Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,392
- 23,558
Mwananchi
Date::7/1/2008
SAKATA la Mbunge wa Buchosa, Samwel Mchele Chitalilo, kuwaita wapiga kura wake waliotoa maoni yao na kumtaka anyamaze kuwa ni wahuni, limeingia hatua mpya baada ya Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) Kanda ya Ziwa, kumtaka awaheshimu wapiga kura.
Akizungumza jana na gazeti hili, katibu wa Raawu Kanda ya Ziwa ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Mwendwa, alisema wao kama wafanyakazi wamesikitishwa na kauli ya mbunge huyo kuwaita wapiga kura wake wahuni kwa kitendo cha kutoa maoni yao.
Alisema kauli aliyoitoa Chitalilo bungeni kutetea ufisadi inatia mashaka na wao wanaona jinsi baadhi ya wabunge wao wasivyo wazalendo kwa nchi yao.
Mwendwa alisema kauli kama za Chitalilo na wabunge wengine zinazotoka bungeni ni hatari kwa vile zitaifikisha nchi hii pabaya siku wananchi watakapoamua kutafuta haki yao kwa vita ama njia nyingine baada ya kuchoshwa na ufisadi ambao umeonekana kukumbatiwa na serikali na baadhi ya wabunge.
''Mbunge amefikia hatua ya kuwaita wapiga kura wake wahuni, hii ni hatari, lakini siku nchi hii ikiamka kutoka katika ujinga na wananchi wakaamua kuitafuta haki yao, vita itaibuka hapa nchini nadhani wabunge wanaweza kujifunza kwa mfano wa Kenya,'' alieleza Mwendwa.
Alisema kukomaa kwa kiburi kwa wabunge wengi dhidi ya wananchi wao ambao ndiyo wapiga kura wao kunatokana na wabunge wengi kuingia bungeni kwa fedha na kuwaonya wabunge
akitumia mfano wa CHitalilo kuwa wanapaswa kuwaheshimu wapiga kura wao kwa vile ndiyo mabosi wao.
''Haya ni matokeo ya wabunge kushinda kwa fedha, dawa yao ni wapiga kura, wakulima kwa wafanyakazi kuwaondoa wabunge kama hawa. Wanajivuna kwa fedha ambazo zimewaingiza madarakani na matokeo yake wamekuwa vinara wa kusimamia ufisadi bungeni na kuutetea badala ya matatizo ya wananchi,'' alisema Mwendwa.
Hata hivyo, katibu huyo amesemaa lawama za wafanyakazi zinaelekezwa kwa serikali kwa vile alidai kuwa ndiyo imeshindwa kuonyesha dhamira ya kweli kwa kupambana na
Ufisadi, hatua ambayo imesababisha serikali kushindwa kutoa ufafanuzi wa suala zima la ufisadi bungeni.