Wafanyakazi Tazara waanza mgomo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,636
2,000
Wafanyakazi Tazara waanza mgomo Tuesday, 14 December 2010 20:57

Jackson Odoyo

ZAIDI ya wafanyakazi 1,000 wa Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Taraza), wameanza mgomo usiokuwa na kikomo kwa lengo la kumshinikiza meneja mwajiri wa shirika hilo, ajiuzuru.

Mgomo wa wafanyakazi hapo umeanza jana wakati abiria wanaotumia usafiri wa treni ya Tazara wakitarajia kusafiri kwa treni ya shirika hilo.

Mgomo wa wafanyakazi jana ulisababisha abiria zaidi ya 322 kushindwa kusafari na baadhi yao walilazimika kushinda katika ofisi za shirika hilo bila kufahamu cha kufanya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Tazara, Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Slvester Rwegasira alisema mgomo huo, uitaendelea mpaka Meneja Mwajiri wa Shirika hilo atakapo achia ngazi.

"Lengo la mgomo wetu ni kushinikiza serikali pamoja na ungozi wa shirika hilo, kumuondoa meneja huyo kwa sababu ni chanzo cha matatizo ya wafanya wa Tazara,"alisema Rwegasira.

Akitaja baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na Meneja huyo, Daison Mlenga ambaye ni raia wa Zambia alisema amawabagua wafanyakazi wanaotoka Tanzania katika shirika hilo.

"Huyu jamaa anabagua wafanyakazi,hatendi haki hata kidogo na ndiyo sababu hatumtaki, hivyo tunataka aondoke ili aletwe mtu mwingine atakayeweza kutenda haki,"alifafanua Rwegasira.


Alisema hawataki Mtanzania awekwe katika nafasi hiyo na kwamba lengo lao ni kumpta mtu mwingine ambaye atawatendea haki bila nchi yoyote anayotoka kati ya Zambia na Tanzania. Mwananchi lilipomtafuta Meneja Mwajiri,Mlenga lilielezwa alikuwa kwenye kikao kujadili mgomo wa wafanyakazi hao.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,636
2,000
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Tazara, Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Slvester Rwegasira alisema mgomo huo, uitaendelea mpaka Meneja Mwajiri wa Shirika hilo atakapo achia ngazi.

"Lengo la mgomo wetu ni kushinikiza serikali pamoja na ungozi wa shirika hilo, kumuondoa meneja huyo kwa sababu ni chanzo cha matatizo ya wafanya wa Tazara,"alisema Rwegasira.
Hivi lile Agizo la Raisi la mwaka 1970 la kuwashirikisha wafanyakazi kwenye uongozi wa taasisi za umma liliishia wapi......................kama wafanyakazi hawa wangelikuwa wanashirikishwa ungekuta huu ubabe wa viongozi bomu ungelikuwa haupo.....................Bodi ya TAZARA hubambikiziwa viongozi ambao haina ubavu wa kuwadhibiti na mabosi hao hufanya kazi zao bila ya kuzijali bodi hizo na matokeo yake ni vurugu kila siku....................Hakuna uwajibikaji hata chembe..............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom