mangonjoli
Senior Member
- Aug 29, 2012
- 154
- 110
Wafanyakazi wanaohusika na kazi za usafi kwenye kiwanda cha Cement Dangote Mtwara. wamelalamika mshahara mdogo wanaolipwa kiwandani hapo na kampuni iliyochukua tenda kwenye kiwanda hicho ya HIGHLAND FUMIGATION ENTERPRISES. "Kiukweli tunalipwa sh 7000. kwa siku na pesa zetu tunalipwa mwisho wa mwezi ila malipo hayo hayahusiki na Siku za mapumziko kama jumapili na Siku za sikukuu.Kwahiyo kila mwezi ukitoa jumapili 4 tunalipwa pesa ya siku 26 au 25 kutegemea ukubwa wa mwezi. mbaya zaidi mwezi kama huu wa sikukuu tunaweza kuja kuambulia 168,000".Aliongea kwa masikitiko mfanyakazi Huyo wa Dangote. Habari za ndani zinasema Muhindi wa Dangote anawalipa sh 12,000. ila kampuni ya HIGH FUMIGATION ENTERPRISES .Ndio inawapiga panga wafanyakazi hao na kuwalipa sh 7000.