni ya wafanyakazi kama walivyozungumza ni kama ifuatavyo;

ITUS BILLA
Mfanyakazi wa Kampuni ya Big Bell.
Anasema: "Nafurahia kipindi chote cha Kikwete kuwepo madarakani, maana mengi aliyoahidi ametekeleza. Nawashauri Watanzania wenzangu tumuongezee kipindi kingine aweze kuleta maendeleo zaidi. Kuhusu nyongeza ya mshahara mimi naona maisha yatakuwa yale yale kwani kila mshahara ukitangazwa kupanda na bidhaa nazo zinapandishwa."


2z8utlu.jpg

Itus Billa

SULEIMAN MAZINGE
Anasema: "Utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni mzuri kwani nchi ina amani na hakuna njaa wala migogoro na hilo ndilo jambo kubwa, mambo mengine ni majaaliwa. Kuhusu ongezeko la mishahara hapo hakutakuwa na jipya kwani uzoefu unaonesha mishahara ikipanda na huduma nazo zinapanda."

devc3q.jpg

Suleman Mazinge

ANNA LUWENA
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri na anaomba uendelee ingawa hauna tofauti kubwa na tawala zingine zilizopita. Kuhusu kupanda kwa mishahara ni bora ingebaki palepale kwani ongezeko la mishahara litasababisha kuongezeka maradufu kwa gharama za huduma mbalimbali."

r938nc.jpg

Anna Luwena


HUSSEIN MAKUBI
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri kwani ameendeleza mazuri yaliyoachwa na marais waliopita. Kuhusu mishahara mwanzoni wananchi watafurahia ongezeko hilo lakini siku zinavyokwenda huduma nazo taratibu zitapanda na kufanya hali kuwa ile ile."

BABY OMARY
Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri hakuna dosari kubwa iliyojionesha ukilinganisha na tawala zilizopita.
Ongezeko la mishahara linatokana na kusonga kwa dunia lakini halina uhusiano wowote na ubora wa maisha kwani hapo zamani mfanyakazi alilipwa 6000/ (elfu sita) mfanyakazi huyo sasa hivi analipwa 600,000/ (laki sita) lakini maisha yake ni yaleyale afadhali ya zamani.

xek569.jpg

Baby Omary

HADIJA HASSAN
Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom anasema: "Utawala wa Rais JK ni mzuri na hasa kwa kuwa ametoa ajira kama alivyoahidi, hivyo kuwakomboa Watanzania. Ongezeko la mishahara anasema litakuwa na mafanikio kwa wenye malengo lakini wasio na malengo wataendelea kuumia."


GHONCHE MATEREGO
Katibu Mtendaji wa BASATA, anasema: "Rais Kikwete uongozi wake ni mzuri sana pia ni mtu anayeona mbele zaidi ndiyo maana anawapa vijana kipaumbele tena anapenda kuwarithisha ili baadaye wawe viongozi wanaofaa kuongoza nchi. Amekuwa ni mchango mkubwa sana kwa vijana, lakini hajawaacha wazee anawataka kuelimisha vijana wao ili waweze kujikwamua kimaisha.

"Kwa upande wa mshahara kuongezwa hilo nalo ni jambo la heri na serikali imetimiza ahadi yake kwani kilikuwa ni kilio cha siku nyingi na sasa imefikia mahali na kuongeza tunashukuru kwa kutimiza ahadi hiyo."

MBAZI OMBENI
Karani wa BASATA, anasema: "Utawala wa Rais Kikwete siyo mbaya sana lakini kuna ahadi ambazo naomba kama akichaguliwa tena awamu ya pili azitekeleze. Shule za Kata zimejengwa nyingi lakini vitendea bado tatizo, naomba aliangalie hilo pamoja na mfumuko wa bidhaa sokoni.

"Suala la mishahara kuongezwa nashuru kwa sababu kilikuwa kilio chetu cha siku nyingi."
zao ni kwa
SOURCE: Global Publishers aka. Shigongo
BABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one
 
BABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one

Bange hizi!
 
BABA yangu ni mkulima na mama yangu ni mfanyakazi wote wameseme watampa kura Kikwete.Mimi na nyumba yangu tutampa kura kikwete.Mgaya na wana TUKTA nao wamesema kura zao ni kwa Kikwete. CCM nambari one
Sishangai watakaompa kura kikwete maana wengi ni wale waliokosa elimu hivyo wakazibwa milango yao yote ya FAHAMU
 
Bill, unamtumikia nani na umelipwa bei gani?
How come majibu yote yafanane hivyo, i smell a rotten kitten here!.
Watu wanajitolea tu,pole wewe unaelipwa kazi unayo siku usipofanyakazi mwajili atakunyima malipo.sijui kama anakulipa KCC cha TUKTA au la.
 
Bill karibu ningeanguka kiharusi nikifikiri ni wewe umeandika. Kumbe umeidaka kwa mnafiki mlokole Shigingo?? Wataleta kila kitu, wasubiri wapinzani waanze kampeni zao. Shigongo umelipwa ngapi na magazeti yako ya udaku? Njaa tu uzalendo huna!!
Angalia usivunje mkono.Ya nini kupata kiharusi ungali mdogo.Kubali yaishe
 
Haya tena, Shigongo baada ya kugaragazwa kwenye maoni ya CCM anaanza kuleta porojo hapa.

Hivi shigongo unadhani wafanyakazi hamnazo sana ...... unaweza kuwanunua kwa udaku wako????

BMW ntamsifu kwa asilimia 120% lakini kwa JKII imekula kwako. siamini kwasasa tunakula mlo mmoja kwa siku. kwani kukua kwa uchumi ni kupanda gharama ya vyakula? the major human basic need ni kula. sasa kama tathmini inafanyika kwa wafanyakazi na watoto wa ushuani hiyo ni tathmini au ni mtazamo?watu acheni ushabik wakijinga. twende ngaz kwa ngaz. anzia gerezani hadi maofisini. nyumbani hadi kwenye matafrija TOA THATHMINI kwa kulinganisha na kiongozi aliyepita.

KIONGOZI BWM Vs JK
MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo 250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500, hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni 120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila waalimu na wenzao.........! 3 years.

Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona hili wameamua kujicholea MIPAKA yao Mapema.

MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA NA KODI ZENU.
Wewe ndiye uliyefumba macho ndiyo maana huoni kama wenzako wamefumba au wamefumbua.Fumbua basi au tumia white stick if any.
 
Jana mgaya alitoa tamko na kukana habari iliyoandikwa na TAnzania daima kuwa "TUCTa yamjibu Kikwete"

Kataika gazeti la leo Nipashe Mgaya amesema Jk amesikiliza kilio cha japo hajafikia lengo lao

Mgaya amesema hapo kawajali wafanyakazi kura watampa
Mgaya juuu.Kura za wafanyakazi kwaaaaa Kikwete.TUCTA safiiii
 
Back
Top Bottom