Wafanyakazi hewa wajitumbue wenyewe

mikeimani

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
3,032
1,855
Ndugu wana jukwaa, salaam

Mimi naamini ni bora wale wote wanaopokea mshahara wa serikali na wanajua hawastahili kuupokea wajitokeze wenyewe na kusema kwamba makosa yalifanyika hivyo wasiendelee kupewa hizo hela.

Inawezekana wapo ambao bado wako serikalin na wanachukua mshahara zaidi ya mmoja. Au inawezekana hawako serikalin lakini bado wanachukua mshahara wa serikali. Au walishakufa lakini ndugu zao bado wanachukua huo mshahara na nk.

Naamini hizo cases zipo na serikali ianzishe desk maalum la kushughulikia jambo hili kwa namna hii.

Inaweza tangazwa kuwa mwisho wa zoezi hili bila kifunguliwa mashtaka 'labda ni mwezi mmoja tangia tangazo litoke'.

Kuweka kipindi cha kurekebisha mambo kabla ya kutoa adhabu ni jambo jema kwani hufanya wafanya makosa kujitokeza wenyewe na hivyo kupunguza usumbufu na gharama za kufuatilia lakini pia ufanisi wa kazi yenyewe unakuwa juu.

Nawasilisha
 
kwenye halmashauri tatizo lipo kwa wakuu wa idara, baaaasi. wanazo taarifa zote za wafu, watoro, walio acha kazi wenyewe,.........................kila mwisho wa mwezi husain karatasi za pay- rool zenye majina ya watu wanaojulikana kutokuwepo kazini kwa sababu yoyote inayo wafanya wasistahili kulipwa mshahara.
 
Back
Top Bottom