Wafanyakazi TRL wakubali kurejea kazin

ishuguy

Member
Nov 3, 2007
76
10
Hatimaye, wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Nchini (TRL), jana walirejea kazini baada ya kusitisha mgomo wao kufuatia amri ya serikali iliyowataka kuendelea na kazi.
Wafanyakazi hao waligoma wiki hii kushinikiza uongozi wao kuwalipa mshahara wa mwezi uliopita.
Akizungumza na wafanyakazi hao, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Sylivester Rwegasira, alisema jana jioni wataingia kazini kama kawaida.
Aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili wapate fedha haraka kwa ajili ya kujilipa mishahara yao.
Aliongeza kuwa uamuzi wa kurejea kazini umekuja kutokana na kuwaonea huruma wasafiri waliokuwa wanasafiri kwa kutumia reli ya kati inayotoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Rwegasira alisema licha ya kuwa wamesitisha mgomo wao, lakini madai yao bado yako pale pale.
Kwa upande wa serikali ambayo ina hisa asilimia 49 katika kampuni hiyo, ilisema haiwezi kuchukua jukumu la kuwalipa wafanyakazi hao kwa siyo kuwa watumishi wake. Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam.
Kuhusu mgomo wa wafanyakazi hao, Waziri Kawambwa alisema serikali haiutambui na kuwataka warejee kazini haraka kwa kuwa ni batili.
CHANZO: NIPASHE


Hawa TRL wanahitaji solution ya kudumu, kila kukicha mgomo.
inaoneka hii migomo inamalizwa kwa nguvu bila kushugulikia, endeleeni kugoma ndugu zangu mpaka Management itakapobadili tabia yao,
 
Back
Top Bottom