Wafanyakazi Sahara Media Group wamuandikia Rais Magufuli barua ya wazi

Jarateng

Senior Member
May 4, 2012
102
43
UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA SAHARA MEDIA GROUP (STARTV) MWANZA
MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
DARES SALAAM
TANZANIA
YAH: MHESHIMIWA RAIS TUSAIDIE ANTHONY DIALLO ATULIPE MAFAO NA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA YETU

Tafadhali husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu

Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, sisi wanahabari tuliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya SAHARA MEDIA GROUP Mwanza, ambayo pia ni mali ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Ndg,Anthony Diallo, tunaomba utusaidie ili serikali yako Tukufu, serikali inayosaidia watu wanyonge itusaidie kupata malipo yetu ya mafao na malimbikizo ya mishahara ambayo tumekuwa tukihangaika kudai kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Mheshimiwa Rais, tumeshajaribu kila namna pasipo ahueni ya kupata stahiki zetu. Tulianza kwa kukaa na mwajiri wetu na kutafuta suluhisho bila mafanikio. Hatua ya pili alitufukuza kazi kwa kusitisha mikataba yetu bila kutulipa, kwa taratibu za kisheria hapa kunaukiukwaji mkubwa maana tumefukuzwa bila malipo ni takribani mika miwili sasa.

Mheshimiwa Rais, hatua nyingine ilikuwa sisi kufungua kesi mahakama ya usuluhishi Commission for Mediation and Arbitration (CMA) ambayo kwa jitihada zake ilichukua zaidi ya miezi sita bila muafaka. Mwajiri wetu SAHARA amekuwa hatokei mahakamani na kila anapotokea amekuwa na sababu zisizo na mashiko na kutoa ahadi za uongo ambazo ulipelekea mahakama ya usuluhishi CMA Mwanza kufunga jalada na kutoa hukumu iliyoipeleka kesi yetu ya madai mahakama kuu Mwanza.

Mheshimiwa Rais, huku nako kesi imekamilika lakini hakuna tofauti na kule CMA maana ni mwaka unaenda sasa malipo hayaridhishi na mwajiri ni mbabaishaji.

Mheshimiwa Rais, tumeshafanya mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Mwanza akaahidi kutusaidia, tumeshaonana na OCS Kirumba wilayani Ilemela, OCD na hata kufanya maadamano ya amani katika ziara ya Katibu wa CCM Taifa Mh, Bashiru Ally, pamoja na haya yote Mheshimiwa Rais hatujaona mafanikio yoyote wala jitihada kutoka kwa kiongozi yoyote mwenye dhamana kutaka kuonesha nia ya kutusaidia kwa kuingilia kati suala hili.

Mheshimiwa Rais hayo ni madai tu ambayo yako mahakamani kwa sasa na kesi imekwisha ila utekelezaji wake ni dhaifu. Bado tuna madai mengine Mheshimiwa Rais ambayo ni tofauti na yale ya mahakamani nayo hayaridhi ulipaji wake.

Mheshimiwa Rais haiingii akilini mtu anadai mamilioni ya pesa alafu analipwa laki moja kwa madai kampuni haina pesa, wakati mwingine wanasema akaunti zimefungwa na TRA au pesa ilikuwepo ila tumelipia bili ya maji, umeme na satellite, kwa uhalisia haya hayamhusu mwajiriwa na huo ni wajibu wake anachotakiwa ni kulipa stahiki zetu ili nasi tuweze kujiendeleza hata kwa kuanzisha viwanda vidogo na kujiajiri.

Mheshimiwa Rais, mwezi wa nne mwaka jana wa 2018, mmiliki wa SAHARA MEDIA Anthony Diallo alituita kwenye kikao ofisini kwake Balewa jijini Mwanza, lengo kuu la kikao hicho ilikuwa kuwataka wafanyakazi ambao hawakuwa wamefungua kesi mahakamani, wasitishe mchakato huo kwasababu alikuwa akitarajia kupata fedha za mkopo kutoka nje ya nchi hivyo angetulipa punde baada ya kuzipokea.

Mheshimiwa Rais, Diallo amekuwa akitoa maneno ya maudhi kwa kusema hata walio mahakamani wanajisumbua maana mfumo wake wa malipo ni wa kusuasua na analipa pale tu anapokuwa na fedha hivyo hata kufungua kesi ni kupoteza muda.

Mheshimiwa Rais, tumeshajaribu kutafuta suluhu kwa vikao zaidi ya ishirini na mwajiri kupitia meneja utawala wake Ndugu Raphael Shillatu bila mafanikio. Katika kikao cha mwisho tuliambulia kulipwa Tsh 100,000 fedha ambayo haina msaada kwa lolote ukizingatia familia zinahitaji lishe bora, kuna madeni yanatuandama, watoto wanahitaji ada na nguo mpya za shule pamoja na vifaa vingine muhimu kwaajili ya kutengeneza mazingira mazuri ya elimu bora kwa maisha yao ya baadae.

Mheshimiwa Rais, kuna viongozi ndani ya kampuni ya SAHARA, mmoja wao anaitwa Nathan Rwehabura, huyu bwana hana kauli nzuri hata kidogo, amediriki kutoa maneno mabaya katika kikao cha mwisho mwezi January 2019, alituambia kuwa “anachokifanya Diallo ni kubuy time hivyo pamoja na maandamano na kubeba mabango yenu Mheshimiwa Rais hawezi kuwasaidia kwa chochote, kwasababu Diallo ni untouchable”.

Mheshimiwa Rais, katika suala la mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kuna shida kubwa sana. Tulio wengi tumejiunga na mifuko hiyo lakini kwa zaidi ya miaka sita katika kampuni hakuna hata senti iliyowekwa katika akaunti za uanachama, matokeo yake tumeshindwa kupata stahiki zetu kama huduma za Bima ya afya, fao la kukosa ajira na stahiki nyingine zitokanazo na michango ya uanachama kwakuwa akaunti hazina michango.

Mheshimiwa Rais, wanahabari ni moja ya nguzo muhimu sana kwa Taifa katika kufichua mambo, kutoa na sambaza taarifa zenye kuonesha yaliyo mema, na kwa namna moja tumefanya kazi hiyo kwa kuwajali wengi hata wale waliokuwa na matatizo kama yetu, lakini ni aibu kama sisi tuliosaidia wenzetu leo tumetengwa na kuonekana hatufai.

Mheshimiwa Rais tunaamini serikali yako tukufu ya awamu ya tano ni serikali ya watu wanyonge, serikali yenye kujali wasiojiweza, wenyeuhitaji, nasi tunaamini fika kwa barua hii Mheshimiwa Rais kilio chetu kimefika na utakuwa tayari kutusaidia.

Tunatanguliza shukrani zetu tukiamini umekubali na unania ya kutusaidia wanyonge, ni sisi wanahabari tuliokuwa wafanyakazi wa SAHARA MEDIA GROUP jijini Mwanza.

Asante Mheshimiwa Rais kwa kuisoma barua yetu.

Mungu akubariki, Mungu ibariki Tanzania.
 

Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    73.4 KB · Views: 46
  • 1.jpg
    1.jpg
    33.8 KB · Views: 47
  • 2.jpg
    2.jpg
    29.7 KB · Views: 48
  • 4.jpg
    4.jpg
    30.3 KB · Views: 50
Nadhani ni bora walipwe chao watambae .
Unafikiri kama sio serikali angalau kuibana Azam na ITV kuna mtu anaijua hiyo kampuni yenu ambayo ni tawi la CCM.
Waiombe CCM iinunue hiyo SAHARA Media.
Hamna namna muone kwa macho mana mnasifia tu hata wenzenu wakilalamikia stahiki zao hamtangazi ,wenzenu wakisema makampuni yanapata hasara hamtangazi ,sasa muone kwa macho yenu wenyewe.
 
Hapo kukamata mali ndo pazuri lakini inaonekana waliopewa hayo mamlaka ikiwa ni pamoja na shirika la hifadhi ya jamii la taifa (NSSF) wameshindwa kuifanya kazi yao ipasavyo pamoja na Mahakama kuna mahali wanalega kwahyo wanatakiwa kushughulikiwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom