Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mnamo Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli anayefahamika kwa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini mkoani Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dk. Makakala amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" amesema Dk. Makakala.

Sambamba na hayo, Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa Wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weledi, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka).

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria, Pia idara hiyo imewataka Watanzania wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Pia soma; Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

20210530_162929.jpg
 
Katika ile video inaonekana askari wasiopungua watano (ikiwemo sauti za wengine kadhaa zikihimiza ile adhabu ikaziwe), kwanini watatu tu ndio waliosimamishwa?
Pia tunataka majina na picha zao ziwekwe hadharani.

Kuna namna hapa watu fulani wanataka kulindwa.
 
Hii ndio reflection ya akili za askari wetu....sijui kama uwa wanafikiria matokeo kabla ya kufanya jambo
 
Huyo Tapeli hajafanya Jambo jema Ila nao maofisa wetu wa vyombo vya dola wajifunze kutumia reasonable force ku handle mtuhumiwa.

Ukimkamata mtuhumiwa inakua vyema ukamfikisha kituo Cha polisi na sio kumdhalilisha kwa namna yeyote.

Jambo hili limejengeka Kwa muda mrefu sana katika jamii yetu kuwaadhibu watuhumiwa kabla ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Tatizo linaweza kuwa limetokana na mifumo labda kutotoa matokeo ambayo baadhi yetu tunadhani ndio sahihi,

Ila jamii inapaswa kuelemishwa kwamba ukiachana na matokeo ya huko ambako utampeleka mtuhumiwa unapaswa kumfikisha Kwanza polisi.
 
Sasa mbona wale wanajeshi wanaopigaga watu sijawahi kuskia wakisimamishwa,

Wanajeshi ndo huwa wanazingua zaidi.
 
Back
Top Bottom