Wafanyakazi Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walia njaa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( Bakwata) waliopo makao makuu Dar es salaam, wamelalamikia hatua ya kutolipwa kwa miezi minne, jambo linalowafanya waishi kwa shida

Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, alisema kukosa mishahara yao kumewafanya waishi kwa kukopa na kujikuta wakidaiwa madeni mengi mitaani

"Tangu Januari mwaka huu hatujalipwa, tunaishi kwa kukopa. Hapa tulipo tuna madeni kila kona, hata futari kwa familia zetu hatuna", alisema

Alisema kuchelewa kulipwa mishahara yao kumewafanya waingie kwenye mfungo wa Ramadhani wakiwa katika hali ngumu

Alipoulizwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka alisema suala hilo lipo chini ya ofisi ya Katibu Mkuu ambaye alishaanza kulifanyia kazi

"Tatizo hilo liko chini ya Katibu Mkuu, lakini lilikuwa linafanyiwa kazi na ninaamini kuwa kwa sasa litakuwa limetatuliwa", alisema Mataka

Lakini Mkurugenzi wa Habari wa Bakwata, Tabutabu Kawambwa alikanusha uwepo wa madai hayo na kusema kuwa hakuna mfanyakazi anadai mshahara, kwani wote walishalipwa tangu ulipoanza mfungo wa Ramadhani

"Hakuna mfanyakazi anayedai mshahara, wote wamelipwa walichokuwa wakidai ilikuwa ni posho ndogo ndogo na tayari wamelipwa", alisema Kawambwa

Alisema anaamini taarifa hizo zimetolewa na watu ambao wana nia ovu ya kulichafua baraza kutokana na kukosa madaraka, kwani wapo waliokuwa wakitarajia kupata vyeo ndani ya baraza hilo na sasa wamevikosa.

My take: Sasa mbona Mwenyekiti wa Bakwata amesema suala hilo linafanyiwa kazi. Na huyu Mkurugenzi anasema hakuna mfanyakazi kazi anayedai mshahara. Inamaana hakuna mawasiliano? Acheni mambo hayo, kama tatizo lipo ni vema likashughulikiwa

Chanzo: Mtanzania
 
Hali ni ngumu sana kwa kweli nakumbuka Ramadan za nyuma huko kila siku ulikua unasikia sijui kuna msanii mara company mara mbunge anafuturisha mtaa lakini siku hizi sizisikii hizi show-offs tena sababu uhakika wa kufuturu mwenyewe ni zero.
 
Mwenyekiti na Kawambwa yupi anasema kweli sisi hatujui.Kila mmoja wao katika nafsi yake anajua analo ongea na ALLAH ndiye mjuzi zaidi.
 
Karibuni Baraza la Maaskofu Tanzania,hakuna njaa
Hahaha kweli kule hakuna njaa kuna siku niliingia kanisa la Roman Catholic msoma matangazo alisoma zaka za mwezi mmoja tu wamekusanya million 185 na sadaka za kila Juma na michango mingine ni million 12 aise nilienda kwenye ubao wa matangazo kujiridhisha utimamu wa masikio yangu sikuamini nilichokiona.
 
Unajua awa wakurugenzi wa habari au ma PR wa organization mbali mbali pamoja government nahic uwa wanakula kiapo cha kuongea positive tu kuhusu organization zao...sasa tatizo linakuja akiwa hana taarifa ya kinachoendelea yeye uwa anakunusha tu..siyo watu wazur kuwahoji...unaweza husipate ukweli wa jambo.
 
Wavumilie tu, inshallah siku Mungu akiweka mambo mazuri watalipwa. Pia hata wakikosa mshahara watalipwa kwa thawabu na Mnyazimungu. Malipo yako Akhera sio duniani.
 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( Bakwata) waliopo makao makuu Dar es salaam, wamelalamikia hatua ya kutolipwa kwa miezi minne, jambo linalowafanya waishi kwa shida

Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, alisema kukosa mishahara yao kumewafanya waishi kwa kukopa na kujikuta wakidaiwa madeni mengi mitaani

"Tangu Julai mwaka jana hatujalipwa, tunaishi kwa kukopa. Hapa tulipo tuna madeni kila kona, hata futari kwa familia zetu hatuna", alisema

Alisema kuchelewa kulipwa mishahara yao kumewafanya waingie kwenye mfungo wa Ramadhani wakiwa katika hali ngumu

Alipoulizwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka alisema suala hilo lipo chini ya ofisi ya Katibu Mkuu ambaye alishaanza kulifanyia kazi

"Tatizo hilo liko chini ya Katibu Mkuu, lakini lilikuwa linafanyiwa kazi na ninaamini kuwa kwa sasa litakuwa limetatuliwa", alisema Mataka

Lakini Mkurugenzi wa Habari wa Bakwata, Tabutabu Kawambwa alikanusha uwepo wa madai hayo na kusema kuwa hakuna mfanyakazi anadai mshahara, kwani wote walishalipwa tangu ulipoanza mfungo wa Ramadhani

"Hakuna mfanyakazi anayedai mshahara, wote wamelipwa walichokuwa wakidai ilikuwa ni posho ndogo ndogo na tayari wamelipwa", alisema Kawambwa

Alisema anaamini taarifa hizo zimetolewa na watu ambao wana nia ovu ya kulichafua baraza kutokana na kukosa madaraka, kwani wapo waliokuwa wakitarajia kupata vyeo ndani ya baraza hilo na sasa wamevikosa.

My take: Sasa mbona Mwenyekiti wa Bakwata amesema suala hilo linafanyiwa kazi. Na huyu Mkurugenzi anasema hakuna mfanyakazi kazi anayedai mshahara. Inamaana hakuna mawasiliano? Acheni mambo hayo, kama tatizo lipo ni vema likashughulikiwa

Chanzo: Mtanzania

Uandishi wa kijinga kweli kweli huu. Para moja hawajalipwa miezi minne, para nyengine hawajalipwa toka July mwaka jana.

Kama si upunguani ni nini huo?
 
Back
Top Bottom