Wafanyakazi nane wa BoT kortini Dar kwa kughusi vyeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi nane wa BoT kortini Dar kwa kughusi vyeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 19, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,369
  Likes Received: 34,094
  Trophy Points: 280
  Date::9/19/2008
  Wafanyakazi nane wa BoT kortini Dar kwa kughusi vyeti

  [​IMG]
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki Kuu (BoT) wakificha nyuso zao baada ya kufikishwa mahakamani Dar es Salaam, Ijumaa wakikabiliwa na makosa ya kughushi vyeti vya shule.

  Ramadhan Semtawa na Nora Damiani
  Mwananchi

  TUHUMA za kuwepo kwa upendeleo wa watoto wa vigogo kwenye ajira za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zimesimamisha kizimbani wafanyakazi wanane ambao wameshtakiwa kwa kosa la kughushi vyeti.

  Tuhuma dhidi ya watoto 16 wa vigogo ziliibuka wakati kashfa ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ikiwa imeshamiri kiasi cha kusababisha aliyekuwa gavana, Daud Ballali kusitishwa mkataba wake na kufanyika kwa mabadiliko kadhaa kwenye uongozi wa chombo hicho nyeti cha fedha.

  Na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, aliahidi kuzishughulikia tuhuma hizo wakati huo baada ya tuhuma hizo kushikiwa bango.

  Jana, wafanyakazi wanane wa BoT, baadhi yao wakiwa wamejifunika nyuso kwa nguo na nywele za bandia, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakishtakiwa kwa tuhuma za kughushi vyeti na kutoa hati za uongo.

  Wafanyakazi hao, wengi wao wakiwa wanawake, ni Justina J Mungai, ambaye imeelezwa kuwa ni mtoto wa Joseph Mungai, ambaye amewahi kushika wizara tofauti ikiwemo ya elimu, Christina G Ntemi, Siamini Eddie Kombakono, Janeth John Mahenge, Beatha Constantine Massawe, Jacquiline David Juma, Philimina Philibert Mutagurwa na Amina Mohamed Mwinchumu.

  Wafanyakazi hao walifikishwa katika mahakama hiyo saa 4.00 asubuhi na kusomewa shtaka mbele ya Hakimu Neema Chusi. Wakili wa serikali, Edgar Luoga, akisaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Abubakar Msangi, ndio walioongoza mashtaka hayo.

  Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa mwajiri wao, ambaye ni BoT.

  Washtakiwa Mungai, Massawe na Mwinchumu, wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2001, wakati Ntemi, Kombakono, Mahenge na Mutagurwa wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2002.
  Wanadaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa BoT hati za uongo, wakionyesha kuwa vimetolewa na Baraza la Mitihani la Taifa, wakati si kweli.


  Ilidaiwa kuwa, Mutagurwa alighushi cheti hicho mwaka 2000.

  Washtakiwa wote walikana kufanya makosa hayo na upande wa serikali ulisema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

  Hakimu Chusi alitoa masharti ya dhamana na kila mshtakiwa alitakiwa awe na wadhamini wawili, ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini dhamana ya Sh5milioni. Pia wadhamini hao walitakiwa wawe na barua za waajiri wao na kwamba, hawatakiwi kusafiri nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali maalumu cha mahakama.

  Mshtakiwa wa saba Mutagurwa, alitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa nje kwa dhamana, wakati washtakiwa wengine walirudishwa rumande hadi Oktoba 6 watakaposimamishwa tena kizimbani.

  Habari zilizopatikana nje ya mahakama na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wa serikali, zilisema kuwa, washtakiwa hao wote wanafanya kazi ya kuhesabu fedha BoT.

  Wakati tayari baadhi ya watoto wa vigogo wakiwa wamefikishwa mahakamani, Gavana wa BoT, Prof Ndulu alisema, benki hiyo itahakikisha wote walioghushi vyeti wanachukuliwa hatua za kiutawala.

  Hatua ya BoT kuhakiki majina ya watoto wa vigogo na watumishi wote, kwa mara ya kwanza iliripotiwa na gazeti hili Mei 29 baada ya kuzungumza na Gavana Ndulu.

  Akifafanua operesheni hiyo, Profesa Ndulu alisema, kazi kubwa ya BoT katika mchakato huo ni kuchukua hatua za kinidhamu na za kiutawala huku zile za kinidhamu zikichukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  Gavana Profesa Ndulu alifafanua kwamba, kwa sasa BoT iko katika hatua za mwisho za kukamilisha zoezi zima la uhakiki wa watumishi wake wote ambao wametajwa katika kipindi husika.

  "Operesheni itaendelea. Sisi tunafanya kazi yetu na kuchukua hatua za kinidhamu, lakini wenzetu Takukuru wanafanya kwa upande wa jinai," alisema Profesa Ndulu.

  Akifafanua sehemu ya hatua iliyofikiwa, Profesa Ndulu alisema, baadhi ya wafanyakazi wanaoghushi wameshachunguzwa na benki na kuonekana kuwa wameongeza sifa zao.

  "Utakuta kipindi kile mtu alikuwa na sifa fulani, lakini watu wamesoma na baadhi hata kufikia katika viwango husika vya elimu. Lakini bado mchakato unaendelea vizuri na uko katika hatua za mwisho, sisi kila taarifa tunayopata tunawapa Takukuru," alisisitiza.

  Miongoni mwa watoto ambao majina yao yanatajwa ni pamoja na watoto wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na gavana wa zamani, marehemu Daud Ballali.

  Ajira za watoto hao zinahusishwa na ushawishi wa nafasi za baba zao, wakati wakiwa madarakani.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  mbona,this sounds fishy,yaani vyeti vyenyewe ni vya form four,yaani hata mtoto wa mungai forged a certificate,does it mean she is only a primary school leaver or what? mbona things dont add up!!!!!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,202
  Likes Received: 1,969
  Trophy Points: 280
  Gwiji... sio lazima unapo-forge cheti cha f4 uwe umemaliza darasa la saba... unaweza ukawa na grades mbofu mbofu na ukataka kuzi-up grade!!!!!!
   
 4. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hi hivi.

  Hapa kuna viini macho. Ishu inatakiwa iwe mtoto wa kigogo mwenye cheti halali cha Form VI au hata stashahada halali ya chuo fulani cha biashara ametumia jina lake kupata kazi inayohitaji shadaha ya chuo kikuu, au qualifications nyingine za juu zaidi. That is the issue.

  Hao hapo sio watoto wa vigogo. Hawa wamepata kazi bila kutumia influence ya baba zao, bali vyeti feki. Vitu viwili tofauti.

  Gazeti lililoandika hii habari limeandikwa na mtupu mmoja ambae yeye ndio anadhani hii ni ishu ya watoto wa vigogo. Ukimuuliza Gavana Ndullu mwenyewe atasema hii ni ishu ya ku forge vyeti. Ni gazeti ndio halielewi. The crummy press I'm talking about.

  Ndio maana umeshtukia kwamba vitu havi add up kwenye hii habari. Nasema Tanzania hatuna press! Inawezekana 50% ya mambo tunayoyapigia kelele hapa yanatokana na misinformation. I tell you. Ohooo! Hakuna viable press! Hakuna anaejua kinachoendelea Bongo kwa kusikiliza hii media uchwara.
   
 5. H

  Humble Servant Member

  #5
  Sep 19, 2008
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  pamoja na yote hayo lazima tujifunze kuappreciate atleast kidogo kilicho fanyika!si sawa na bure inajenga precedence nzuri kuonya watu wenye michezo ya kuforge vyeti ili kupata kazi kwenye mashirika ya uma au pengine popote nchini! kwa mtazamo wangu badala ya kukazana kulaumu tumpongeze gavana ndulu na tumtie moyo kwenda hatua nyingine mbele kufika hadi huko tunapo tamani, tusimkatishe tamaa kwa kuwa wachoyo wa shukrani!

  hongera gavana!jitie nguvu uende hatua ya pili ili tukushangilie kwa nguvu zaidi.........!!!!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,286
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Changa la macho......
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mnaonea Dagaa.

  Watu wamegushi Bachelar Masters na PhD mnawatazama tu.
  Mnakamata walio gushi Vyeti vya O Level.

  Huu ni ufisadi mwingine wa kutumia madaraka vibaya.
   
 8. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2008
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Madele wa -Madilu,
  Tangu lini ulisikia wanliwa samaki wakubwa? hali ya sasa ni ngumu kuingia hao watoto wa wakubwa kwani yupo mtoto wa Lowasa sasa wanajua itaonekana wanamfuata EL. Sasa hata mtoto wa Kigoda anayesemekana alifeli kaingia kwa gia hapa kapona. Waandishi wetu feki walitakiwa waambane gavana kwa hili, huyu mtoto wa Mungai katumika tu kunyamazisha walalahoi. Vita ni kali na ngumu.
   
 9. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kila kiumbe hulia mama yangu na hali mama yetu (fumbo mfumbie mjinga )
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Sep 20, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine huwa nasikia kichefu chefu ninapo sikia au kusoma hizi habari. Yaani hata huyo mtoto wa kigogo babake hakujuwa kuwa mwanawe ni zero minus...! Duh! Mi nilifikiri kufoji ni kwa walala hoi tu...!? Inabidi tuige style ya China jinsi ya kuwahukumu Mafisadi...!
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hawa wametolewa kafara. Hoja ya msingi imewekwa pembeni kabisa....
   
 12. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  :D:rolleyes::confused:

  Teh hehe teh! Yaala...Migogo hiyo. Hizi Kafara!, Lo!-:eek:


  Waandishi wa Habari lazima waombe samahani kwa Wana-Nchi na vigogo wote!

  Mbona Tunadanganyana? Watoto wa Vigogo wana Hesabu hela?


  Wito.

  Ramadhani na Nora..Naomba mjiuzulu Kalamu zenu!!!
  Kula Breki!!!
   
 13. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,075
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya uchunguzi wa ajira tata za watoto wa vigogo BoT. Habari ndio hiyo!
   
 14. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du makubwa hata mtoto wa Mh!!!!!!!!!!!!!!Baba hakujua au alimsaidia upata kazi??Bado tunataka hela yetu ya EPA msikwepekwepe eti watu waligushi vyeti.
  Kugushi umekua mchezo wa wengi kila kazi ikichunguzwa hata za Serikalini wengi watakamatwa.Na wabunge wanaopata degree fake tuwafanye nini???
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hapo kiiini macho tu mbona watoto wengine tunao wajua walifeli na wamebebwa kihuni huni wameachwa??Hawa dagaa tu wametolewa kafala.
  Kumbukeni huyo mtoto wa Mungai wamemmaliza kutokana na hali ya siasa ya Joseph Mungai J.J graph yake kushuka mpaka kuwa zero....kwa sasa Mungai hana chake ndo maana wamemmaliza....saizi Mungai hata arudi Mufindi agombee ubalozi wa Nyumba kumi watu hawamchagui katu.
  Kumbukeni alivyo dondokea pua kwenye uchaguzi wa uenyekiti mkoa na ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kwa hiyo hana nguvu tena ndo baba wa watu wanammaliza kabisa........hana chake tena graph yake imeshuka na inasoma zero sijui kama ana hamu tena hata ya kugombea ubunge 2010.
   
 16. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tafsiri ya kughushi kama tungeifuatilia, na kurudisha standard zitakiwazo mtu awe na cheti kipi ili kitambuliwe watu wengi wanaosema wana "Degree" wangekuwa nao wamegushi. Kuna waTZ kibao mpaka mawaziri ni maDr. lakini vyuo walivyosoma kazi kweli kweli (non-accredited Colleges and Universities). Hawa hawashughulikiwi, na ndio walio juu. Lakini walighushi vyeti wanakuwa "Bangusilo".
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii kweli kiini macho, changa la macho!!!!!!!!

  Wapi mbunge Chitalio??????????????????????????????? Au yeye ni above the rim the so called law of the land.
   
 18. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,251
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  "Habari zilizopatikana nje ya mahakama na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wa serikali, zilisema kuwa, washtakiwa hao wote wanafanya kazi ya kuhesabu fedha BoT."
  Pants On Fire!!
   
 19. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa wanakamata hao waliogushi form 4 badala ya wale walioiba mamilioni? (Rostam, Lowassa, Apson...etc)...
  akamatwe pia na Dr. Nchimbi kwa kufoji cheti.
  kweli nchi inaendeshwa kiutani utani tu.
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,815
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hapa huenda tunachanganya vitu viwili, kugushi cheti na kutumia cheti toka chuo ambacho hakina accreditation ni vitu viwili tofauti.

  Tumshukuru Prof. Ndullu maana japo yeye kajaribu. Ni rahisi sana kupata matokeo halali ya form four na six na kisha kulinganisha.

  Tatizo liko kwa serikali ambayo imeshindwa kutunga sheria zenye meno za kuwashughulikia wale wanaogushi vyeti vya elimu za juu.

  Kwa mfano huwezi kumshitaki Nchimbi kwa kugushi cheti, ingawaje kama nchi inaweza isitambue cheti chake na hivyo kumfanye yeye asijiite Dr.

  Pia kuna jambo lingine ambalo linachanganya Tanzania. Nafikiri hata uwe na Ph.D unapoomba kazi lazima utoe na matokeo ya form four, hapo ndipo kugushi kunaanza. Wengine huko nyuma walikuwa na matokeo mabaya au kuna watu wamesahau matokeo yao.

  Kwenye hili mimi nampongeza prof. Ndullu, japo ni hatua ndogo lakini angalau yeye ameanza. Laiti spika Sitta na yeye akaanza na wabunge, JK na mawaziri wake nk. huenda tukasogea kidogo.
   
Loading...