Wafanyakazi 134 wakutwa na vyeti feki hospitali ya Muhimbili, majina yao haya

itakuwa ndo hao walikuwa wakiwafanyia watu surgery za kichwa badala ya miguu manza fanta zao
 
Hawa ni watu wenye ujuz kabisa leo wanaondoka muhimbili pamoja na changamoto zote za utabibu zilizopo pale, MH. Ungedeal na hawa wanaonza kuingia makazini hao waliopo wangepotea wenyewe tu nje ya hapo mtaua watu pressure na pia tutapungukiwa na wataalamu hasa katika sekta muhimu kama ya afya.

Yaani wewe unawazia kupata ajira juu ya maumivu ya wenzio?

Hivi vyeti vya form four and form six ni gate passes za kuingia vyuoni, ukisha ingia unapikwa na kuiva. Yaani, mmeshindwa kuwapima pale walipo kama wameiva au hapana?. Unesi, upolisi , uganga n,k ni zaidi ya form 4. hapa watawala wameshindwa kutumia busara hili tatizo ni kubwa la kijamii kuliko mnavyofikiri. Kibaya zaidi limefanyika kiupendeleo vyombo vinavyolinda watawala vimeachwa bila kuguswa. Double standrads hii sio nzuri kwa mstakabali wa nchi yetu.
 
Kuna kasoro kubwa sana mahali na watakaoumia ni wale ambao hawana watetezi. Kama hili zoezi ni la haki na huru kwa Watanzania wote kwanini list ya wahusika wa Jeshi na Polisi nayo haiwekwi hadharani? KULIKONI?
Hata hiyo ya Jeshi ikiwekwa hadharani haiwafaidii chochote hawa waliokwisha tajwa. Maana hawa elimu zao walizopata juu ya cheti fake zinaenda kufutwa wakaanze shule upya kulingana na vyeti vyao Halisi.

Ila mkuu kama hamu yako ni kuona msiba kwa jirani kisa kwako upo endelea kusubiri Jeshini watajwe
 
Hawa ni watu wenye ujuz kabisa leo wanaondoka muhimbili pamoja na changamoto zote za utabibu zilizopo pale, MH. Ungedeal na hawa wanaonza kuingia makazini hao waliopo wangepotea wenyewe tu nje ya hapo mtaua watu pressure na pia tutapungukiwa na wataalamu hasa katika sekta muhimu kama ya afya.
Wataalam gani hao wa kufoji tunaanza upya wapo wataalam wa ukweli ma hawana ajira hao wezi wa elimu wakae tu pembeni
 
Maadam wana ujuzi kazini bas naomba waachwe. Kuna mjomba wangu aliishia la nne enzi zilee. Akawa mfagizi kwenye zahanati moja ya kimishenari inaitwa Nkinga. Kuna mzungu mmoja akampenda akawa anachukua kusogeza mikasi na kushikilia mgonjwa wakati wa oparesheni, taratibu akawa anamuelekeza kupasua. Baada ya miaka kadhaa Anko akawa mtaalamu wa upasuaji na ile zahanati ikakuwa na kuwa hospitali kubwa na maarufu mkoani Tabora na mikoa mingine . Na anko akajulikana kama daktari bingwa wa upasuaji. Hadi anastaafu dokta John alikuwa ni mpasuaji mbobezi japo hakuwahi kuingia darasani. Wanaoijua Nkinga hospitali watakuwa wanamjua!
 
Dunia nzima wanakubaliana ya kuwa Elimu ni muhimu sana na pia tunatakiwa kutambua kuna Elimu nje ya kuta nne za darasa, kuna Elimu za aina nying sana lakini Elimu bora kuliko zote ni Elimu ya Maarifa au Ufahamu ambayo inapatikana kupitia Experience. Ndio maana Dunia nzima hakuna kazi inayotangazwa kwa sasa kusiwepo kipengere cha Experience so kutambua umuhimu ya Elimu hii pia ni muhimu sana

Leo ukiangalia waliofukuzwa wengi ni kutokana na vyeti vya O &A level sasa niambie kuna mtaalamu gani anazalishwa kuanzia form 1-6?

Pia jambo hili ni aibu sana kwa nchi madhara yake hayawezi kuonekana sasa lakini nataka kukwambia Watanganyika mnakwenda kuonekana ni watu wenye Mifumo ya Elimu ya kimagumashi mifumo ambayo mtu anaweza kufoji cheti au kuchukua cheti cha mtu mwingine nakuendelea na Elimu ya juu watu wanajiuliza kama zaidi ya watu 10000 tena ni kada mbili tu Afya na Elimu bado kwingine wameweza kudanganya Serikali yenye Necta na TCU je itakuwa mashirika na taasisi ambazo hazina vitu hvyo ajira za taasisi na mashirika ya kimataifa zinakwenda kuwa ngumu sana kwa Watanganyika soon
Natambua mkuu kwamba experience ni muhimu.Ila experience ije baada ya kujua kilicho nyuma ya pazia au kujua the theory behind what you are doing,hii inaongeza efficiency.Halafu mkuu jiulize,anayekufanya wewe uwe na experience ni nani?Nadhani ni mtu aliyesomea hiyo fani.Sasa tukisema experience inatosha,hiyo experience itapatikanaje bila wasomi wakui-impart?Huoni kwamba ni kitendawili.In addition mkuu experience pekee inaweza kusaidia kiasi fulani in some areas,lakini sio kila sehemu.Na hata huko ambako experiece peke yake inaweza kusaidia,ili kuongeza efficiency,lazima mtu awe na appropriate education and certificates.Sasa mkuu utaniambia kweli kwamba "kuunda'' simu (sio kutengeneza)unahitaji experience peke yake au kuzalisha variety ya Mpunga you only need experience,nadhani itakuwa kichekesho.Kila eneo linahitaji elimu mkuu,tusijidanganye.Na kama tunaweza kuwa na mtu ambaye ana elimu na experience,kwa nini tu opt for one with only experience,I think it doesn't make sense.
 
Natambua mkuu kwamba experience ni muhimu.Ila experience ije baada ya kujua kilicho nyuma ya pazia au kujua the theory behind what you are doing.Halafu mkuu jiulize,anayekufanya wewe uwe na experience ni nani?Nadhani ni mtu aliyesomea hiyo fani.Sasa tukisema experience inatosha,hiyo experience itapatikanaje bila wasomi wakui-impart?Huoni kwamba ni kitendawili.In addition mkuu experience pekee inaweza kusaidia kiasi fulani in some areas,lakini sio kila sehemu.Na hata huko ambako experiece peke yake inaweza kusaidia,ili kuongeza efficiency,lazima mtu awe na appropriate education and certificates.Sasa mkuu utaniambia kweli kwamba "kuunda'' simu (sio kutengeneza)unahitaji experience peke yake au kuzalisha variety ya Mpunga you only need experience,nadhani itakuwa kichekesho.Kila eneo linahitaji elimu mkuu,tusijidanganye.Na kama tunaweza kuwa na mtu ambaye ana elimu na experience,kwa nini tu opt for one with only experience,I think it doesn't make sense.
Ndugu tunapozungumzia Elimu ambayo inazalisha wataalamu ni Elimu ya juu na tatizo ambalo wengi limewakumba ni vyeti vya O & A level ambapo ni Elimu ambayo ni kama basics ya kile utakachokikuta mbele kielimu. Hakuna wataalamu wanaozalishwa kuanzia form 1-6 pia utakubaliana na mm kuwa pamoja na Elimu ya darasani kuna Elimu nyingine nje ya kuta nne za darasa ambayo ni Elimu ya Ufahamu au Maarifa ambayo inapatikana through Experience kitu ambacho wengi waliofukuzwa kazi tayari Elimu hii wanayo
Mfano mm sisemi kwamba waliofoji vyeti wako sawa hapana wamekosea sana lakini pamoja na kukosea tayari hii ni Product ambayo hipo tayari kwa matumizi tofauti na leo ukiajiri watu wengine wapya. Hapa tayari kosa limeshafanyika na hii ni kutokana na mifumo ya Kielimu na ajira kuruhusu watu ambao ni Fake kuingia kwenye sehemu ya Original

Ningekuwa ni mm wala nisingefukuza Product hii, ndugu hakuna jambo gumu na baya kama kumuumiza mtu kiakili ni kufanya yule aliyefoji cheti cha form 4 akasome na yule aliyefoji cha sex naye wakasome unatoa muda wa miaka 2 kwani kuna Elimu ya QT then ni kutengeneza mfumo ambao hautoruhusu tena ujinga huu kujirudia kwani mpaka sasa hata wakifukuzwa hawa bado mfumo unaruhusu watu fake kuendelea kufoji na kupata ajira au kuendelea na Elimu ya juu, pia swala hili linakosa credibility kwa sababu limegusa watu wachache tu na wengi wameachwa
 
WARUDI DARASANI wakasome.. Muda upo bado..

tena hawa ndio wanawasemea mbovu wagonjwa.. Shubaamiti
 
Watu wengine wanatetea uzoefu, kwani kuna MTU anaingia kazini akiwa anajua kila kitu %, uzoefu ni huko huko, but ni muhimu uwe na data za ziada kichwani ambazo umezitoa katika sources tofauti. Nini maana ya kuanzia chekechea up to top, kwa hali hii ni bora serkali isingeweka exams kusudi kila MTU aingie hatua nyingine free.
 
Ndugu tunapozungumzia Elimu ambayo inazalisha wataalamu ni Elimu ya juu na tatizo ambalo wengi limewakumba ni vyeti vya O & A level ambapo ni Elimu ambayo ni kama basics ya kile utakachokikuta mbele kielimu. Hakuna wataalamu wanaozalishwa kuanzia form 1-6 pia utakubaliana na mm kuwa pamoja na Elimu ya darasani kuna Elimu nyingine nje ya kuta nne za darasa ambayo ni Elimu ya Ufahamu au Maarifa ambayo inapatikana through Experience kitu ambacho wengi waliofukuzwa kazi tayari Elimu hii wanayo
Mfano mm sisemi kwamba waliofoji vyeti wako sawa hapana wamekosea sana lakini pamoja na kukosea tayari hii ni Product ambayo hipo tayari kwa matumizi tofauti na leo ukiajiri watu wengine wapya. Hapa tayari kosa limeshafanyika na hii ni kutokana na mifumo ya Kielimu na ajira kuruhusu watu ambao ni Fake kuingia kwenye sehemu ya Original

Ningekuwa ni mm wala nisingefukuza Product hii, ndugu hakuna jambo gumu na baya kama kumuumiza mtu kiakili ni kufanya yule aliyefoji cheti cha form 4 akasome na yule aliyefoji cha sex naye wakasome unatoa muda wa miaka 2 kwani kuna Elimu ya QT then ni kutengeneza mfumo ambao hautoruhusu tena ujinga huu kujirudia kwani mpaka sasa hata wakifukuzwa hawa bado mfumo unaruhusu watu fake kuendelea kufoji na kupata ajira au kuendelea na Elimu ya juu, pia swala hili linakosa credibility kwa sababu limegusa watu wachache tu na wengi wameachwa
Nakubaliana na wewe mkuu 100% kwamba zoezi limekosa credibility kwa kuwa wengine wameachwa.Hata hivyo ni mwanzo mzuri. I do not however concur with you on the other points.

Mkuu no body really knows how much damage these guys have caused to our country,lakini kwa jinsi hali ilivyo,inaonyesha wazi kwamba uharibifu ambao wamesababisha ni mkubwa.To me atleast, it will be stupid to continue with the current situation while we know very well that these guys are part of the problem.Najua initially wakiondolewa kutakuwa na matatizo,lakini eventually tuta-catch up with the right people.We must rectify the situation quickly,hatuna muda wa kupoteza.
 
Kuna kasoro kubwa sana mahali na watakaoumia ni wale ambao hawana watetezi. Kama hili zoezi ni la haki na huru kwa Watanzania wote kwanini list ya wahusika wa Jeshi na Polisi nayo haiwekwi hadharani? KULIKONI?

Ili kujua kwanini list ya wahusika wa Jeshi na Polisi nayo haiwekwi hadharan mwulize rafiki au ndugu ambaye ameajiriwa huko akwambie mchakato aliopitia kupata ajira.
 
Back
Top Bottom