Wafanyakazi na Wafanyabiashara, mnajilinda vipi dhidi ya COVID19 huku mkitimiza majukumu?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Ugonjwa wa Corona unaambukiza kwa kupitia hewa, majimaji yanayokaa kwenye mate na ute wa kohozi. Tangu kutokea kwa mlipuko wa Ugonjwa wa Corona mnamo mwaka jana (2019) mataifa mbalimbalimbali yamekuwa yakichukua tahadhari ili kuzuia maambuki zaidi kwa Wananchi.

Tanzania ni moja ya Nchi iliyofanya taratibu hizo za kuzuia kusambaa kwa kasi kwa maambukizi hayo ikiwemo kufunga Shule na Vyuo, baadhi ya mikusanyiko kama kudhuria nyumba za Ibada iliahirisha, matumizai ya usafiri wa Umma yalibadilika na mambo mengine mengi.

Mnamo Mei 21, 2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alitangaza rasmi kufunguliwa kwa Vyuo na Shule (Kidato cha Sita) kutokana na maambikizi kupungua kwa kiasi kikubwa katika Nchi. Vilevile, Rais alitangaza kufunguliwa/kurejea kufanya kazi kwa biashara na ofisi tofauti tofauti ambazo zilifungwa ili kuchukua tahadhari.

Rais alitangaza kurejea kwa shughuli hizo ila kwa tahadhari kwa kuwa Ugonjwa wa Corona bado upo. Kwa kuwa shughuli mbalimbali zinarejea kama awali ni vyema tukajua namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa
(1) Wafanyakazi na (2) Wafanyabiashara. Wafanyakazi wamegawanyika kwenye makundi mawili: (a) Wanaokutana na watu (Wafanyakazi wa Benki n.k.) (b) Wasiokutana na watu sana

JINSI YA KUJILINDA NA MAAMBUKIZI YA CORONA WAFANYAKAZI WASIOHUDUMIA WATEJA ANA KWA ANA

 Kuvaa Barakoa: Kama unatumia usafiri wa Umma, wakati wote unapokuwa kwenye usafiri unatakiwa kuwa umevaa Barakoa au unapokuwa kwenye eneo lenye watu wengi kama Stendi ya Magari. Hii itasaidia usipate maambukizi na kama umeshapata maambukizi basi utalinda wengine
 Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia Sanitizer: Kila mfanyakazi afikapo atatakiwa kunawa mikono kabla hajashika kitu au eneo lolote la ofisi na wakati wowote anaposhika kitu kilichoshikwa na mtu mwingine. Hii itasaidia kuwalinda wafanyakazi wengine na maambukizi iwapo kwa namna yeyote atakuwa ameshika sehemu zisizo salama alipokuwa nje ya ofisi
 Mpangilio wa ukaaji wa wafanyakazi ofisini: Wafanyakazi watatakiwa kukaa kwa namna itakayosaidia kudhibiti maambukizi ikiwa kuna aliyepata maambukizi. Umbali kati ya mtu na mtu unashauriwa kuwa kuanzia Mita Moja (1)
 Kuepuka kujishika Uso (Pua, Mdomo au Macho): Kwa kuwa ugonjwa huu unaambukizwa kupitia majimaji kutoka kwenye mate na ute wa kohozi hivyo unashauriwa kuepuka kujishika sehemu hizo za uso kwani mikono yako inaweza kuwa imebebeba virusi hivyo
 Jengo la Ofisi na maeneo yote yanatakiwa kusafishwa na Dawa maalum: Kwa kuwa wafanyakazi wote wanatakiwa kuchukua tahadhari mbalimbali kujikinga kama maeneo wanayofanyia kazi hayatawekwa salama basi tahadhari zao hazitafanya kazi. Hivyo maeneo ya ofisi yanatakiwa kuwa salama kwa kusafishwa na kupuliziwa dawa
 Beba chakula kutoka Nyumbani: Kwa kuwa ni ngumu kuangalia na kulinda namna ya uandaaji wa chakula kwa mtu mwingine hivyo utakuwa salama zaidi pale unapobeba chakula ulichoandaa mwenyewe kwa kuzingatia tahadhari
 Wafanyakazi kuepuka mkusanyako/msongamano usio wa lazima: Kuwe na utaratibu maalum wakati wa kula na kujipatia huduma nyingi ambazo mara nyingi hukusanya watu eneo moja.
 Kuhakikisha upatikanaji wa vitakasa mikono: Uwepo wa vitakasa mikono utasaidia kuweka wepesi kwa mtu kujisafisha anapokuwa eneo la ofisini
 Uwepo Vibandiko vinavyokumbusha kujiweka salama: Kunapokuwa na vibandiko hivi itasaidia kukumbusha watu iwapo amesahau au anataka kuzembea kuchukua tahadhari hizi za kujikinga na gonjwa la Corona

WAFANYAKAZI WANAOHUDUMIA WATEJA ANA KWA ANA

Wafanyakazi wanaokutana na wateja ana kwa ana watatakiwa kuchukua tahadhari zinazofanana na wasiohudumia wateja ana kwa ana ila wao watatakiwa kwenda mbali zaidi
 Umbali kutoka kwa mfanyakazi (Mtoa huduma) hadi anayehudumiwa: Inashauriwa ili kuzuia maambukizi umbali wa kutoka mtu mmoja hadi mwingini uwe ni kuanzia Mita Moja (1) hadi Sita (6)
 Uwepo wa uzio maalum ili kutenganisha : Ili kumtenga mtua huduma na mhudumiwa kuwe na uzio ili iwapo mmoja wao akisahau kuchukua taadhari basi uzio ule utakuwa umewatenganisha
 Sanitize au nawa mikono unaposhikia vitu ambavyo vinashikwa na wengine: Wakati wowote unapokuwa unatoa huduma na ikatokea kuna kitu unakishika ambacho mteja ia alishika basi utatakiwa kunawa mikono ili kujiepusha na maambukizi
 Kuhakikisha upatikanaji wa vitakasa mikono: Uwepo wa vitakasa mikono utasaidia kuweka wepesi kwa mtu kujisafisha kabla ya kupokea huduma hivyo kuwalinda na watoa huduma pia
 Uwepo Vibandiko vinavyokumbusha kujiweka salama: Kunapokuwa na vibandiko hivi itasaidia kukumbusha watu iwapo wamesahau au wanataka kuzembea kuchukua tahadhari hizi za kujikinga na ugonjwa wa Corona

WAFANYABIASHARA

 Usafi wa maeneo ya biashara: Usafi wa eneo la biashara ni jambo la lazima kwani hii itasaidia kuondoa maambukizi yoyote iwapo kuna maambukizi
 Kuvaa Barakoa: Wakati wowote mfanyabiashara anapokuwa anatoa huduma anatakiwa kuwa amevaa Barakoa ili kujilinda na maambukizi na pia kuwalinda wale anaowahudumia
 Uhifadhi wa Pesa kwenye simu: Kwasababu pesa hupita mikononi mwa watu wengi hivyo ni vyema kutumia njia ya uhifadhi wa pesa kwenye mitandao ya simu au benki wakati wa kufanya malipo
 Kunawa mikono: Mfanyabiashara anatakiwa kunawa mikono wakati wowote anaposhika bidhaa iliyoshikwa na mteja kwani kwa kufanya hivi atajiepusha na maambukizi iwapo mteja atakuwa na maambukizi
 Umbali kati ya mfanyabiashara na mteja: Inashauriwa kuwa na umbali wa Moja (1) hadi Sita (6) kati ya mteja na mfanyabiashara ili kuepusha maambukizi wakati wa kuongea au kupiga chafya.
 Hakikisha upatikanaji wa vitakasa mikono: Uwepo wa vitakasa mikono utasaidia kuweka wepesi kwa mtu kujisafisha kabla ya kupokea huduma hivyo kuwalinda na watoa huduma pia
 Uwepo Vibandiko vinavyokumbusha kujiweka salama: Kunapokuwa na vibandiko hivi vitasaidia kukumbusha watu iwapo wamesahau au wanataka kuzembea kuchukua tahadhari hizi za kujikinga na gonjwa wa Corona
 Hudumia mteja mmoja kwa wakati: Ukifanya hivi itasaidia kupunguza msongamano wa wateja ambapo kwenye msongamano. Ni ngumu sana kuchukua tahadhari hivyo panapokuwa na mteja mmoja kwa wakati itasaidia zaidi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom