Wafanyakazi ofisi ya Bunge: Makinda ana ubaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi ofisi ya Bunge: Makinda ana ubaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 23, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  BAADHI ya wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wametoa tuhuma nzito kwa baadhi ya viongozi wao wa juu kutokana na kile wanachokiita ni kubaguliwa kwa kuitwa ni watu wa kundi la Spika mstaafu Samuel Sitta.

  Wakizungumza Dares Salaam jana kwa sharti la kutotajwa, watumishi hao ambao ni waathirika wa ubaguzi huo, walisema kitendo hicho ni ubaguzi unaodhoofisha ufanisi uliokuwa umefikiwa na uongozi wa Bunge uliopita.

  Kwa mujibu wa watumishi hao, hatua hiyo imekuwa ikitokana na hofu ya kufichuka maovu na udhaifu wa utendaji na kuvuja kwa jamii ndiyo maana, kuna watu wanaitwa, "hawa wa Sitta."

  Mmoja wa wafanyakazi hao alifafanua zaidi kwamba, hata Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah, ingawa ni mteule wa rais, lakini naye amekuwa akibaguliwa akiitwa mtu wa Sitta na kuna kipindi alifikia hatua ya kutaka kujiuzulu.
  Lakini, Dk Kashilila ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge, alipoulizwa kwa simu jana, alisema: "Acha nifanye uchunguzi kuona kama kuna kitu hicho."

  Dk Kashillilah alisema jambo kama hilo anapaswa kuwasiliana na idara mbalimbali za Bunge na kusisitiza: "Nikianza kuzungumza bila kushirikisha wenzangu ambao labda wanajua vyema sitakutendea haki wewe na mimi pia."

  Aliongeza kuwa hadi sasa yeye hajapata malalamiko hayo mezani kwake na kwamba, labda yatakuwa pembeni.
  Alisema hadi sasa hakuna ajira mpya ambazo Bunge limefanya na kusisitiza, kama wapo miongoni mwa waliopo wanabaguliwa kwa msingi huo, atajaribu kulifuatilia na wenzake kuona ukweli wake.

  Alipoulizwa kwamba yeye ni mmoja waathirika hao wanaoitwa 'watu wa Sitta na alikuwa akitaka kuachia ngazi kutokana na majungu hayo,' alicheka kisha akasema: "Hilo mimi silijui."

  Mtendaji mkuu huyo wa bunge alisema wafanyakazi hao waliendelea kuhoji aina hiyo ya uongozi wa kubagua watu wakati spika aliyepita alimrithi hadi katibu wa bunge.Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, kutokana na kuajiriwa baadhi ya watu wakiwamo madereva wasiokuwa na sifa, kumesababisha hata gari aina ya Mercedes Benz iliyokuwa ya Spika kupata ajali, baada ya dereva wake kugonga gari kwa nyuma.

  Walidai kuwa baadhi yao wamekuwa wakifika ofisini bila kupangiwa kazi, hali ambayo inawaathiri kisaikolojia.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama ndivyo, ni hatari sana hii!
  Moja ya dalili za ulegevu wa uongozi ofisini ni kuzalisha makundi!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi hawa watu wataendelea kuiyumbisha nchi mpaka lini?
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Yule mama makinda uwezo mdogo anafikiri watanzania wa leo ni sawa na wa enzi za ujana wake.Atakoma siri zake zote zitakuwa nje nje mpaka atajuta.Labda asifanye ufisadi ndani ya ofisi yake
   
Loading...