Wafanyakazi Bulyanhulu kugoma

...i dont like politics kwenye issue zenye maslahi pande zote kama hii na sitaki serikali iingilie kimabavu is just one company Vs wafanyakazi 900...sheria ifanye kazi yake tuone nani mwenye haki,hapo ndio utajua kama wafanyakazi wanajua kuweka fight ya kweli au ni unafiki mwingine tuu...haki yao iko mahakamani watafute lawyer mzuri na waendelee kugoma au kurudi mezani for more negotiations
 
so CMB wataka kusema wasupport barrick?
if its so just immagine umepata fweza za bingo..then can u go to a foreign country kama uko europe au hata kwa bush na kimada wake rice..ukanunu kampuni halafu ukaweza just fire them all 900 workers??????

I said support meaning that, statement ya barrick itaelezea mengi kuhusu wafanyakazi, sio kwamba na support wao kufukuzwa.
 
Ndugu Mwiba upo hapo ? This is another big test kwa JK and his leadership na wala Nchi wenzake na ndiyo maana kainuka kwenda china kukwepa majukumu.Kweli watu 900 kwa wazungu wachache ndani ya Tanzania ambayo neema inawezekana ? Nchi yao na maliasili zao toka Mbinguni ? Ama kweli Mwiba tutaona JK atafanya nini .

UK watu 200 walisababisha tukauziwa rada ambayo ilikufa kabla ya kazi yake na bado tunalipia je watu 900 can they be sacrified kisa wawekezaji ?
 
...jamani kama mnapenda free market acheni hii issue iwe btn Barric Vs 900 employee,kwanini mnataka serikali ichukue side? hizi ndio double standard naita,nina uhakika kuna sheria za kazi hope zitatoa haki na wala sio JK kama wengi mmnavyotaka aingilie...sio kwa sababu Barrick ni Foreigners ndio tuone kama wana makosa,nchi itaendelea kama haki na usawa unatolewa kutokana na sheria zilizopo ambazo sisi wenyewe ndio tumeziweka na ukiona tunazilalamikia itabidi sisi wenyewe ndio tuzifanyie kazi kuzirekebisha ,najua hao employee they'll fight this tooth & nail to the end na wakishindwa sheria haikuwa upande wao na itakuja tena kupunish wengine next time
 
...jamani kama mnapenda free market acheni hii issue iwe btn Barric Vs 900 employee,kwanini mnataka serikali ichukue side? hizi ndio double standard naita,nina uhakika kuna sheria za kazi hope zitatoa haki na wala sio JK kama wengi mmnavyotaka aingilie...sio kwa sababu Barrick ni Foreigners ndio tuone kama wana makosa,

Ok hapa nakubaliana nawe kiaina

nchi itaendelea kama haki na usawa unatolewa kutokana na sheria zilizopo ambazo sisi wenyewe ndio tumeziweka na ukiona tunazilalamikia itabidi sisi wenyewe ndio tuzifanyie kazi kuzirekebisha ,najua hao employee they'll fight this tooth & nail to the end na wakishindwa sheria haikuwa upande wao na itakuja tena kupunish wengine next time

Hapa umeanza kuchanganya, hapo juu umesema kuwa JK hatakiwi kuingilia, na hapa chini unasema sheria zibadilishwe! Nadhani unatambua nafasi ya rais kwenye kutunga au kubadili sheria za nchi? ni kipi basi ambacho hutaki JK afanye au asifanye?
 
Mwafrika kazi ya JK sio kutunga sheria na hana huo uwezo kikatiba ni BUNGE TUU...back to the isue sioni why JK ajiingize kwenye issue kama hii labda for a goodwill kusaidia pande zote mbili waelewane tuu,ukiona Raisi aningilia issue kama hizo ni dalili za udikteta...acheni sheria ifanye kazi,kama haifanyi kazi bunge litunge nyingine ndio demokrasi
 
Mwafrika kazi ya JK sio kutunga sheria na hana huo uwezo kikatiba ni BUNGE TUU...back to the isue sioni why JK ajiingize kwenye issue kama hii labda for a goodwill kusaidia pande zote mbili waelewane tuu,ukiona Raisi aningilia issue kama hizo ni dalili za udikteta...acheni sheria ifanye kazi,kama haifanyi kazi bunge litunge nyingine ndio demokrasi

Yup,

nimetumia neno nafasi ya rais kwenye kutunga au kubadili sheria.
Bunge linatunga sheria lakini raisi anasaini ili ziwe sheria au anazikataa. Bunge la Tanzania linaunda kwa kiwango kikubwa na serikali ya sisiemu ambayo Kikwete na mkiti wake. On the other side Kikwete ananafasi ya kupush whatever anataka kiwe sheria kwenye vikao vya sisiemu na kisha akasaini mara tu vinapopita kwa kishindo bungeni (kama nguvu ya sisiemu bungeni iliyomfukuza zitto toka bungeni).

Barrick kulingana na kinachoonekana kwenye mkataba wa Buzwagi wamemepewa nguvu kubwa sana ya kufanya wanachotaka. Bila Raisi au uongozi wa sisiemu kuingilia kati hawa jamaa watafanya kila wapendacho.

Unachosema ni kweli kama hiyo sheria unayotaka ifuatwe ingekuwa fair in the first place!
 
...whatever it is hicho chama cha wafanyakazi ndio kilitakiwa kuwa lobbyst mkubwa katika bunge ili kubadilisha sheria za kutetea maslahi ya wafanyakazi lakini kazi yao ni kutishia tishia tuu useless migomo kila mwaka ambayo haina faida yeyote na kupotezea watu muda tuu,sometimes tunajirudisha nyuma wenyewe tuu
 
...whatever it is hicho chama cha wafanyakazi ndio kilitakiwa kuwa lobbyst mkubwa katika bunge ili kubadilisha sheria za kutetea maslahi ya wafanyakazi lakini kazi yao ni kutishia tishia tuu useless migomo kila mwaka ambayo haina faida yeyote na kupotezea watu muda tuu,sometimes tunajirudisha nyuma wenyewe tuu

mhhh,

kwa hiyo wa kulaumiwa hapa ni wafanyakazi wa Barrick na wala sio kampuni la Buzwagi linalowanyonya au JK na serikali yake walio saini mikataba na kutunga sheria mbovu!

kwa mwendo huu haya maisha bora yawe ndoto!
 
...unavuna ulichopanda,sio siri chama cha wafanyakazi ni one wing ya CCM na CCM ndio watunga sheria na nyie wafanyakazi ndio supporter wakubwa wa serikali ya CCM mnaowaweka madarakani...sasa leo mnamlaumu nani? unafiki wa vyama vya wafanyakazi na kujipendekeza kwao CCM huku wakisahau kazi yao ni maslahi ya wafanyakazi wao ndio mwanzo wa matatizo yote haya
 
...unavuna ulichopanda,sio siri chama cha wafanyakazi ni one wing ya CCM na CCM ndio watunga sheria na nyie wafanyakazi ndio supporter wakubwa wa serikali ya CCM mnaowaweka madarakani...sasa leo mnamlaumu nani? unafiki wa vyama vya wafanyakazi na kujipendekeza kwao CCM huku wakisahau kazi yao ni maslahi ya wafanyakazi wao ndio mwanzo wa matatizo yote haya

Haya Mkuu,

hapa umenena, nanukuu pia maneno ya Mramba kuwa watanzania hata wakila nyasi.......

kazi ipo!
 
...jamani kama mnapenda free market acheni hii issue iwe btn Barric Vs 900 employee

..nani alikudanganya kuna free market duniani? ina maana hawa wazungu wakija kuambia wewe ni mjukuu wa babu yao utaamini kiurahisi bila kuchungua family tree yenu?

..halafu nani alikuambia kwamba wafanyakazi hawana haki ya kudai kile wanachoona kuwa ni haki yao?

..we unajua kitu inaitwa uaw au kitu kama hicho huko us of a?



kwanini mnataka serikali ichukue side? hizi ndio double standard naita

..ichukue what?ushaona kutetea wananchi ni kuchukua sides sio?kwa hiyo,tuseme hii serikali ni ya nani? jk&co.? acha kutukana viongozi wa nchi katika suala lisilohusika!


nina uhakika kuna sheria za kazi hope zitatoa haki na wala sio JK kama wengi mmnavyotaka aingilie

..regardless ya sheria,ana uwezo wa kuingilia kadri atakavyo!au haujui?...hata kukaa kimya ni kuingilia pia!

..achana na sheria za kazi!wao si wajinga kuzi-ignore!

sio kwa sababu Barrick ni Foreigners ndio tuone kama wana makosa

..kwakuwa we ni local ndio tuone uko sawa na unachokisema hakina dosari?

nchi itaendelea kama haki na usawa unatolewa kutokana na sheria zilizopo ambazo sisi wenyewe ndio tumeziweka

..how naive of you?....sina la zaidi hapa!

nb:jaribu kama utaweza kuongea na wanaofanya kazi huko! labda utapata mwanga zaidi! btw....no hard feelings,take it easy on above comments!
 
....dar si lamu emotions kwenye vitu kama hivi u'll end up looser,na wala sitetei Barrick ninachokataa hapa ni watu kufikiria JK anaweza kutoa haki kwa hao wafanyakazi...yeye sio Judge wala court ambako naamini ndiko haki ya kweli itapatikana,na kama umenielewa kuna haja ya kubadilisha sheria nyingi sana ambazo zinamwonea mfanyakazi ambazo wawekezaji smart & experience wana uwezo wa kuzitumia effectivelly to their advantage....anyway support JK aingilie uone TZ tutakavyoburuzwa kwenye international court and end up compensating millions to Barrick,better be smartn vitu kama hivi and follow the law kuliko politics mbele utaumia...remember IPTL? who s the looser?
 
....dar si lamu emotions kwenye vitu kama hivi u'll end up looser

..haya sio mapenzi mkuu,kwahiyo issue ya emotions haipo!

..ila point taken!

na wala sitetei Barrick ninachokataa hapa ni watu kufikiria JK anaweza kutoa haki kwa hao wafanyakazi

..kutoa haki anaweza,kama atakavyofanya haki kutimiza ahadi zake kwa wananchi!


yeye sio Judge wala court ambako naamini ndiko haki ya kweli itapatikana,na kama umenielewa kuna haja ya kubadilisha sheria nyingi sana ambazo zinamwonea mfanyakazi

..nimekupata mkuu,heshima mbele!ila the guy can be above the judges at times[for the sake of fairness,of which you are talking about]!

ambazo wawekezaji smart & experience wana uwezo wa kuzitumia effectivelly to their advantage....anyway support JK aingilie uone TZ tutakavyoburuzwa kwenye international court and end up compensating millions to Barrick

..hapa umekuza kidogo mkuu,ingawa kuna ukweli!
 
" SITAJIHUSISHA NA MGOMO WOWOTE BATILI" hii ndio law of the land inayotumika kuwaadhibu wote wanaogoma kazini,na barrick wameitumia effectivelly na mbele ya sheria wako sawa...sasa bora kuanza kupigana na sheria za kikoloni na unyanyasaji kama hizi ndio tutaendelea la sivyo ni ndoto
 
Sheria batili ni katika kuyaweka mambo yasionekane makali kama yalivyo. Mgomo ni mgomo tu, na sasa wafanyakazi ndio wamenyanganywa right ya kugoma pale kunapotokea kutokubaliana baina ya pande mbili. Sasa wafanyakazi wanatakiwa wafanye nini? Sheria za kazi Tanzania imeweka bayana, migomo ni illegal. Personally, I have a big problem with that.

Speaking of which, Vitu kama hivi ndio inabidi watu, nahii sio waTanzania na Tanzania pekee, bali dunia tupigane navyo. We give Corporations too much power and in turn they use them against us. Ku-sign hizi contract za kazi inabidi u-sign, kwasababu unataka kazi. It should be a win win, but in this case, makampuni yana win in most cases and wafanyakazi wana-lose. Really, Employers wana-retain too much power! Sasa hizi ndio ethical issues tunazozungumzia kila siku, kwakweli inabidi tuanze kuzi-address. Wanasheria mko wapi?
 
Hapana kwenye hili wakuu tuwe wakweli, sheria ni sheria, Barrick hawana kosa lolote kuhusiana na mikataba na the rest of the story, tatizo ni letu wenyewe, kuanzia bunge na viongozi wetu, tuliowachagua wenyewe,

Sheria za kazi za Barrick, ambazo wafanyakazi waliogoma walizisaini wenyewe wakati wakiajairiwa ziko clear kuwa ukigoma, Barrick, wakakupa dead line ya kurudi kazini, usiporudi ni haki yao kisheria kukufukuza na kuzitangaza nafasi hizo kwa public, na ukiweza unaweza omba tena upya lakini hutakuwa na any special consideration,

Tanzania, au Barrick sio wa kwanza kukutwa na hii kitu, hata serikali ya USA, hairuhusu wafanyakazi wake kugoma, ukigoma unakuwa umejifukuza mwenyewe, mnyonge mnyongeni, lakini kwenye hili wafanyakazi waliogoma simply wamekuwa missguided warudi tu kuomba msamaha au kuomba radhi wasamehewe, au waombe kazi upya, wanafukuzwa wananfunzi wetu, sasa itakuwa Barrick?
 
Si kweli kama ukigoma kwa nchi uliyotolea mfano(USA) kuwa unafukuzwa kazi. Kuna sheria zinazowalinda wafanyakazi, migomo siku zote hai-result kufukuzishwa watu kazi.
 
Back
Top Bottom