Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bill, Aug 20, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete


  Na Waandishi Wetu
  Wakati Shirikisho la Vyama vya Wanyakazi nchini (TUCTA) likidaiwa linajipanga kutoa tamko la kuwataka wafanyakazi wote nchini kutompigia kura Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, inaonekana mambo ni kinyume.

  Sehemu kubwa ya wafanyakazi wanaeleza kufurahishwa na utawala wa JK, hivyo kuwa tayari kumuongezea kipindi kingine cha uongozi cha miaka mitano (2010-2015).

  Wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili kwa wiki nzima iliyopita, Dar es Salaam, walieleza kufurahishwa na kazi ya JK aliyoifanya Ikulu kwa miaka mitano, hivyo wanaamini ataendeleza mazuri endapo ataongezewa kipindi kingine.

  Walisema kuwa Rais Kikwete ameweza kuonesha moyo mzuri kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mara kwa mara pia kukabiliana na ufisadi, hivyo hawaoni sababu ya kuliunga mkono TUCTA endapo litasema JK asipigiwe kura.
  Baadhi ya maoni ya wafanyakazi kama walivyozungumza ni kama ifuatavyo;

  ITUS BILLA
  Mfanyakazi wa Kampuni ya Big Bell.
  Anasema: "Nafurahia kipindi chote cha Kikwete kuwepo madarakani, maana mengi aliyoahidi ametekeleza. Nawashauri Watanzania wenzangu tumuongezee kipindi kingine aweze kuleta maendeleo zaidi. Kuhusu nyongeza ya mshahara mimi naona maisha yatakuwa yale yale kwani kila mshahara ukitangazwa kupanda na bidhaa nazo zinapandishwa."


  [​IMG]
  Itus Billa

  SULEIMAN MAZINGE
  Anasema: "Utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni mzuri kwani nchi ina amani na hakuna njaa wala migogoro na hilo ndilo jambo kubwa, mambo mengine ni majaaliwa. Kuhusu ongezeko la mishahara hapo hakutakuwa na jipya kwani uzoefu unaonesha mishahara ikipanda na huduma nazo zinapanda."

  [​IMG]
  Suleman Mazinge

  ANNA LUWENA
  Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri na anaomba uendelee ingawa hauna tofauti kubwa na tawala zingine zilizopita. Kuhusu kupanda kwa mishahara ni bora ingebaki palepale kwani ongezeko la mishahara litasababisha kuongezeka maradufu kwa gharama za huduma mbalimbali."

  [​IMG]
  Anna Luwena


  HUSSEIN MAKUBI
  Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri kwani ameendeleza mazuri yaliyoachwa na marais waliopita. Kuhusu mishahara mwanzoni wananchi watafurahia ongezeko hilo lakini siku zinavyokwenda huduma nazo taratibu zitapanda na kufanya hali kuwa ile ile."

  BABY OMARY
  Anasema: "Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri hakuna dosari kubwa iliyojionesha ukilinganisha na tawala zilizopita.
  Ongezeko la mishahara linatokana na kusonga kwa dunia lakini halina uhusiano wowote na ubora wa maisha kwani hapo zamani mfanyakazi alilipwa 6000/ (elfu sita) mfanyakazi huyo sasa hivi analipwa 600,000/ (laki sita) lakini maisha yake ni yaleyale afadhali ya zamani.

  [​IMG]
  Baby Omary

  HADIJA HASSAN
  Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom anasema: "Utawala wa Rais JK ni mzuri na hasa kwa kuwa ametoa ajira kama alivyoahidi, hivyo kuwakomboa Watanzania. Ongezeko la mishahara anasema litakuwa na mafanikio kwa wenye malengo lakini wasio na malengo wataendelea kuumia."


  GHONCHE MATEREGO
  Katibu Mtendaji wa BASATA, anasema: "Rais Kikwete uongozi wake ni mzuri sana pia ni mtu anayeona mbele zaidi ndiyo maana anawapa vijana kipaumbele tena anapenda kuwarithisha ili baadaye wawe viongozi wanaofaa kuongoza nchi. Amekuwa ni mchango mkubwa sana kwa vijana, lakini hajawaacha wazee anawataka kuelimisha vijana wao ili waweze kujikwamua kimaisha.

  "Kwa upande wa mshahara kuongezwa hilo nalo ni jambo la heri na serikali imetimiza ahadi yake kwani kilikuwa ni kilio cha siku nyingi na sasa imefikia mahali na kuongeza tunashukuru kwa kutimiza ahadi hiyo."

  MBAZI OMBENI
  Karani wa BASATA, anasema: "Utawala wa Rais Kikwete siyo mbaya sana lakini kuna ahadi ambazo naomba kama akichaguliwa tena awamu ya pili azitekeleze. Shule za Kata zimejengwa nyingi lakini vitendea bado tatizo, naomba aliangalie hilo pamoja na mfumuko wa bidhaa sokoni.

  "Suala la mishahara kuongezwa nashuru kwa sababu kilikuwa kilio chetu cha siku nyingi."

  SOURCE: Global Publishers aka. Shigongo
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bill, unamtumikia nani na umelipwa bei gani?
  How come majibu yote yafanane hivyo, i smell a rotten kitten here!.
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Haya tena, Shigongo baada ya kugaragazwa kwenye maoni ya CCM anaanza kuleta porojo hapa.

  Hivi shigongo unadhani wafanyakazi hamnazo sana ...... unaweza kuwanunua kwa udaku wako????

  BMW ntamsifu kwa asilimia 120% lakini kwa JKII imekula kwako. siamini kwasasa tunakula mlo mmoja kwa siku. kwani kukua kwa uchumi ni kupanda gharama ya vyakula? the major human basic need ni kula. sasa kama tathmini inafanyika kwa wafanyakazi na watoto wa ushuani hiyo ni tathmini au ni mtazamo?watu acheni ushabik wakijinga. twende ngaz kwa ngaz. anzia gerezani hadi maofisini. nyumbani hadi kwenye matafrija TOA THATHMINI kwa kulinganisha na kiongozi aliyepita.

  KIONGOZI BWM Vs JK
  MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

  Unga 460 Vs 1000 = 217%
  Mchele 600 Vs 1200 = 200%
  Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
  Mkate 250 Vs 700 = 280%
  Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
  Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
  Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
  Nazi 100 Vs 550 = 550%
  Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

  unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo 250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500, hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni 120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila waalimu na wenzao.........! 3 years.

  Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

  Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

  Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

  Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

  FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona hili wameamua kujicholea MIPAKA yao Mapema.

  MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA NA KODI ZENU.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dawa ya mpuuzi ni kupuuzwa (Malaria Sugu, 2010)
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,312
  Trophy Points: 280
  rehula_nyaulawa.jpg
  TANGAZO HILI LIMELETWA KWENU KWA HISANI YA Uday Saddam Hussein al-Tikriti wa Msoga-Chalinze

   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nimewasilisha tu kutoka Buchosa - Global Publishers. Subirini mtaiona hiyo kwenye Gazeti la udaku la IJUMAA
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama bado hizi ndizo kampeni za chama kilichotawala kwa muda wa karibia miaka 50, to hell! Really we need change..
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  kama wafanyakazi wameamua hivyo.....nami sinabudi kuwaunga mkono
   
 9. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev naona wapuuzi wanazidi kuongezeka, hizo Bilion 50 zimeanza kazi, na hivi Bongo - Bongo zimelala
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  TANGAZO HILI LIMELETWA KWENU KWA HISANI YA Uday Saddam Hussein al-Tikriti wa Msoga-Chalinze

  Vigezo na Masharti kuzingatiwa!
   
 11. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .....????? aaargggg!
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Eric Shigongo kagombea ubunge amekosa, na JK alisema waliokosa ubunge atawapa ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa. Sasa ulifikiri Eric anaweza kuandika nini zaidi ya huo upupu ili JK ampe japo wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake na watoto?
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,913
  Likes Received: 12,067
  Trophy Points: 280
  kweli serikali imeumia hadi inatia huruma na wapiga debe nao hovyo hovyo anafikiri kuandika maneno mengi na kupamba picha itasaidia wajipange upya hatudanganyiki.
   
 14. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,172
  Trophy Points: 280
  Mimi hii habari inatia kichefuchefu sitaki hata kuisoma na hao waliohojiwa nao loh!! kweli maisha bora kwa kila mtanzania aliyehojiwa na kujibu upupu huu
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa Wilaya ya Buchosha akiwa kazini!
   
 16. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Rev lakini ni vizuri kumjibu mpumbavu sawa na upumbavu wake asije akajiona anahekima mbele za watu. As what you are doing to MS.
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Thanks God ni udaku!
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,913
  Likes Received: 12,067
  Trophy Points: 280
  kumbe ni gazeti la udaku nilikuwa nafikiri gazeti real.
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Shigongo si ndiye yule mtunga thamthria??? Kwa hiyo sasa ameamua kutunga hadithi na kuziweka kwenye magazeti badala ya vitabu!!!!!
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  duh inasikitisha mtanzania anaposema bora mshahara usipande maana ukipanda na bei za bidhaa zinapanda maradufu.duh
  Kwa kweli hilo tangazo la CCM halina tija kabisa,kwanza nani aliyesema asilimia 100 ya wafanyakazi hawatampigia kura mkwere .Hapa tunaongelea wengi wao.
   
Loading...