Wafanyakazi 30 wa kilimo Gairo wamenyimwa mshahara Jan na kuwekwa mahabusu

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Wafanyakazi wa kilimo Kama 30 - 40 wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wamekamatwa na kuwekwa ndani baada ya kunyimwa mshahara wa January kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baada ya kupewa kufanya kazi ya kukusanya ushuru katika vijiji tofauti na kuwasilisha mapato Kama walivyoelekezwa wakati wanakabidhiwa hiyo kazi

Cha kushangaza ni kwamba Watumishi wamefanya kazi kwa uwaminifu mkubwa na kukabidhi mapato Kama walivyotakiwa lakini inaonekana Kuna viongozi wa juu wamefanya ubadhirifu wa hizo fedha na kuwasingizia Watumishi wa chini ambao wana taarifa zao zote kikazi kwa maana ya Kila wakifanya kazi wanakabidhi taarifa zao kwa wakubwa wao.

Sasa wanasakwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kulazimishwa kulipa Kila mmoja kitu ambacho kinaleta ulakini kwa wale waliofanya kazi kwa uwaminifu mkubwa.

Kuna umuhimu wa vyombo vya juu kuangalia namna ya kufanya Watumishi wa chini waipende Serikali yao kuliko hivyo inavyofanywa kwa kuwaonea baadhi ya Watumishi waaminifu na wanyonge

Nimejitahidi kufanya mawasiliano na viongozi wa Wilaya na mkoa ktk hilo sakata lakini simu zao hazipokelewi na zingine


Updates
Wafanyakazi wote yaani maafisa ugani wameachiwa huru juzi usiku baada ya kuhojiwa na wapelelezi kutokana mkoani Morogoro na kubaini irregularities nyingi Sana ktk ukusanyaji na makabidhiano ya hizo pesa kiasi cha kupanga jinsi ya kuwahoji viongozi wakuu wa Halmashauri ili kubaini ukweli wake zoezi zima

Ila maafisa ugani wote inasemekana watahitajika kufika Tena Makao makuu ya Halmashauri tarehe iyopangwa Kati ya tarehe 3 au 4.
 
Wanalazimishwa kulipa na wengine wanalipa kupitia Polisi lakini wengine wanasema kwanini walipe wakati hawana makosa? Na hawajala pesa yoyote?
Duh!..haya mambo ya matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa mikoa na wilaya yameshamiri Sana kipindi hiki.
 
Vitu hivi huenda mbele na kurudi nyuma..

Kuna watu watataabika saana baada ya nyakati zao kwa kujiona Miungu watu kipindi cha kuanzia 2015-2020.

Kuna baadhi ya viongozi akili zao zinashindwa kwenda na wakati.Wanaturudisha enzi zile za Mjerumani na Mwingereza.
 
Pesa yote ya serikali inakusanywa kwa kutumia machine zinaitwa POS yani point of sales nakula unapokata risti inasoma moja kwa moja makao makuu ya Halmashauri unapoenda kukabidhi makusanyo unatolewa bill kwa kutumia ID yako unakwenda kudipost makusanyo kwa kutumia control namba iliyopo kwenye bill yako. Unaweza kulipa kwa m- pesa, benki au kwa wakala.Unapolipa
 
Pesa yote ya serikali inakusanywa kwa kutumia machine zinaitwa POS yani point of sales nakula unapokata risti inasoma moja kwa moja makao makuu ya Halmashauri unapoenda kukabidhi makusanyo unatolewa bill kwa kutumia ID yako unakwenda kudipost makusanyo kwa kutumia control namba iliyopo kwenye bill yako. Unaweza kulipa kwa m- pesa, benki au kwa wakala.Unapolipa
Sasa kwanini mnawalizimisha kulipa Kama huo ndiyo utaratibu??
 
Back
Top Bottom